Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

Wabongo wanakera sana tabia ya kusikiliza mpira redioni kibanda umiza wakati mechi inaendelea

Kuna jamaa tulikuwa naye uwanjani sijui alikuwa anasikiliza redio gani ile...yani alikuwa anashangilia kabla ya goli, na kweli huku nyavu zinatikisika
Kwhy redio inaanza kutangaza tukio ambalo ww uliekua live hulion,haiwezekani daima
 
Hakuna kitu kama hicho, labda kama alikuwa anasikiliza mechi nyingine tofauti na hiyo iliyokuwa inachezwa uwanjani

Ikatokea tu coincidence na hapo uwanjani likaingia goli
Hakika
 
Uwanjani haina impact kwasababu redio inakuwa inaenda sawa na kile kinachoonekana uwanjani

Ila kama una stream au kuangalia kwenye TV, redio hua mbele ya muda kuzidi TV.

Mabanda umiza ya kitaa mengi yamepiga marufuku kusikiliza redio ukumbuni
Uwanjan pia ni nadra sana kukuta kuna radio inayoendana na kasi ya uwanjani...huwaga zipo nyuma.
 
Kuna jamaa tulikuwa naye uwanjani sijui alikuwa anasikiliza redio gani ile...yani alikuwa anashangilia kabla ya goli, na kweli huku nyavu zinatikisika
Acha uongo mkuu sasa mpo wote uwanjani yeye hayo matangazo ya goli yalikuwa yanatoka wapi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila nimecheka kinoma yani ila nimefikiria zaidi nkahisi labda jamaa alikuwa anasikiliza radio ya mganga wa timu
 
Leo kwenye kibanda nusu mshabiki wa Simba achapike baada ya kushangilia kabla ya goli kuingia kukazuka zogo kubwa bandani baada ya shabiki mmoja wa Yanga mwenye hasira kali kukereka na kutaka kumpigia .
 
ni ustaarabu tu utumike kama unataka kuskiliza mpira redioni tafta chimbo lako kaa sikiliza ila ukileta redio kwenye kideo watu watakupasua makofi nshashuhudia mtu kapokonywa simu ikatupwa chumvini ferry sasa hasara kama hizo kisa kushangilia goli kabla ya wenzako[emoji23][emoji23]
 
Ni ushamba wa hali ya juu nakumbuka goli la kona alilofunga kichuya mpira haujapigwa mtu anashangilia yaani wanazingua kinoma
 
Back
Top Bottom