Nchi iko kifungoni tayari.laa! Sasa taarifa za nje tutazipataje?
Kama sheria ndiyo zinasema hivyo ... wao walikuwa wapi siku zote mpaka leo. Au hili ndiyo kosa la kwanza la aina yake kutokea Tanzania....!!?Matakwa ya sheria,huo ndiyo utawala wa sheria mnazolilia kaa kimya.
Tatizo ni Lissu! Na hii ni kuvitisha vyombo vingine vya habari!Kama sheria ndiyo zinasema hivyo, wao walikuwa wapi siku zote mpaka leo. Au hili ndiyo kosa la kwanza la aina yake kutokea Tanzania....!!?
Unamlenga Lissu ambaye habari zake nyingi tunazikia kupitia BBC, DW, VOA, n.k. Vyombo vya ndani vya habari vinaogopa kurusha habari zake.kwamba wametengeneza kanuni ambazo zinaelekeza masuala hayo. huu uoga sijui unalenga nini
Wanajua baada ya mgomo nini kitawatokea.Wakuu nawasalimu,
Uhuru wa vyombo vya habari umedidimia kama sio kufa kabisa kuanzia magazeti,radio na Televisions hali ni mbaya sana vyombo vya habari havina sehemu ya kupumulia vimebanwa kila kona faini kila kukicha,kufungiwa na vingine kufutiwa usajili kabisa mbaya zaidi wanahabari wanapotea mfano Azory,Tasnia ya habari kwa sasa inapitia wakati mgumu sana nawashauri wamiliki wa vyombo vya habari wote wakutane waitishe mgomo wasitoe huduma ili kushinikiza wakandamizaji kuacha uhuni wanaoufanya kwa sasa
Hakuna utumwa mbaya kama kunyimwa uhuru wa kupata habari. Hawataki tusikie watu wanavyohangaishwa na Covid-19 duniani; hawataki tusikie habari za Tundu Lissu, n.k? Hawa watu ni wa TZ. au vipi?Kazi ipo.
Atatoka tu kama Abacha alivyotoka kwani hakuna aliyeamini wakati ule kuwa Abacha utawala wake wa kiimla ungekoma ghafla kivile.Ukishaona kwenye nchi kuna sheria zinazotungwa kufuata tabia binafsi ya kiongozi wa nchi, ujue itakuwa vigumu kiongozi huyo kutoka madarakani, na sio kutoka tu, bali kutoka kwa amani.
Kwa ufupi ni kwamba wamefungia matangazo ya nje kuingia ndani. Full stop. Joto la Lissu limewafanya wameingia mtegoni wamenasa tena kwa Mabeberu. Yaani hapo wameanzisha ugomvi wazi wazi dhidi ya BBC na sio Redio free.TCRA wakiongea na vyombo vya habari vya Tanzania wamesema ni marufuku vyombo vya ndani kujiunga ma vyombo vya habari vya nje kama BBC, DW au VOA bila kuwa na kibali kutoka TCRA.
Pia vhombo ambacho kitakuwa kinarusha matangazo hayo na chombo hicho cha nje kikatoa maudhui ambayo wao TCRA wataona yanakiuka sheria za nchi basi chombo hicho cha ndani kitawajibishwa.
Dotto Bulendu akipata muda aje atugafanulie maana ndio alikuwa anahojiwa na DW mchana huu
Usiniambie kumbe TV na computer zilishawahi pigwa marufuku? Basi ndio haya haya ya enzi za mwalimu.
Balaa hili.Niliwahi kusikia TV ilikuwa kwa Nyerere tu, huku akiwalaghai wananchi kwa taarifa za mbele kuwa ameoteshwa kama nabii!!
Hiyo sentensi ya kwanza ni swali au mshangao? Kwa sababu naona alama ya swali, basi pata jibu kwenye ukurasa wa kwanza (namba za Kiarabu), paragraph ya tatu kutoka chini ndani ya document ya serikali yenye link https://www.tanzania.go.tz/egov_uploads/documents/ictpolicy2003_sw.pdfUsiniambie kumbe TV na computer zilishawahi pigwa marufuku? Basi ndio haya haya ya enzi za mwalimu.