Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

Moja kwa moja.

Inakera sana unakuta upo kibanda umiza mnaangalia mechi mtu anaanza kushangilia goli kabla ya mpira kuingia wavuni au mtu anahadithia tukio la mbele kabla kutokea wakati mechi inaendelea.

Watu wa namna hii nashinda kuwatafsiri kichwani mwao kupo vipi natamani niwatandike makofi kabisa kama wanapenda kusikiliza mpira redioni bora wangekuwa wanabaki makwao kuliko kuwaharibia Ladha ya mpira wenzao.

#UziTayari
Viwe na grades

  1. Vibanda vya kelele
  2. Vibanda vya kutikisa kichwa tu bila kusema chochote
 
Hiyo tabia imeenea sana kanda ya nyonyo...yan kuna muda unataman kupiga quenz hizo komwe ila ukiangalia ni mzee inabid utulie tu
 
Kuna kibanda hapa wameandika si ruhus kusikiliza mpira kweny redio nikawa nashangaa ..kumbe bado watu wanasikiliza kweny redio.
 
Kikawaida mwenye kibanda anatakiwa azuie huo nmtindo
 
Kuna jamaa tulikuwa naye uwanjani sijui alikuwa anasikiliza redio gani ile...yani alikuwa anashangilia kabla ya goli, na kweli huku nyavu zinatikisika
Hakuna kitu kama hicho, labda kama alikuwa anasikiliza mechi nyingine tofauti na hiyo iliyokuwa inachezwa uwanjani

Ikatokea tu coincidence na hapo uwanjani likaingia goli
 
kwanini unaangalia mpira live kwenye tv au uwanjani wakati huohuo unasikilza kwenye radio,inamaana huamini unachokiona ama ni fujo tu?
 
Hizi tabia wanazo hasa baadhi ya wakurya🤣🤣, halafu watata kinoma, anaweza akasimama akasema" atakae nigusa ni vita"..
Wanapenda kuamini wanachokisikia kuliko wanachokiona.
 
Na hii kitu ndo inanifanya game hasa za simba na yanga niamue tu kusikilizia ndani kwenye radio maana ukumbini ni upuuzi mtupu.
Mimi ya leo nataka nidowee kwa jirani hapa kitaa maana kuna nyumba moja jirani kuna amsha amsha ya mechi kama kibanda umiza wadau wengi wa michezo kitaani wanakusanyika hapo kuna kuwa na watu kama kumi na kitu hivi hakuna hata upuuzi wa kusikiliza redio unaenjoy game kistaarabu.
 
W
Kuna jamaa tulikuwa naye uwanjani sijui alikuwa anasikiliza redio gani ile...yani alikuwa anashangilia kabla ya goli, na kweli huku nyavu zinatikisika
Itakuwa alikuwa anasikiliza Magic efuemu😂
 
Hao hawatofautiana sana na wale mnaangalia move yeye kama alishaiangalia ataanza kuhadithia ya mbele yake aloooo hakuna kitu kinanikera kama hicho yaani sipendi

Sasa unakuwa unapoteza umakini wa kuangalia inabidi mumsikilize aisee.

Hawako mbali na wale tukio limetokea na mlikuwepo wote mkishatoka anakuja tena kuwahadithia kilichotokea wakati mwingine wanaongeza chumvi wewe jamaa si tulikuwa wote sasa unasimlia nini tena
 
Yaani GENTAMYCINE natizama zangu 'Derby' ya Kariakoo na wewe unasikiliza mpira kupitia 'Earphones' zako unaotangazwa na TBC Taifa halafu Mayele ameshafunga Goli unaruka kushagilia mbele yangu tegemea kupata bonge la kofi au kichwa kutoka kwangu kutokana na hasira.

Jana huko Ulaya chama langu pendwa la Liverpool FC limefungwa na nina mihasira yangu halafu nimekaa kibandani kuangalia Simba na Yanga itokee Mayele au Fei Toto au Aziz K anifunge na uanze kushangilia kabla yetu tunaotizama runingani (katika TV) halafu nikuache?

Leo kuweni makini 'mtapigwa' sana!!!
 
Back
Top Bottom