Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Mkuu,

Kwa mfano mtu anafanya mambo yake clean, by the book. Tangu amelamba visa Tanzania hajawahi kuwa out of status hata sekunde. Na ursia kashschukua US. Analipa kodi kubwa kuliko mishahara ya watu wengine.

Akaingia katika hizo besdei za wabongo, kapotea njia tu siku moja.

Wanaanzaje kumchoma?

Unamchoma vipi mtu kama huyu?
 
Wabongo wengi wana matatizo ya ego na mashindano.

Wanapoteza energy kubwa sana kwenye mashindano ya ego yasiyo na maana.

Mtu anaenda kufukua uzi huko, akuoneshe tu alivyoshinda ligi.
Kabisa.
Bora west africans wanashindania nani ana big investments.
Tunaigina kuanzia kazi makazi na lifestyle hakuna anayewaza nje ya box
 
Take this important rule of life.

Live as if no one is obligated to help you.

Bring value to others so that they recognize you and want to associate with you because of your value, not because they want to help you.
 
Uko sahihi kuwa jinsi ya kufika huko nje ni kipengele sababu wenzetu hawana njia za janjajanja ila inawezekana na ndio mana mkuu Kiranga akakuuliza yale maswali.Hajakurupuka.
Majibu yako kwa yale maswali yatasaidia watu wenye uzoefu kukushauri nini cha kufanya mkuu.
 
Kumbe mkuu upo amerika??
 
Mkuu wewe unafahamu mambo kibao tu ambayo unapaswa kuwasaidia wabongo wafike huko na kufanikiwa hata kama si mimi,wasaidieni watanzania na muache roho mbaya
Hii mentality ya "unapaswa" ni tatizo.

Nikisaidia mtu ni kwa sababu nimependa, si kwa sababu ninapaswa.

Ninapaswa kumlea mwanangu.

Hizo habari za kusaidia wabongo ni jambo la hiyari, sina sharti.

Sielewi kama una tatizo la kuelewa Kiswahili na maana ya neno "unapaswa", au una tatizo kubwa zaidi la kifalsafa la kuona kwamba wewe una haki ya kusaidiwa na watu usiowajua na wasiokujua.

Huna haki hiyo.
 
Mkuu mbona nisha kitumia hapo mambo yangu na hujibu?
 
Naomba umwambie ajibu vizuri yale maswali aliyoulizwa then akishayajibu tuone mkuu Kiranga atamshauri nini.
Msikimbilie kulaumu
 
Mkuu sio huko tu hata hapahapa bongo, nafikiri fitina na roho mbaya zipo deep within our genetic code, tena usiombe wawe WAHAYA utajuta sana.
 
Mkuu Clepatina jamaa baada ya kumwambia haya kageuka tena.

Wabongo ni shida alidhani nipo tu nalalamika bila kuwa skilled yeyote
 
Amerika ni kubwa mkuu, kuanzia Patagonia mpaka The Yukon.
Namaanisha USA mkuu ndo ulipo? Hongera mkuu, nyie ndo mnaishi duniani sasa, sio huku mtu muda wote mimacho inamtoka kutaka kujua your progress in life.. Tena wasiwe WAHAYA watu wa ajabu sana.
 
Mkuu sio huko tu hata hapahapa bongo, nafikiri fitina na roho mbaya zipo deep within our genetic code, tena usiombe wawe WAHAYA utajuta sana.
Kuna Mtanzania alimsaidia Mtanzania mwingine kumkatia tiketi ya ndege.

Kwa sababu wote Watanzania.

Aliyekatiwa tiketi alisema ana hali mbaya, hana hela, hana hata credit card, mgeni.

Baadaye, ikagundulika jamaa aliyekatiwa tiketi alibeba madawa ya kulevya. Alituhumiwa hivyo kukawa na kesi.

Wamarekani wakamdaka mpaka aliyenunua tiketi. Wakiamini kwamba naye alihusika katika biashara ya madawa ya kulevya. Hawakuamini mtu anaweza kukununulia tiketi hivihivi tu.

Jamaa aliyenunua tiketi akawa na kazi kubwa ya kuwaeleza Wamarekani kuwa sisi Watanzania tunaishi kwa kusaidiana hata watu ambao hatujuani sana, huyu mtu nilimsaidia kwa sababu ni Mtanzania mwenzangu tu, hatujuani kihiivyo na mimi sikujua habari zake za biashara ya madawa ya kulevya.

Wamarekani hawakumuamini.

Ikabidi jamaa apate kazi sana kuaelewesha kwamba huyo wala si mtu wa kwanza kumsaidia, kashasaidia Watanzania wengi tu.

Mpaka Wamarekani waelewe somo, jamaa alikuwa kashapata tabu sana.

Haya ndiyo baadhi ya matatizo yanayotokana nankusaidiana kiholela kwa sababu ni Watanzania tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…