Wachezaji kumi bora wa Afrika mpaka sasa

"Tofautisha uwezo na mafanikio wewe hapa unaongelea mafanikio sisi tunaongelea uwezo .."

Sasa mkuu kutokana na hiyo statement yako juu, huoni kama unataka tu ligi isiyokuwa na kichwa wala miguu

kama ushajua mleta mada anaongelea mafanikio na akatoa na vigezo vya kupima hayo mafanikio na Okocha hana hivo vigezo sasa huku kuzozana kunatoka wapi?

Au tuweke vigezo vya mleta Uzi pembeni, Naomba unipe namba ambayo angekaa Jay Jay Okocha kwenye top 10 ya wachezaji Bora wa Africa kisha utoe na vigezo utakavyotumia kumweka katika hiyo Namba.....!
 
Mkuu naona hujaelewa kabisa umeenda op kabisa nadhani mtoa mada alieelewa muangalie alichojibu.
 
Mleta uzi. Sisi tunamtaka Okocha.

Full stop πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸƒπŸΏβ€β™‚οΈπŸƒπŸΏβ€β™‚οΈπŸƒπŸΏβ€β™‚οΈπŸƒπŸΏβ€β™‚οΈ
Okocha alikuwa mchezaji mzuri kwa entertainment lakini hakuwa na rekodi ya mafanikio.
 
Hujamweka Okocha? Hapo hamna kitu.achana na hii list kabisa. Kocha alikuwa anafundisha vizuri ndo hao wachezaji wanafanya vizuri ulitakiwa umweke na Kocha kama wengi wanavyosema.
 
Yupo Mkongwe Mmoja wakuitwa EMANUEL KUNDE .... Najua wengi hapa hamjamuona akicheza, unamuachaje mkongwe huyo kabla ya Roger Milla.
Huyo beki alikuwa mzuri lakini hakuwa na rekodi ya mafanikio binafsi yanayoweza kumfanya awe wa kipekee kuliko hao waliopo top ten.
 
Hujamweka Okocha? Hapo hamna kitu.achana na hii list kabisa. Kocha alikuwa anafundisha vizuri ndo hao wachezaji wanafanya vizuri ulitakiwa umweke na Kocha kama wengi wanavyosema.
Okocha awekwe kwa rekodi ipi ikiwa hata uchezaji bora wa Afrika hakuwahi kushinda?
 
Huyo beki alikuwa mzuri lakini hakuwa na rekodi ya mafanikio binafsi yanayoweza kumfanya awe wa kipekee kuliko hao waliopo top ten.
Nikiwa Mdogo sana, nasikia Radio Tanzania ama BBC hivi, Babu yangu akisikiliza na kulikua na mechi siku hiyo, nikasikia kila wakati jina la EMANUEL KUNDE....!

Siku moja tukaenda kwenye Msiba wa Ndugu toka kijiji kimoja kwenda kingine, nikiwa kwenye Gheto la Ndugu ambaye yeye alikua Kijana wakati huo, ndo naona Chumba kizima kimepambwa na Magazeti Ukutani, yenye Picha ya EMANUEL KUNDE!!!

Nikaanza kuvutiwa nae ila sikuwahi kumuona akicheza.
 
Basis huyo in mchezaji bora asiye na rekodi bora
Kweli kabisa, alikuwa na kipaji lakini hakuwa na mafanikio kwasababu hata kipindi yupo kwenye peak bado walioshinda tuzo ya mchezaji bora Africa walikuwa wengine.
 
Tatizo hapa ni hivyo vigezo vinavyotumiwa kuwapa hao hizo namba. Wengine wamo kwa bahati tu si kuwa ndio wazuri zaidi. Historia ya J. J. Okocha inaeleza mengi. Na wapo wengi tu wa aina yake kwa bara la Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…