Waarabu kushangilia huku wakipeperusha bendera ya Tanzania inatuma ujumbe gani?

Waarabu kushangilia huku wakipeperusha bendera ya Tanzania inatuma ujumbe gani?

Hao ni Watanzania walio kwenye mji mtakatifu Iraq walipokwenda kuhiji katika miji mitakatifu ya madhehebu ya Shia ya Najaf kulipo msikiti maarufu mtakatifu na Karbala kulipo kaburi la Imam Husayn .
Tumepiga hatua kubwa sana.... Siku hizi tunasali/swali tukiwa tunapeperusha bendera ya Taifa. Kanzu, barkashia, makubazi tupa kule..
 
Kuna tofauti gani kati ya washia na Qadiani/Ahmadiyya?

Ahmadiya hawaamini MUHAMMAD kuwa mtume wa mwisho.

Ahmadia hawarusiwi kuingia makka kufanya hija wala hawarusiwi kuoa muislamu.

Wanahesabiwa kuwa sio waislamu.
 
Tumepiga hatua kubwa sana.... Siku hizi tunasali/swali tukiwa tunapeperusha bendera ya Taifa. Kanzu, barkashia, makubazi tupa kule..

IMG_4806.jpg

IMG_4807.jpg
 
Ahmadiya hawaamini MUHAMMAD kuwa mtume wa mwisho.

Ahmadia hawarusiwi kuingia makka kufanya hija wala hawarusiwi kuoa muislamu.

Wanahesabiwa kuwa sio waislamu.
Kumbe sio waislamu ila wanapenda kujitambulisha kama waislamu.
 
Ndugu mleta hii thread penda kufanya uchunguzi kabla ya kupost.[mention]Etwege [/mention]

Hao ni waislamu wa TANZANIA [emoji1241] wameenda kufanya hija nchini iraq [emoji1131] kwa kukumbuka kifo cha mjukuu wa mtume (s.a.w) anaeitwa IMAM HUSSAIN (a.s).

IMG_4805.jpg

IMG_4807.jpg

IMG_4808.jpg

IMG_4806.jpg
 
Hapo wanasema ‘hawa watu weusi wametushindwa, na hao wazee wao wa TEC pia wametushindwa’[emoji23].
 
Na muda huu ndiyo msimu wenyewe ndugu zetu toka Tanzania wapo huko kutekeleza jambo muhimu la kiimani katika miji Najaf na Karbala iliyopo Iraq.

View attachment 2741675
Waislam sijui shida huwa nini yaani hamuoni yajayo wala machungu ya baadae nyie mnaona anachofanya ni sawa tu jueni hili nyani sio mmoja walizaliwa wengi na siku ya nyani wote kufa miti huteleza usifurahi juu yangu huu uwimbo sikiliza kwa makini. Hii hali ya bandari na kuuzwa kwa nchi yako iliyohenyewa halafu mtu au watu wanaona ni fine kuharibu utaratibu haya situpo ?? Hawatawajua kisa nyie mnasali pamoja wao wanachukiaga watu weusi mbaya mbaya sana tunarudi chini badala ya juu
 
Kuna video imesambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha kundi la warabu wakishangilia na kuimba nyimbo huku wakipeperusha bendera ya Tanzania kitu ambacho kimeibua maswali mengi miongoni mwa watanzania wakijiuliza inawezekanaje?

Yani katikati ya sakata la kuuzwa kwa bandari zote za Tanganyika kwa warabu wa DP world ya Dubai alafu tena waonekane warabu wakishangilia kama wamechukua kombe kwa nini?
Kweli viongozi wetu hawaoni hili?View attachment 2741665

Mkuu ni unalipwa au ...mbona chuki za kike izo
 
DPW imefanya waarabu waogopwe na watanganyika kama chawa na kunguni ndani ya nyumba.

Mkataba ule wa bandari uvunjwe, hatuutaki kabisa, hao waarabu hata kama wanashangilia mambo yao, hapa mkataba wa DPW hatuutaki hili muelewe.

Kila muarabu sio wa dubai punguza siasa
 
heshima kwa Tanzania kwani kiongozi wa mashia Afrika mashariki na kati makao makuu yake yapo Tanzania anaitwa Shkh.Hemed Jalala kama sijakosea.

Toka maktaba:

Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Kuna video imesambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha kundi la warabu wakishangilia na kuimba nyimbo huku wakipeperusha bendera ya Tanzania kitu ambacho kimeibua maswali mengi miongoni mwa watanzania wakijiuliza inawezekanaje?

Yani katikati ya sakata la kuuzwa kwa bandari zote za Tanganyika kwa warabu wa DP world ya Dubai alafu tena waonekane warabu wakishangilia kama wamechukua kombe kwa nini?
Kweli viongozi wetu hawaoni hili?View attachment 2741665
wamejipatia linchi la bure bila kutoa senti moja! SSH we are watching you and these!!
 
😆 😂 😆 😂 hii bandari itawatoa roho
Naona hujawahi kuwaona Mashia wakiomba na hapo hawaimbi bali wana yao huku wakijipiga kifuani
Hebu Google Shia wanavyojipiga kifuani hao ni Iranians sasa kama wako Tz sijui maana kama wana ubalozi kwenu basi waacheni wafanye yao ila hao wa Dubai ni Sunni tofauti kabisa na hao Shia

Sasa hapo sijui bandari imeingiaje halafu utakuta wajinga wengine wqnafuata mkumbo badala hata ya kujifunza au hata ku Google
 
Kuna video imesambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha kundi la warabu wakishangilia na kuimba nyimbo huku wakipeperusha bendera ya Tanzania kitu ambacho kimeibua maswali mengi miongoni mwa watanzania wakijiuliza inawezekanaje?

Yani katikati ya sakata la kuuzwa kwa bandari zote za Tanganyika kwa warabu wa DP world ya Dubai alafu tena waonekane warabu wakishangilia kama wamechukua kombe kwa nini?
Kweli viongozi wetu hawaoni hili?View attachment 2741665
Wangeshangilia waisrael mabwana zenu hapo ingekuwa poa kkenge ww
 
Back
Top Bottom