Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Naomba kuuliza maduka ya bei rahisi ya phone accessories kariakoo plz[emoji18]
Ngja nku pm namba ya Mdau mmoja ana duka hapo kko mtaa wa likoma ana duka la spear za simu tu...anatoa nje

Ova
 
Habari wakuu! Jana nilitembea k/koo mtaa wa sokoni nilikuwa natafuta Vijora vya Mombasa kwa ajili ya biashara sasa si mzoefu ila bei niliyoikuta ni hii je ni sahihi au wapi naweza pata iliyopoa zaidi.

Vijora vyenye mtandio kwa 12000 jumla
Vijora bila mtandio 6000
Vijora vile vya Shiffon bila kamba 6000
Vijora vya shiffon na kamba 12000

Nikaelekea kitumbini hapa nilienda angalia vitenge nilikutana na hali hii ya bei;-

1.Java zile za china zisizopauka bei 20000 hadi 19500 hapa ni (oriental au Disco) nilivoshauriwa na wanaofanya hii biashara kuwa hizi brand ndo nzuri
2.Java no 2 ambazo ni brand nyingine au wanasema nyepesi bei ni 15000 hadi 14000

3.Nikaja wax hapa sikujua brand gani ni nzuri ila kuna dada aliniambia ANGEL ndo haichuji na kupauka huwa inatoka china ambayo bei ni 21000 hadi 20000

4.Wax no 2 ambazo hizi za moro na nyingine nyingi kuna za 10000 hadi 15000

5.Vitenge vya kawaida nikakuta na vile vya pc 2 kwa bei ya 7000 kwingine 5000 kwingine 6000. Nikauliza urafiki wakasema saaa hivi haifanyi kazi ko hawana mzigo wake

Nimeleta hapa ili kama kuna yeyote anafahamu wapi ntapata mzigo mzuri kw bei nzuri zaidi pia napokea ushauri kipi kibaya kipi kizuri kabla ya kufanya maamuzi ya kuingiza pesa.Karibuni sana.
 
Back
Top Bottom