Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Wabongo wa mamtoni sio wa ku socialize nao.
Mim nikiwa mamtoni ni wazungu na big brain nigerians tu.
wabongo wa nje hawana issue na vibesdei vyao vya sebuleni umbea wanaume na wanawake.
Wote wanafanya kaz za kufanana ukifanya cha tofauti lazima wakupe shida.
Wana roho mbaya hawaoni shida kukuchoma mkose wote.
Mkuu,

Kwa mfano mtu anafanya mambo yake clean, by the book. Tangu amelamba visa Tanzania hajawahi kuwa out of status hata sekunde. Na ursia kashschukua US. Analipa kodi kubwa kuliko mishahara ya watu wengine.

Akaingia katika hizo besdei za wabongo, kapotea njia tu siku moja.

Wanaanzaje kumchoma?

Unamchoma vipi mtu kama huyu?
 
Wabongo wengi wana matatizo ya ego na mashindano.

Wanapoteza energy kubwa sana kwenye mashindano ya ego yasiyo na maana.

Mtu anaenda kufukua uzi huko, akuoneshe tu alivyoshinda ligi.
Kabisa.
Bora west africans wanashindania nani ana big investments.
Tunaigina kuanzia kazi makazi na lifestyle hakuna anayewaza nje ya box
 
Take this important rule of life.

Live as if no one is obligated to help you.

Bring value to others so that they recognize you and want to associate with you because of your value, not because they want to help you.
 
Mkuu Qualification siyo ishu,kuna watu wanaingiza mpunga mrefu na hawana hizo qualification unazotaka wewe.

Fursa zipo kibao,wewe unachotakakiwa ni kuzimwaga humu hapa na namna ya kuzifikia.Tunafahamu kufika huko ndiko tatizo,wewe inapaswa utusaidie namna ya kufika huko kwakuwa unauzoefu hata kama ni kwa pesa tutalipa.
Uko sahihi kuwa jinsi ya kufika huko nje ni kipengele sababu wenzetu hawana njia za janjajanja ila inawezekana na ndio mana mkuu Kiranga akakuuliza yale maswali.Hajakurupuka.
Majibu yako kwa yale maswali yatasaidia watu wenye uzoefu kukushauri nini cha kufanya mkuu.
 
Kumbe mkuu upo amerika??
Wewe ni sawa na yule mtu aliyeota ndoto.

Halafu akaenda kwa mtafsiri wa ndoto, akitaka atafsiriwe ndoto yake.

Mtafsiri wa ndoto akamuuliza, sawa, niambie ndoto yako nikutafsirie.

Badala ya kumwambia mtafsiri wa ndoto ndoto yako akutafsirie, unampa kazi ya ziada, unamwambia mtafsiri wa ndoto kwanza akuambie umeota nini, halafu aitafsiri hiyo ndoto.

Nakupa kanuni muhimu ya kusaidiwa.

Msaidie anayetaka kukusaidia, fanya kazi yake ya kukusaidia iwe rahisi, usimuongezee mzigo wa kufanya kazi ya ziada ya kutafuta akusaidiaje. Nenda kuomba msaada ukiwa unajua unataka kusaidiwa wapi.

Juzi nilikuwa katika kikao na Profesa mmoja Mtanzania yuko US anatoa michongo ya scholarship. Tuna network ya kusaidia wanafunzi kuja kusoma US.

Alisema kitu kimoja ambacho hapendi ni mtu kuja kumwambia anataka scholarship, bila detail.

That is too general, too vague.
 
Mkuu wewe unafahamu mambo kibao tu ambayo unapaswa kuwasaidia wabongo wafike huko na kufanikiwa hata kama si mimi,wasaidieni watanzania na muache roho mbaya
Hii mentality ya "unapaswa" ni tatizo.

Nikisaidia mtu ni kwa sababu nimependa, si kwa sababu ninapaswa.

Ninapaswa kumlea mwanangu.

Hizo habari za kusaidia wabongo ni jambo la hiyari, sina sharti.

Sielewi kama una tatizo la kuelewa Kiswahili na maana ya neno "unapaswa", au una tatizo kubwa zaidi la kifalsafa la kuona kwamba wewe una haki ya kusaidiwa na watu usiowajua na wasiokujua.

Huna haki hiyo.
 
Hii mentality ya "unapaswa" ni tatizo.

Nikisaidia mtu ni kwa sababu nimependa, si kwa sababu ninapaswa.

Ninapaswa kumlea mwanangu.

Hizo habari za kusaidia wabongo ni jambo la hiyari, sina sharti.

Sielewi kama una tatizo la kuelewa Kiswahili na maana ya neno "unapaswa", au una tatizo kubwa zaidi la kifalsafa la kuona kwamba wewe una haki ya kusaidiwa na watu usiowajua na wasiokujua.

Huna haki hiyo.

Sent from my SM-S908U1 using JamiiForums mobile app
Mkuu mbona nisha kitumia hapo mambo yangu na hujibu?
 
Mkuu habebeki kivipi?
Mambo mengine madogomadogo ni ya kueleweshana tu, kuna watu wana ndoto za kwenda nje lakini wanakosa abc's za namna ya kufanya ili waje huko. So ni jambo la kujitoa hasa nje ya hapo unaweza kuwaona watu hawako serious.

Mfano kuna mtu ana ndoto ya kwenda kufanya kazi nje lakini hajui huko wanahitaji watu wa fani gani, skilled au unskilled n.k. Wengine hawajui hata kutofautisha passport na visa, wengine hata uhamiaji hawajawahi kusogea. Kwa hiyo nyie mliopo nje endeleeni kuwapa madini vijana wanaotaka kutoka nje kusaka fursa nzuri zaidi
Naomba umwambie ajibu vizuri yale maswali aliyoulizwa then akishayajibu tuone mkuu Kiranga atamshauri nini.
Msikimbilie kulaumu
 
Wabongo wa mamtoni sio wa ku socialize nao.
Mim nikiwa mamtoni ni wazungu na big brain nigerians tu.
wabongo wa nje hawana issue na vibesdei vyao vya sebuleni umbea wanaume na wanawake.
Wote wanafanya kaz za kufanana ukifanya cha tofauti lazima wakupe shida.
Wana roho mbaya hawaoni shida kukuchoma mkose wote.
Mkuu sio huko tu hata hapahapa bongo, nafikiri fitina na roho mbaya zipo deep within our genetic code, tena usiombe wawe WAHAYA utajuta sana.
 
Mkuu Kiranga mimi nina elimu ya kawaida,nilifika form 6 lakini nilifeli kwa ishu zilizosababishwa na mapenzi(Haya hayana umuhimu).

Mimi ni dereva mzuri tu na nina miliki leseni daraja C,pia nina passport,kadi ya chanjo ya korona,kadi ya chanjo ya yellow fever.

Nahitaji kufika nje kwa fursa kama udereva lakini pia fursa yeyote ya unskilled mimi napiga,ishu ya pesa ya nauli kwangu siyo ishu.

Wewe niambie nifanye nini mimi nitafanya ili niweze kufika hapo
Mkuu Clepatina jamaa baada ya kumwambia haya kageuka tena.

Wabongo ni shida alidhani nipo tu nalalamika bila kuwa skilled yeyote
 
Amerika ni kubwa mkuu, kuanzia Patagonia mpaka The Yukon.
Namaanisha USA mkuu ndo ulipo? Hongera mkuu, nyie ndo mnaishi duniani sasa, sio huku mtu muda wote mimacho inamtoka kutaka kujua your progress in life.. Tena wasiwe WAHAYA watu wa ajabu sana.
 
Mkuu sio huko tu hata hapahapa bongo, nafikiri fitina na roho mbaya zipo deep within our genetic code, tena usiombe wawe WAHAYA utajuta sana.
Kuna Mtanzania alimsaidia Mtanzania mwingine kumkatia tiketi ya ndege.

Kwa sababu wote Watanzania.

Aliyekatiwa tiketi alisema ana hali mbaya, hana hela, hana hata credit card, mgeni.

Baadaye, ikagundulika jamaa aliyekatiwa tiketi alibeba madawa ya kulevya. Alituhumiwa hivyo kukawa na kesi.

Wamarekani wakamdaka mpaka aliyenunua tiketi. Wakiamini kwamba naye alihusika katika biashara ya madawa ya kulevya. Hawakuamini mtu anaweza kukununulia tiketi hivihivi tu.

Jamaa aliyenunua tiketi akawa na kazi kubwa ya kuwaeleza Wamarekani kuwa sisi Watanzania tunaishi kwa kusaidiana hata watu ambao hatujuani sana, huyu mtu nilimsaidia kwa sababu ni Mtanzania mwenzangu tu, hatujuani kihiivyo na mimi sikujua habari zake za biashara ya madawa ya kulevya.

Wamarekani hawakumuamini.

Ikabidi jamaa apate kazi sana kuaelewesha kwamba huyo wala si mtu wa kwanza kumsaidia, kashasaidia Watanzania wengi tu.

Mpaka Wamarekani waelewe somo, jamaa alikuwa kashapata tabu sana.

Haya ndiyo baadhi ya matatizo yanayotokana nankusaidiana kiholela kwa sababu ni Watanzania tu.
 
Back
Top Bottom