Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

Vituo vya utangazaji vyatakiwa kuomba kibali TCRA kurusha matangazo ya Vyombo vya Habari vya Nje

laa! Sasa taarifa za nje tutazipataje?
Nchi iko kifungoni tayari.

Sugu alipofungwa alisema " wanashangaa yeye kufungwa physically wakati nchi ilikuwa gerezani mentally "

Tumehama kutoka mental restraint sasa tumeingia kwenye physical and situational restraint.

Tuna kila sababu sasa ya kumuondoa Magufuli madarakani.
 
Wakuu nawasalimu,

Uhuru wa vyombo vya habari umedidimia kama sio kufa kabisa kuanzia magazeti,radio na Televisions hali ni mbaya sana vyombo vya habari havina sehemu ya kupumulia vimebanwa kila kona faini kila kukicha,kufungiwa na vingine kufutiwa usajili kabisa mbaya zaidi wanahabari wanapotea mfano Azory, Tasnia ya habari kwa sasa inapitia wakati mgumu sana.

Mfano Azam tv walipost video Lissu akichukua fomu wakatishwa wakazifuta haraka,radio free kutakiwa kujieleza sababu tu wanajiunga BBC na Dw nawashauri wamiliki wa vyombo vya habari wote wakutane waitishe mgomo wasitoe huduma ili kushinikiza wakandamizaji kuacha uhuni wanaoufanya kwa sasa.
 
Wakuu nawasalimu,

Uhuru wa vyombo vya habari umedidimia kama sio kufa kabisa kuanzia magazeti,radio na Televisions hali ni mbaya sana vyombo vya habari havina sehemu ya kupumulia vimebanwa kila kona faini kila kukicha,kufungiwa na vingine kufutiwa usajili kabisa mbaya zaidi wanahabari wanapotea mfano Azory,Tasnia ya habari kwa sasa inapitia wakati mgumu sana nawashauri wamiliki wa vyombo vya habari wote wakutane waitishe mgomo wasitoe huduma ili kushinikiza wakandamizaji kuacha uhuni wanaoufanya kwa sasa
Wanajua baada ya mgomo nini kitawatokea.
 
Ukishaona kwenye nchi kuna sheria zinazotungwa kufuata tabia binafsi ya kiongozi wa nchi, ujue itakuwa vigumu kiongozi huyo kutoka madarakani, na sio kutoka tu, bali kutoka kwa amani.
Atatoka tu kama Abacha alivyotoka kwani hakuna aliyeamini wakati ule kuwa Abacha utawala wake wa kiimla ungekoma ghafla kivile.
 
TCRA wakiongea na vyombo vya habari vya Tanzania wamesema ni marufuku vyombo vya ndani kujiunga ma vyombo vya habari vya nje kama BBC, DW au VOA bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Pia vhombo ambacho kitakuwa kinarusha matangazo hayo na chombo hicho cha nje kikatoa maudhui ambayo wao TCRA wataona yanakiuka sheria za nchi basi chombo hicho cha ndani kitawajibishwa.

Dotto Bulendu akipata muda aje atugafanulie maana ndio alikuwa anahojiwa na DW mchana huu
Kwa ufupi ni kwamba wamefungia matangazo ya nje kuingia ndani. Full stop. Joto la Lissu limewafanya wameingia mtegoni wamenasa tena kwa Mabeberu. Yaani hapo wameanzisha ugomvi wazi wazi dhidi ya BBC na sio Redio free.
 
Hili la kuzuia hizi redio za majuu kuungana na local radio stations za hapa kusudi kuwanyima wapinzani jukwaa la kushushia nondo zao kwa utawala wa Magufuli naona kama ni kazi bure tu vile.

Wanachoweza kufanya hizi redio za nje ni kurejea tu tena kwenye urushaji wa matangazo kupitia masafa ya kati (Short Wave) na mchezo unaishia hapo.

Serikali hii haina namna ya kuweza kuzuia matangazo ya redio ktk masafa hayo. Siku ya kufa kwa nyani ikiwadia hakuna mti atakaopanda usitereze.

If you're a fool try also to be smart even for a little bit.
 
Serikali ya kishindo inayojinasibu kupendwa na wanyonge, hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom