Wababa wenye magari, kwanini mnasimama kwa dakika kadhaa kabla ya kuingia majumbani mwenu?

Sasa kwa kuwa ni majirani, na unaonana nao kila siku, ni kwanini usiwaulize?
 
Kwa wanaume baadhi yenu, anakuwa anamalizia kuongea/kuchat na mwanamke wake wa pembeni. Au mambo yake ya siri. Wengine Mr & Mrs wanatumia gari moja. Anajaribu kutoa ushahidi wa chochote asikamatwe.

Kwa wengine ni mazoea tu, hakuna baya lolote analofanya, huenda anaongea na washkaji au ndugu kwa simu. Mimi ndiyo nikipark ndani ya gate, naweza kaa dakika 10 na zaidi ndiyo nashuka. Huwa wanaogopa huenda nimepata tatizo, nashindwa kushuka but ni mazoea tu.
 
Kuna swala linaitwa CLEAR DATA and CLEAR CACHES ni muhimu sana!
 
Kufuta meseji zote tata.
 
Gari ni yangu lakini Walimwengu mnataka nishuke kama vile notoka kwa Mwendo Kasi au Daladala ya Mbagala.

Kwanini hamtaki raha kwa wenzenu?
 
Tunaweka mambo sawa
 
Huwezi kuelewa. Wanaishi na ma CIA wanakaguliwa WhatsApp Calls SMS kila kitu
Huyu wangu huwa si kila siku ni kuna siku tu ghafla anaamua anapitia kila sehemu meseji WhatsApp mpaka dm za mitandao ya kijamii. Ni kujiandaa kujitetea...

Now huwa nikishajibu text yeyote mahala popote nafuta hapo hapo.
 
Nimeuliza wababa wenye magari humu Jf, naamini hii sio tabia iliyopo mtaani kwangu tu.

Na tayari nimepata majibu
Unajichanganya. Umesema mtaani kwenu wapo. Ila sasa unadai huamini kama wapo.
 
Wanachunguza CCTV camera kuona yaliyotokea wakati wakiwa hawapo.
 
Kweli Wengine ni mazoea tu, lakni kama ulivyosema ni heri wafanye hivyo wakiwa ndani ya mageti yao
 
Wanacheza game maana nyumbani watagombea kucheza na familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…