Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

Yaani GENTAMYCINE natizama zangu Derby ya Kariakoo na Wewe unasikiliza Mpira kupitia Earphones zako unaotangazwa na TBC Taifa halafu Mayele ameshafunga Goli unaruka Kushagilia mbele yangu tegemea kupata bonge la Kofi au Kichwa kutoka Kwangu kutokana na Hasira.

Jana huko Ulaya Chama langu pendwa la Liverpool FC limefungwa na nina Mihasira yangu halafu nimekaa Kibandani kuangalia Simba's ina na Yanga itokee Mayele au Fei Toto au Aziz K anifunge na uanze Kushangilia kabla yetu tunaotizama Runingani ( katika Television ) halafu nikuache?

Leo kuweni makini 'mtapigwa' sana!!!
Huwa inakera sana kwa kweli.
 
Wasukuma na Wamasai ndo wanaongoza kwa hii tabia ya ovyo.[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji85][emoji85][emoji85][emoji85][emoji85]
 
Wanakera sana, ungesikiliza huko basi sasa kwenye TV umefuata nn?
Halafu nimefanya research wengi ni waha
Mkuu nawe una Utani wa Kikabila na Waha kama Mimi au hapana? Kama hapana tegemea Kushambuliwa nao hapa JamiiForums na hata Kurogwa vile vile.
 
Nenda kibandaumiza sehem zingine hawana hizo mambo
Nimecheki ratiba kuna mechi ya Arsenal saa 10 na vibanda umiza vyote mtaani wameandika mechi hizo mbili unacheki kwa jero tu ,kea hiyo hamna namna lazima niende kibanda umiza nipate faida ya mechi mbili.
 
Unaua dege wa wawili kwa jiwe moja, sema binafsi ikicheza simba sipendi kuwe na mechi nyingine ambayo inanitoa kwenye concentration
 
Unaua dege wa wawili kwa jiwe moja, sema binafsi ikicheza simba sipendi kuwe na mechi nyingine ambayo inanitoa kwenye concentration
kwa mfano mimi ni shabiki wa Arsenal alafu ni Simba mnyama nacheki mechi zote kibanda umiza.
 
Hao hawatofautiana sana na wale mnaangalia move yeye kama alishaiangalia ataanza kuhadithia ya mbele yake aloooo hakuna kitu kinanikera kama hicho yaani sipendi

Sasa unakuwa unapoteza umakini wa kuangalia inabidi mumsikilize aisee.

Hawako mbali na wale tukio limetokea na mlikuwepo wote mkishatoka anakuja tena kuwahadithia kilichotokea wakati mwingine wanaongeza chumvi wewe jamaa si tulikuwa wote sasa unasimlia nini tena
Umenikumbusha siku moja kuna mzee alipata ajali akawa anampigia simu mkewe kumtaarifu.

" eti mama nani hii, unaifahamu ile vx yangu mpya?? Imepata ajali tuko hapa kituoni nikimaliza nitakuja nyumbani"

Yaani anavyomsimulia mkewe ni kama anamhadithia mtu ambaye hafahamu anamiliki gari ya aina gani.
 
Back
Top Bottom