Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Mmeanza kutetemeka kama kawaida yenu na maneno mengi, mkutano wa leo na waandishi wa habari ndio utatoa majibu ya maswali yote.
 
Mmeanza kuyetemeka kama kawaida yenu na maneno mengi, mkutano wa leo na waandishi wa habari utatoa majibu ya maswali yote.
Yaani tutetemeke kwa sababu gani?

Mkutano wa leo wa nini? Nielimishe zaidi!
 
Mbowe is a political genius.. Chadema hakitakaa kije kufa kisiasa hasa hasa kama chama kikuu cha kuaminiwa cha upinzani..

Mbowe hatoongea, atasubiri upepo upite then anapiga spin moja tu ya uhakika na mioyo yote ya waliojifanya kutoka au kutokuwa na imani na CDM itarejea..

Mmeambiwa muandamane mmejificha mitandaoni hamuonekani barabarani, mliwapuuzia na sasa eti mnakasirika wameenda bungeni mnataka wasiwapuuzie kama ninyi mlivyowapuuzia??
 
Mkutano wa leo wa nini? Nielimishe zaidi!
Chadema wamesema watafanya press na wanahabari leo saa tano asubuhi.

Nachomaanisha zaidi, maamuzi yatakayotolewa kwenye press ya leo ndio yatakayotoa majibu ya kweli ya kinachoendelea, na sio hizi hisia zako ulizoandika hapa.
 
Umeandika vitu vya kufikirisha.

Kama Chadema waliamua kufanya hivyo (kujiongeza baada ya maandamano kutofanyika) na kuwapeleka hao wanawake bungeni basi wangekuja na kauli moja, lakini sio Mnyika aseme lake, na wale wanawake nao waseme lao.

Mbowe kuzungumza au kutozungumza leo haitakuwa na maana yoyote provided Katibu Mkuu ataongea, na ambacho atakisema katibu Mkuu ndicho kitachukuliwa kama msimamo wa chama ambacho Mbowe ndie mwenyekiti, hapa sioni tatizo.
 

Hakuna akili kubwa pale, yule ni msaliti tu! Kaisaliti taifa, sasa hivi amesaliti na chadema. Ndo maana baada ya uchaguzi amekimbilia nje, hebu jiulize kama ana dhamira ya dhati na anamaanisha anachoongea kwa nini asiwe na wenzake hapa hapa tz? Shujaa na Jasiri wa kweli mnakuwa pamoja wakati wote, iwe shida, iwe raha nk. Yaani yeye amekimbilia ulaya halafu anawapangia ufipa nini cha kufanya? Hivi mtaelimika lini?
 
Uko sahihi kabisa.
 
Wale watu wana baraka za chama. Fedha imeshinda kwa mara nyingine tena (mishahara then michango na ruzuku kwa chama)

Wekeni tu akiba ya maneno maana wakiongea wao mtakuja kupiga U turn
 
Nimepitia mabandiko yote kuhusu hili sakata lakini hili la Msemakweli lina ukweli.Hapa Mbowe kacheza mchezo wa kuwazunguka viongozi wote wa juu,na mimi naongezea ,kwa maslahi yake mwenyewe.Ameona asipoteze vyote.
 
Lissu anasemaje?
 
Mbowe anawajua vizuri hawa wanaopiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kama ni ''debe tupu...''

Nakwambia hawa hawa baada ya kauli ya Mbowe utawasikia wakisema, ''tumeamua kwenda bungeni kwa sababu hatuwezi kumwachia fisi bucha''.

Hawa ''makamanda'' hawana msimamo bali wana makelele tu mengi yasiyoeleweka!
 
Chadema wamesema watafanya press na wanahabari leo saa tano asubuhi.

Nachomaanisha zaidi, maamuzi yatakayotolewa kwenye press ya leo ndio yatakayotoa majibu ya kweli ya kinachoendelea, na sio hizi hisia zako ulizoandika hapa.
Nimekuelewa! Asante.
 
Bado unaendeleza hisia.

Kama ni kumuachia "fisi butcher" lazima ufuate maamuzi ya chama chako, sio kupingana na maamuzi ya viongozi wako halafu useme hutaki kumuachia "fisi butcher"

Hiyo defence kwangu haina maana, kuna viashiria vingi vinavyoonesha hao wanawake wamelaghaiwa na CCM, hasa nikikumbuka yule alietolewa jela juzi Singida, DPP akamuachia kwa nolle, then akapandishwa gari haraka kuwahi Dodoma akaapishwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…