Vitengo vya habari viwe makini katika video na picha za Rais zinazotumwa kwa jamii

Vitengo vya habari viwe makini katika video na picha za Rais zinazotumwa kwa jamii

Jana nimeona clip ya mh rais wetu mpendwa mheshimiwa ukht Samia kuhusu taarifa ya kifo cha mzee Mwinyi

Clip ile inamakosa yamejitokeza ambayo mh rais hakupenda yafike kwa jamii lkn yamefika. Wakosoaji wa kisiasa wanatumia fursa hio
Ushauri

Taarifa kama zile zisiwe live zirkodiwe zieditiwe ndio ziletwe kwa jamii. Zipo software nyingi za video editing. Wapo vijana wengi wamesoma audio and video production, wamesoma adobe photoshop, premium and software nyingi za picture , audio and video tuwajiri vijana hawa ili tuimarishe kitengo cha habari Ikulu.

Neno moja la rais wa nchi ni thamani kubwa na sisi watu wa research huwa tunalitumia ktk literature review zetu.

Kwa hivyo vitengo vya habari viwe makini ktk video na picha za mh rais zinazotumwa kwa jamii.

Mambo kama haya ktk baadhi ya nchi mkuu wa kitengo anawajibika kwa kujiuzulu kutokana na kasoro.
Without prejudice ingawa ilikuwa ni live lakini nahisi rais amedhalilishwa.

Tumsitiri kwenye hili
 
Alichoongea mtoa mada ni sahihi siyo kwamba hao watu hawapo ili kuwajibika ndiyo kibarua kizito kwao hawajui majukumu yao
Walipata vipi hizo nafasi za kufanya kazi ofisi nyeti kama majukumu yao hawayajui!?
 
Yaani kuna makosa na husemi???
Haya tuache hilo, hivi kwa fikra zako timamu ikulu haina wataalamu wanaozijua hizo software vyema??

Aisee unajiaibisha, hivi unadhani production zote za Rais zinafanywa na nani?
Lazima uandike kwa hasira? Umekunywa chai lkn?
 
Wewe unaetumia masaa mengi kuangalia tv tujulishe sisi tusioangalia tv Mara kwa Mara ni nini uliona .
 
Wewe unaetumia masaa mengi kuangalia tv tujulishe sisi tusioangalia tv Mara kwa Mara ni nini uliona .
Hujafahamu? Inaonekana mwalim wa std 1 akipata shida sana wakati anakufundisha jadweli
 
Sasa wanawateua watu huko upande wa media wanawaokota mitaani
Kujuana jana,unategemea nini!

Ova
 
Walipata vipi hizo nafasi za kufanya kazi ofisi nyeti kama majukumu yao hawayajui!?
Wewe unaongea kama vile huijui vizuri hii nchi kwenye maswala ya utumishi umma, nakwambia kama kuna nchi ambayo inaongoza kwakua na watumishi wengi ambao ni incompetent basi ni Tanzania.

Kila idara imejaza watu wajingawajinga tu, huko kwenye afya zimeenda mpaka division four za 28, Police ndio imejaa uozo wa failures, wanasiasa wenyewe elimu ni za kuungaunga wakiongozwa na kiongozi wao mkuu, mawaziri, wabunge na wengine wengi.

Unashangaa nini kusikia kuwa ikulu kuna watu wasiojua kutumiza majukumu yao, ikiwa kigezo cha kwanza ni kuwa UVCCM?
 
Mleta mada saafi sana. Akili kubwa.

Umeonesha upatani wa kiakili na kimantiki.

Nnaona wengi wanakuomba clip hiyo

USIILETE!

Kaa hivyohivyo, umepatia kabisa maana ukiisambaza na wewe utakuwa umejipinga kiotomati.

Lengo libaki kuwa taarifa mbovu zisisambae, zisisambazwe kamwe
Mimi mwenyewe nnayo na siiweki humu,Acha watu waendelee kupingapinga

Ova
 
Watanzania tunapenda kuleta mijadala kwenye mambo ya kipuuzi puuzi tu, kwenye matangazo ya Live suala la kukosea sio kitu cha ajabu, Tangu lini uliona taarifa ya Kifo cha mkuu wa serikali ikitolewa ikiwa recorded??!! Tujifunze kujadili hoja za msingi na sio kudandia kila mada kwa mihemko
Uko sahihi ni vitu vya kawaida huwa vinatokea. Hata kwa rais wa marekani ilishatokea.
 
Marekani ndio nani? Marekani washaruhusu ushoga? Marekani isiwe role model wetu
Hata hujui ni kitu gani hadi nikasema hivyo? Maana issue za teknolojia si ndizo zimewekwa hapa kuhusu sijui adobe photoshop au malaria imepanda kichwani?
 
Watanzania tunapenda kuleta mijadala kwenye mambo ya kipuuzi puuzi tu, kwenye matangazo ya Live suala la kukosea sio kitu cha ajabu, Tangu lini uliona taarifa ya Kifo cha mkuu wa serikali ikitolewa ikiwa recorded??!! Tujifunze kujadili hoja za msingi na sio kudandia kila mada kwa mihemko
Kwani ikiwa recorded wewe utajua? Mbona jambo la kawaida. Hujasoma ethics za media. Utakuja humu ukiwa umejaa usingizi
 
Ile ilikuwa mubashara, wangeifuta vipi sasa?
Kwamba raisi alishindwa kusoma kilichoandikwa au kilichoandikwa hakikuhaririwa? Nashindwa kuelewa.
 
Sema ukijua vingi nayo ni shida sana, mbona me naona fresh tu.
 
Back
Top Bottom