Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

.....
......mifuko ya jamii kama NSSF wangewekeza huko kwaajili ya wazawa haswa mahoteli ....ili wabongo angalau waonye matunda
Hili linawezekana ila hii kazi risk yake ni kubwa sana sidhani kama mifuko hii itakubali..
Na lingine vionhoinwetu hawatakubali .. Wanapenda wageni ili wawe wanaenda kuchukua %
 
....
.....Well Noted Mkuu

hilo la KADI linakimbiza kabisa utalii wa ndani target yao ilikuwa wazungu tu ...TANAPA pitieni huu uzi ...THEY should have the "ocean brain" Watanzania kwanza wengine baadaee...

Asante Mkuu kwa mchango wako ....
 
Hili linawezekana ila hii kazi risk yake ni kubwa sana sidhani kama mifuko hii itakubali..
Na lingine vionhoinwetu hawatakubali .. Wanapenda wageni ili wawe wanaenda kuchukua %
....
.......Mkuu wanajenga hoteli za kawaida tu kama za huku mtaani self safii tu na kozikodisha kwa wazawa kuziendesha Mangi watu watakwenda
 
Mkuu


Mkuu nashukuru kwa heshima uliyonipa kuhusu kesi kwa sasa niko kwenye mchakato wa kutoa kitabu, nitawajulisha kikitoka.
Kuhusu mada husika natarajia pia mchango wako hapa.
Watanzania wengi pamoja serikali yetu tunaamini kuwa kwa sababu tuna Simba, Faru,Twiga, Tembo, Mbwa mwitu na Fisi Chui Simba pamoja Nyumbu basi wanadhani watakii dunia nzima watahangaika ili waje Tanzania watazame sura za wanyama wakila majani.

Watalii hawana haja na sura ya Nyumbu wa Simba wala Tembo wai wanataka kuona mazingira ya kuvutia yaliyo tofauti na mahali pengine na kuwe hamna usumbufu.

Mkuu nadhani mchango wangu kiduchu huu.
 
Ngorongoro zipo nyumba za kulala wageni kwa bei reasonable kabisa. Sijui Serengeti sijafika mda sasa. Changamoto ya utalii wa ndani ni bei kali sana kurent gari zuri kukupeleka mbugani, hapa watanzania wengi hawamudu. Kingine tozo kwa waTz.....mimi sikubaliani kulipa zaidi ya 11,000 kwa kichwa kwa mTz. Hii ni tozo Ngorongoro, Manyara nako tozo kwa kichwa ni juu. Nasema hivi kwasababu miaka michache imepita ilikuwa 1,500 tozo kwa mTz ikapanda 5,000 sasa hivi ndiyo wameamua iwe 11,500 Huwasielewi wanatumia vigezo gani? High season? Ku-discourage mass tourism au ni nini? Utalii wa ndani utakuwa unafanywa na elites tu.....vinginevyo unatakiwa ujipange kwelikweli kuona wanyama na madhari nzuri ya nchi yako ambayo unaamini hakuna mwenye hati miliki nayo.
 
NASHAURI WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII NA WAKURUGENZI WAKE WAWE WANACHAGULIWA KWA KUFANYIWA INTERVIEW NA MCHUJO KUTOKANA NA TAALUMA ZAO KAMA ZINAKIDHI HADHI YA UHIFADHI,WAAJIRIWE KWA MIKATABA MAALUMU.

NASHAURI PIA WADAU WA SEKTA HII WAHESHIMIWE HUSUSANI WAZAWA KWANI NDIO WANAOITANGAZA NCHI VYEMA,HAKI ZAO ZILINDWE NA ZIBORESHWE,HIZI KAMPUNI NDOGO NDOGO ZINAPENDWA SANA NA WAGENI NA NDIO WAFANYA MARKETING WAZURI SANA NA KUITANGAZA TANZANIA,MSIWADHARAU SIO JAMBO DOGO HILI,IKIBIDI UUNDWE UMOJA WAO NA MAMLAKA YA MAPATO IHUSUSHWE ILI KUWALINDA KATIKA COMFLICT OF INTEREST

NASHAURI SERIKALI IPIGE MARUFUKU BAADHI YA MAKAMPUNI MAKUBWA MALIPO YA WAGENI KUFANYIKA NJE YA NCHI,KWANI KINACHOTUMWA HUKU NI HELA YA DIESEL NA PARK FEES TU,MALAZI NAKADHALIKA NYINGI HUBAKIA KULEEEE NA MKIONA LODGES NA MAKEMPU YAMEJAA MJUE 1.5 HELA IPO LONDON AU BOMBAY NYINGINE NI HIZI KAMPUNI NDOGONDOGO WAMELIPIA LIVE AMBAZO TOKEA ANAPOKEA MGENI KIA MPAKA ANA MRUDISHA KIA BAADA YA SAFARI AMESHA KOMBWA KAFAIDA CHAKE HUKO NJIANI EITHER NA TRAFIKI AU WENGINEO! NASISITIZA UUNDWE UMOJA WAO
 
....

NASHAURI SERIKALI IPIGE MARUFUKU BAADHI YA MAKAMPUNI MAKUBWA MALIPO YA WAGENI KUFANYIKA NJE YA NCHI,KWANI KINACHOTUMWA HUKU NI HELA YA DIESEL NA PARK FEES TU,MALAZI NAKADHALIKA NYINGI HUBAKIA KULEEEE NA MKIONA LODGES NA MAKEMPU YAMEJAA MJUE 1.5 HELA IPO LONDON AU BOMBAY NYINGINE NI HIZI KAMPUNI NDOGONDOGO WAMELIPIA LIVE AMBAZO TOKEA ANAPOKEA MGENI KIA MPAKA ANA MRUDISHA KIA BAADA YA SAFARI AMESHA KOMBWA KAFAIDA CHAKE HUKO NJIANI EITHER NA TRAFIKI AU WENGINEO! NASISITIZA UUNDWE UMOJA WAO

Dublin
 
Hongera Sana wenye kuelewa wataelewa hasa viongozi WA maliasili
Tuna Kila sababu ya kuwa matajir tatizo viongozi wabovu hii sekta unaweza tamani kujifukia ukiwaza yule wazir jina kapuni anamchukua bongo movie aunt kutangaza utalii....tembo wameuwawa had inatia Huruma..twiga hadi airport wanasafirishwa...mlima Kilimanjaro watalii wanapitia Kenya....Tanzanite ndo usiseme

Tumekalia kiti cha gold ila tunaomba kila uchao hii sekta ingekuwa Na wazalendo tungekuwa Na pato kubwa Sana la pesa tunaingiza
 
Hiii sector ya utaliii inahitaji apace overhauling kuanzia kwenye management mpaka infrastructures, ni swala la aibu sana nchi kama Tanzania kuzidiwa na majirani kwa gap kubwa sana kimapato hiliali hao majirani wanatumia hizo hizo rasilimali zilizopo Tanzania.
 
Wakati fulani nilikuwa naongea na mmiliki wa kampuni ya utalii kutoka nchini Kenya, akaniambia kwamba kule kwao baada ya kuandamwa na Alshabaab walianzisha kampeni maalum waliyoiita TEMBEA KENYA, Hii kampeni ilianzishwa na serikali yao ili kulinda ajira za wafanyakazi katika sekta ya utalii ambayo iliyumba kiasi cha kutishia ajira za wafanyakazi wengi nchini humo katika sekta hiyo.

Makampuni mengi ya utalii zikiwemo hoteli zilipunguza gharama za safari za utalii na mahoteli pamoja na camps zilipunguza pia gharama za malazi na chakula kwa wazawa na wananchi walihamasishwa kufanya utalii wa ndani ambapo kulikuwa na muitikio mkubwa na serikali katika kuunga mkono kampeni hiyo ilichangia wafanyakazi katika sekta mbalimbali kufanya utalii wa ndani na mikutano na makongamano yalihamishiwa huko ili ku generate revenue katika makampuni ya utalii na mahoteli.

Kampeni hiyo ilipelekea kuzaliwa kwa Kampuni ya Bonfire homepage ambayo ilianzishwa na wajasiriamali wadogo mtu na mkewe bila mtaji mkubwa ambao walianza kwa kuuza safari za utalii kupitia mtandao wa facebook.

Wajasiriamali hawa walianza kwa kupatana na Mahoteli yaliyoko kwenye mbuga za wanyama na camps na ku book vyumba vingi kwa mpigo kisha kuviuza kwa mtindo wa groups kwa gharama nafuu na kuhamasisha wazawa kulipa kidogo kidogo kabla ya safari na hapo mtu anajihakikishia safari yake ya kutalii kwa gharama nafuu zilizopunguzwa kutokana na kuuzwa kwa vyumba vingi kwa mpigo.

Hivi sasa kampuni hiyo ni kubwa na ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini humo na sasa imevuka mipaka ambapo sasa inauza safari za nje kama Dubai na nchi za ulaya na Marekani jambo ambalo imejijengea sifa na kutwaa tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya Qatar Aiways kutokana na manunuzi ya tickets kwa shirika hilo.

Hii ni changamoto kwa nchi yetu kuruhusu wajasiriamali wadogo kujiingiza kwenye biashara hii kwa kuuza safari za utalii kwa njia ya mitandao ya kijamii ili kujiongezea kipato na kujiimarisha kiuchumi. Tunaweza kuiga wenzetu waliafanya nini kwa mfano tunaweza kujifunza kupitia Kenya na Afrika Kusini.

Iwapo kutawekwa utaratibu mzuri wa kupanua wigo wa wafanyabiashara wa utalii hakika serikali itakusanya fedha nyingi sana za kodi na hivyo uchumi wetu kukua kwa kiwango cha ajabu.

Ombi langu kwa wizara ya Utalii.

Naomba wapitie uzi huu na kuchukua mawazo mazuri ya wadau na kuyafanyia kazi ili nchi yetu isonge mbele. Hii ni nchi yetu sote na tuna wajibu kama wananchi kuishauri serikali ili kujenga uchumi imara utakaonufaisha serikali na wananchi wake na vizazi vijavyo.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
 
Jambo lingine ni elimu kwa umma, Wa TZ wengi hawajui umuhimu wa kutembelea mbuga zetu za wanyama na gharama za utalii kwa wazawa zipunguzwe ili kuwavutia Watanzania wengi kutembelea vivutio hivi.

Kuna wakati nilisikia Benki moja nchini ikitangaza kwamba imeandaa safari za wafanyabiashara kwenda nchini china kibiashara na gharama zilikuwa resonable kabisa kwa safari na malazi. Hili lingeweza kufanyika pia kwa safari za Utalii. Mabenki yangekuja na wazo hilo kwa kuwahamasisha wateja wao kulipa kidogo kidogo kwa safari za utalii wa ndani kipindi cha Low Season ambapo gharama za safari na hoteli hupungua sana. Hii itawawezesha kutengeneza faida na pia kuongeza wateja.
 
Maoni yangu vyuo vinavyojiita vya utalii vilivyoko vichochoroni vihakikiwe kwani hivi ndivyo vinavyozalisha vibarua badala ya kutoa taaluma stahiki inayoendana na ukuaji wa sekta ya utalii.

Hivi sasa kuna utititri wa vyuo ambavyo hata mitaala yao ni ya hovyo na vifaa vya kufundishia hawana zaidi ya kutoa mafunzo ya nadharia kwa miezi mitatu na kuwasukumia wanafunzi kwenye mahoteli ili kupata uzoefu wakati hata taaluma yenyewe ni ya mashaka matupu.

Hivi vyuo navyo ni Jipu inabidi vitumbuliwe.
 
Kuweka kumbukumbu sawa:

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MHESHIMIWA ESTHER NICHOLAS MATIKO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA BAJETI WA MWAKA 2015/16 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

SEKTA YA UTALII

HOTELI ZA KITALII NDANI YA HIFADHI


Mheshimiwa Spika, takribani 80% ya watalii wanaoingia nchini hulala katika hoteli mbalimbali zikiwemo za ndani ya hifadhi. Licha ya hoteli za ndani ya hifadhi kuchangia kiasi kikubwa cha mapato ya Wizara hii, hoteli hizo zimekuwa na changamoto nyingi jambo linaloathiri ufanisi wake na mapato yatokanayo na hoteli hzio.

Mheshimiwa Spika, ndani ya hifadhi kuna hoteli za wawekezaji wazawa na zile za raia wa kigeni. Lakini hoteli za wazawa zimekuwa zikikumbwa na changamoto kubwa sana. Mathalani wakati wa msimu wenye wateja wachache (low season) hoteli za wawekezaji wa kigeni hutenga vyumba yaani hufanya “block booking” kwa wageni wao katika hoteli hizo za wazawa kwa kipindi cha muda mrefu na kwa gharama ndogo (low price), hivyo basi inapofika kipindi cha msimu wenye wateja wengi (high season) tayari unakuta hoteli hizi za wazawa zinakuwa haziwezi tena kuuza vyumba hivyo na hawawezi tena kufaidika na bei za high season kwa kuwa vyumba hivyo vinakuwa vimeshachukuliwa (blocked). Aidha; changamoto nyingine ni kwamba; fedha hii inayokuwa imelipwa kwa vyumba hivi vya hoteli za wazawa ni ndogo na inakatwa kodi kubwa , lakini Hoteli zile za wawekezaji wageni hupokea wageni wengi kwa kipindi hicho cha high season kwa bei kubwa na huwa haikatwi tena kodi.

Mheshimiwa Spika , pamoja na hayo, imekuwa ni vigumu sana makampuni madogo ya utalii kuweza kumudu soko la ushindani kwa kuwa vipaumbele vya kupata vyumba vya hoteli kwa ajili ya kulaza wageni kutolewa kwa makampuni makubwa pekee na zaidi yale ya kigeni. Hii inasababisha makampuni madogo ya ndani kushindwa kuhimili soko la ushindani na mengi hufilisika kabisa. Suala hili sio tu linaua hoteli za wazawa hapa nchini bali pia linaisababishia serikali hasara kubwa ya kupoteza mapato.

Mheshimiwa Spika, Nchi hii ina Tume ya Haki ya Ushindani (Fair Competition Commision) ambayo imebainisha wazi katika tovuti yake kwamba: “FCC has a mandate to regulate the competitive market. “FCC deals with all issues of anti- competitive conduct, abuse of dominance and has provision for curtailing merges and acquisitions if outcomes are likely to create dominance in the market or lead to uncompetitive behavior”

Mheshimiwa Spika, kwa tafsiri rahisi kabisa ni kwamba tume hiyo ina mamlaka ya kuhakikisha kunakuwepo na kiwango cha uadilifu miongoni mwa washindani katika masoko. Hivyo basi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuhakikisha jambo hili linatafutiwa ufumbuzi kwa kuwa ni wajibu wa serikali kunusuru makampuni haya ya wazawa ili kuweza kumudu soko la ushindani wa kibiashara. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutumbua pia majipu katika eneo hili ambapo wawekezaji katika hoteli za hifadhini wamekuwa wakiwanyonya wawekezaji wazawa na hivyo kudumaza juhudi za Serikali na wananchi za kukuza uwekezaji wa ndani katika sekta ya utalii.

LESENI YA KUENDESHA BIASHARA YA UTALII (TALA LICENCE)

Mheshimiwa Spika, Licha ya hotuba ya Rais John Pombe Magufuli wakati akilizindua Bunge la kumi na moja mwezi Novemba , 2015 kueleza nia ya kuwasaidia Watanzania wanaotaka kuwekeza hapa nchini; hakuna dalili za utekelezaji wa azma hiyo ya Serikali jambo linatoa taswira kuwa kauli ile ilikuwa ni ya kisiasa tu.

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu kumekuwa na urasimu na tozo nyingi za kuendesha biashara hii ya Utalii jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wawekezaji wa ndani na hivyo kushindwa kumudu ushindani katika sekta hiyo. Mzigo mkubwa umewaelemea wafanyabiashara wadogo na wengi wao wako katika hatari ya kufunga biashara hizo kwa kushindwa kupambana kwenye soko la ushindani. Kwa mfano katika malipo ya leseni , makampuni ya nje yanalipa dola elfu tano ($5000) na makampuni ya kitanzania ni dola elfu mbili ($2000).

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani ina mtazamo kwamba hiki kiwango cha (flat rate) ya dola 200 kitazamwe upya kwa kuwa kwa kuwa kinawaumiza wawekezaji wadogo/wachanga katika sekta hiyo. Mathalani, unakuta kampuni yenye magari 5 inalipa tozo sawa na kampuni yenye magari 300. Huu ni uonevu wa hali juu kwa wafanya biashara hawa wadogo na ni kinyume na kauli ya Rais katika kuwasadia wafanyabiashara wadogo. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza tozo ya dola 1000 kwa wawekezaji wadogo . Aidha, tunapendekeza pia orodha ya tozo ipuguzwe ili kubaki na tozo chache ambazo ni nafuu ili wawekezaji wadogo waweze kumudu.

Mheshimwa Spika, Pamoja na tatizo hilo la tozo serikali inawataka wafanya biashara hawa wadogo katika sekta hii ya utalii kuwa na uwezo wa kumiliki idadi ya magari yasiyopungua matano (5) ili waweze kupata leseni. Hii inaonyesha dhahiri kuwa Serikali hii ya CCM inataka biashara ya utalii iendele kuhodhiwa na watu wachache wenye fedha nyingi jambo ambalo linaondoa dhana nzima ya uchumi shirikishi ambapo kila mtanzania anatakiwa kuwa na fursa sawa katika kujenga uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu gharama ya kumiliki gari kwa ajili ya safari za utalii mbugani ni shilingi za kitanzania milioni 120 mpaka 200. Bei ya chini kabisa ya gari ambalo limeshatumika ,kwa umbali wa kilomita 400,000 na kuendelea ni milioni 25 na kuendelea. Kwa hali hiyo, ni vigumu sana kwa mtanzania wa kawaida kuweza kumudu gharama hizo na kuweza kumiliki magari matano ili apatiwe leseni ya kufanya biasahara ya usafirishaji wa watalii.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kubadili utaratibu wa sasa wa utoaji wa lesni kwa wafanyabiashara wanaosafirisha watalii kwa kuondoa sharti la umiliki wa magari matano ndipo wapewe leseni ya kufanya biashara hiyo. Tunapendekeza kiwango cha umiliki wa magari kama kigezo cha kupata leseni kipunguzwe hadi kufikia magari mawili.

UWEKEZAJI KATIKA IDARA YA UTANGAZAJI WA VIVUTIO VYA UTALII

Mheshimiwa Spika, Biashara ya Utalii ni matangazo. Pamoja na vivutio vingi vya utalii tulivyo navyo, kama vivutio hivyo havitatangazwa ipasavyo, tusitegemee kupata watalii wa kutosha na kwa sababu hiyo tusitegemee pia kukusanya mapato ya kutosha katika sekta hiyo. Ili tuweze kunufaika katika sekta hii kwa kiwango kinachokusudiwa ni lazima kuwe na mpango madhubuti na bajeti ya kutosha kufanya matangazo ya vivutio vyetu vya utalii nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili, imeandaa mpango gani wa utangazaji wa vivutio vya utalii na imetenga fedha kiasi gani kwa ajili ya kugharamia matangazo hayo kwa mwaka mpya wa fedha 2016/17. Lengo la kuitaka Serikali kufanya hivyo, ni kuisaidia kuwekeza katika utangazaji wenye tija, isije ikawa inatumia fedha nyingi kwenye utangazaji halafu faida inayopatikana ni ndogo kuliko fedha iliyotumika kufanya utangazaji. Hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani hapa ni kuwa na uwiano kati ya fedha tunazotumia kwenye utangazaji na tija inayopatikana (proportional result between input and output).

MIUNDOMBINU KATIKA SEKTA YA UTALII

Mheshimiwa Spika, Utalii wa nchi yetu unategemea sana huduma bora katika viwanja vya ndege. Hali ya viwanja vya ndege nchini bado hairidhishi. Hali hii inaathiri mapato yatokanayo na utalii kwa kuwa ubovu wa miundo mbinu na huduma katika viwanja hivi vinasababisha vishindwe kutumika kabisa au kutumiwa na wageni wachache kutokana na hadhi zake.

Mheshimiwa Spika, Mathalani uwanja wa Kilimanjaro International Airport (KIA) hakuna taa za kutosha za kutoa ishara nyakati za usiku na ni hatari sana kwa waongoza ndege na abiria, mashine za kupokea mizigo ziko chache sana na wageni husubiri muda mrefu sana ili kupokea mizigo na hakuna maeneo maalum lililojengwa kwa ajili ya kupokea wageni. Jambo hili linaleta usumbufu mkubwa kwa wageni na hata wale wanaowapokea wageni hao.

Mfano mwingine ni kiwanja cha ndege cha Musoma kilichojengwa kwa kiwango cha changarawe na hivyo ndege nyingi haziwezi kutua. Uwanja wa Musoma ni muhimu hasa kwa wageni wanaotembelea Mkoa wa Mara kwa shughuli za utalii wa wanyama.Ni dhahiri uwanja huo ungeboreshwa ungechangamsha zaidi shughuli za kitalii kwa kuwa ni karibu na nchi jirani ya Kenya,na pia ungehamasisha wageni kutembelea kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mheshimiwa Spika, Changamoto za miundo mbinu na huduma ziko takribani kwenye viwanja vyote nchini ikiwa ni pamoja na Songwe,JKNA, Dodoma, Kigoma n.k . Athari za Changamoto hizi zilijionyesha dhahiri wakati wa mgogoro kati ya Tanzania na Kenya ambapo Idadi kubwa ya wageni waliokuwa wanakuja Tanzania walionyesha kuwa hushukia uwanja wa Jomo Kenyatta.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kuboresha viwanja hivi vya ndege ili kuvutia wageni wengi zaidi na hata wawekezaji wanaotamani kuleta ndege zao hapa nchini waweze kuwa na uhakika wa usalama wa ndege zao na abiria pia. Vilevile, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali kuhakikisha watendaji wote ndani ya viwanja hivi wanapata elimu ya namna ya kuwahudumia wateja kwa ukarimu zaidi (customer care and hospitality).

NJIA YA MALIPO KATIKA VIWANJA VYA NDEGE NA HUDUMA MBALIMBALI ZA HOTELI KWA WATALII (MODE OF SERVICE PAYMENT)

Mheshimiwa Spika, katika viwanja vyetu vya ndege na hata mahoteli ya kitalii nchini bado malipo mbalimbali yanafanyika kwa pesa taslimu (cash payment). Takribani 9.3% ya wageni wanaoingia nchini hulipa kwa kutumia credit card na 89.8% wanafanya malipo kwa njia ya fedha taslimu kwa mujibu wa ripoti ya International Visitor’s Exit Survey Report ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, nchi nyingi duniani zinatumia mfumo wa kieletroniki wa kufanya malipo mbalimbali kwa njia ya kadi yaani (credit card) . Nchi nyingi zilizoendelea hutumia mfumo huu ili kupunguza hatari za kubeba fedha nyingi ikiwa ni pamoja na kuibiwa, kupoteza n.k

Mheshimiwa Spika, wageni wanapokuja nchini hukutana na changamoto za kulazimika kufanya malipo kwa njia ya fedha taslimu ilhali wengi wao hawasafiri na fedha.Wageni hawa wanakumbana na usumbufu mkubwa wa kuchukua fedha katika mashine (ATM) ili waweze kufanya malipo. Hali hii imewafanya wageni wengi wanaoingia nchini kupata usumbufu mkubwa na kuona nchi yetu ni nchi iliyojaa urasimu.

Mheshimiwa Spika, Serikali kuendelea kuruhusu tabia ya kutumia mfumo wa kizamani wa kupokea fedha taslimu ilhali njia ya kadi ni salama zaidi kwa wageni wetu na hupunguza mianya ya wizi, ubadhirifu na hata rushwa basi huko ni kuendelea kuturudisha nyuma kusikoendana na matumizi sahihi ya mabadiliko ya kiteknolojia. Mfumo huu ukitumiwa vizuri utarasihisha kuongeza zaidi manunuzi (purchasing power) ya bidhaa zetu za kitanzania zinazouzwa katika mahoteli na maeneo mengine ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali kuanza kuwaelimisha wadau wa sekta ya utalii kujua manufaa ya matumizi ya kadi (credit card),pia kuwahamasisha kuanza kutumia mfumo huu ili kuendana na soko la utalii la kimataifa,na kuendelea na mabadiliko ya kiteknolojia duniani.

Vilevile Kambi Rasmi inaitaka serikali kuhakikisha kuwa pale mgeni anapolipia fedha za visa anapewa risiti ya kielectroniki kama ilivyo katika mfumo wa serikali unaowataka wafanya biashara wote nchini kuzitumia.
 

POINT HII---

Mfano..Leopard Tour ni Kampuni kubwa ya Mhindi, pia anapewa bei rahisi zaidi na Hotel & Lodges (Mhindi) anaendesha.

Sopa Lodges nazo za wahindi

Leopard owner ni Makamu mwenyekiti TATO
 
serikali yetu haina mazingira rafiki kwa sisi wazawa tunaotaka kuendesha biashara hii hapa nchin zaidi ya kuendelea kuwapigia magoti hawa wakubwa.
 
serikali yetu haina mazingira rafiki kwa sisi wazawa tunaotaka kuendesha biashara hii hapa nchin zaidi ya kuendelea kuwapigia magoti hawa wakubwa.
Ndiyo tuseme sasa hapa kwamba nini kifanyike?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…