Vyuo Vikuu 2 vya Tanzania ndani ya Top 10 kwa Ubora wa Elimu Kusini mwa Jangwa la Sahara. UDSM haimo

Vyuo Vikuu 2 vya Tanzania ndani ya Top 10 kwa Ubora wa Elimu Kusini mwa Jangwa la Sahara. UDSM haimo

Sawa tu wewe dunia ya leo degree holder ajui kutumia email unadhani nini kinafuta hapo dunia ya leo bado assignment mnafanya kwenye magroup haaa haaaa
 
Yaani UDSM imekuwa ya hovyo Sana siku hizi,Generali Ulimwengu alisema "sikuhizi UDSM imekuwa form ten" yaani chuo kinampangia mtu namba ya kugikiri.
UDSM miaka hiyo mambo sensitive ya nchi Yalikuwa yananzia pale kupingwa au kuungwa mkono kwa hoja,rejea kipindi Cha Akina Samweli Sita waanzilishi wa Revolution Square darajani kwenda hall 5.
Tangu Prof Mkandala aachie ngazi chuo kimeendelea kudolola.No research za maana,no hot discussion,kupungua kwa idadi ya waandamizi(senior academician) kama akina Prof Shivji,Mbonile n.k,,,siku hizi wanaopiga lecture ni vijana wanaosomea masters,na Hawa ndio wanaendekeza sana ngono na wadada ilikupata maksi.
Jitihada za Makusudi zifanyike kuokoa chuo hiki,binafsi nilijivunia kusoma UDSM ilivyokuwa na hadhi yake,miaka hiyo wanachuo wanaargue kweli na migomo Kwa kwenda mbele.
Niliingia UDSM mwaka 1974.Wakati huo, it was the only University in Tanzania.Kulikuwa na Campuses mbili,Morogoro Campus ambayo leo ni SUA na Muhimbili Campus.Oh,my goodness,UDSM ilikuwa inaheshimika worldwide.Leo dah,imekuwa laughing stock,inasikitisha sana.

Hata hivyo nadhani niseme hivii,tutainyoshe vidole UDSM,lakini frankly,sio UDSM peke yake ambayo imeoza, institutions zetu zote of higher learning ni kichekesho.Kijana aliyemaliza hata M.Sc.leo huwezi kuamini kamaliza M.Sc.Ufahamu wake hata kwenye fani aliyo-specialize,is so low.Ninao,so I know.

Siku moja nilikuwa SUA nikamsikia Lecturer mmoja ana-lecture undergraduates, nilichoka.Nikamuliza Professor mmoja rafiki yangu, is what I am hearing real?Aliniambia,"brother hiyo ndiyo hali halisi." Akaongeza, "kama Lecturer yuko hivyo,wanafunzi wakoje." Nilichoka,unajua,nilichoka!" Kwa hiyo hali ya elimu yetu ni mbaya sana.Msingi umeoza,na sina shaka yeyote kwamba it is by design,kwani mamlaka husika hazioni?.
 
Naona serikali ni kama imekitosa mazima The Hill, ambacho ndio jicho la TZ kwa higher education. Kwa mambo yanayoendelea pale, sio rahisi kufikia level za kimataifa.

First impression starts with watumishi husika ( mind set, comfortability, readiness and proudness),

Frankly speaking, watumishi hawako proud and readiness na working environment ya pale the hill.

Serikali lazima ichukue hatua haraka
Mara nyingi chachu ya maendeleo inaanzia chini; waanze kuweka wakuu wa vyuo wenye 'vision' ya kufika mbali kimataifa, wasiokuwa na element za kisiasa; hawa wanaweza wakashauri kitu ambacho ni 'positive', na mambo yakaenda vizuri.​
 
Siasa imeingia pale ukileta mawazo mbadala unatafutiwa zengwe hata enzi za mzee kifimbo paliendeshwa mijadala huru.....
 
UDSM imeharibiwa na siasa za JPM. Between 2015-2020 elimu ya vyuo vikuu na tasnia ya habari vilivamiwa na siasa za uchawa. Wasomi na wanahabari wakaanza kulamba teuzi kama hisani ya uchawa na upotoshaji. UDSM ikiaanza kuwa kichaka cha kulinda maslahi ya wanasiasa huku waandishi wa habari nao wakipoteza mwelekeo kwa vitisho na uchawa. Hadi leo hii wasomi wa nchi yetu hawana uhuru baada kuuza taaluma zao na utu wao kwa vipande vya mkate. Tumebaki kuzalisha machawa badala ya wasomi wanaoweza kutoa mawazo huru ya kusaidia nchi kupiga hatua. Sahizi hata serikali za wanafunzi vyuoni hazina uwezo wa kuzalisha viongozi wa maana zaidi ya machawa. Uwezo wa wanafunzi kitaalama umeshuka sana (mawazo ya kichawa) hawako independent katika kufikiri mana wanafundishwa na machawa. Ukiona mtu yuko independent ujue huyo anaakili ya kuzaliwa (kipaji) siyo ya kufundishwa. Mbaya zaidi serikali ya kichawa haina uwezo wa kuzalisha ajira (wasomi waliowengi wananjaa muda wote) hata waliopo kwenye ajira hawafaidi matunda ya kazi zao pasina uchawa . Sasa kwa hali hiyo ulitegemea UDSM ishike nafasi ya ngapi?.
This👉 is so stupid,"UDSM imeharibiwa na siasa za JPM. Between 2015-2020."Hatuzungumzii UDSM peke yake,we are talking of the entire education system, pamoja na UDSM,it is rotten.Sasa an entire education system iharibiwe so much within a short span of five years,si kweli,wewe unamtafuta tu mchawi.

Mimi naomba niseme hivi, uharibifu wa elimu sio issue ya Tanzania tu,it is a world-wide phenomenon na ni agenda kamili kabisa ya NWO.Nia ni mass production of fools.Agents wamesambazwa duniani kote,and have infiltrated all world governments and are already in high government positions za kubuni sera,nia ikiwa moja tu, kutimiza adhma yao ya kuharibu elimu.
 
Umemkamata huyo muongo, hamna siku hata moja chuo chochote EAC yote kimefika top 5, yeye anasema UDSM iliwahi kufika top 5.
Mwaka jana MUHAS ilitutoa tongotongo...
Au sijui walipika data

1708273317465.png
 
UDSM imeharibiwa na siasa za JPM. Between 2015-2020 elimu ya vyuo vikuu na tasnia ya habari vilivamiwa na siasa za uchawa. Wasomi na wanahabari wakaanza kulamba teuzi kama hisani ya uchawa na upotoshaji. UDSM ikiaanza kuwa kichaka cha kulinda maslahi ya wanasiasa huku waandishi wa habari nao wakipoteza mwelekeo kwa vitisho na uchawa. Hadi leo hii wasomi wa nchi yetu hawana uhuru baada kuuza taaluma zao na utu wao kwa vipande vya mkate. Tumebaki kuzalisha machawa badala ya wasomi wanaoweza kutoa mawazo huru ya kusaidia nchi kupiga hatua. Sahizi hata serikali za wanafunzi vyuoni hazina uwezo wa kuzalisha viongozi wa maana zaidi ya machawa. Uwezo wa wanafunzi kitaalama umeshuka sana (mawazo ya kichawa) hawako independent katika kufikiri mana wanafundishwa na machawa. Ukiona mtu yuko independent ujue huyo anaakili ya kuzaliwa (kipaji) siyo ya kufundishwa. Mbaya zaidi serikali ya kichawa haina uwezo wa kuzalisha ajira (wasomi waliowengi wananjaa muda wote) hata waliopo kwenye ajira hawafaidi matunda ya kazi zao pasina uchawa . Sasa kwa hali hiyo ulitegemea UDSM ishike nafasi ya ngapi?.
Huyo magufuli hatunaye tangu 2021 na hatuta kua naye anaye tuharibia UDSM tunaye mbona humsemi huyu Gagula mzurulaji kama hana ndoa
 
Walitufikisha wapi na hizo hoja na misimamo?
Halafu kipindi kile, kusoma chuo na malazi na chakula ni bure
Kwa hiyo muda walikuwa nao wakupiga soga wakiita midahalo kule nkurumah hall
Leo, mimi nijitegemee ada, kula, na malazi, saa ngapi nianze kulopokalopa, eti tuite ni midahalo badala ya kupambana na maisha, maana unayaanza tangu unasoma chuo, siku nyingine siku inapita hujala hata msosi mmoja
 
Mbrrrr mbrrr mbrrr
 
Hivi chawa maarufu JF Lucas de mwashambwa Lucas mwashambwa ana degree ya UDSM?

Mwijaku najua anayo.
😀😀😀Ndio ninayo na hata makamu mkuu wa chuo kwa sasa profesa William anangisye ni mwalimu wangu. Profesa Bernadeta Kilian aliyekuwa mkuu wa chuo kishiriki cha Elimu Mkwawa naye pia ni mwalimu wangu na wengine wengi sana .
 
Aisee boss, sijui nakupataje unipe madini kidogo kuhusu maelezo yako ktk maada hii,NWO naifaham kwa sehem lakini sijajua kama wanaagenda kama hizi.
Nakupataje mkuu at least unaweza indirect hata source za kilichonyuma ya picha hii
 
Back
Top Bottom