Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Kwenye maelezo ktk barua haikuonyesha popote kuwa maafisa wamesimamishwa kazi zaidi ya kuwa wamechukuliwa hatua za kinidhamu.
 
Mara nyingi Wanajeshi hutoa adhabu kali kwa mwarifu pasipo kumpiga
Unamaanisha nini sasa! What’s the difference? Kuna adhabu nyingine ni mbaya maradufu kuliko kupiga.
Mfano, hao askari wa uhamiaji kuna kuna kipindi walimlaza jamaa chali wakamwagia maji usoni. Hiyo inakuzuia kupumua..Mateso hayo yanaitwa Water boarding. Na yameharamishwa hata kimataifa.
 
Hizo adhabu wawe wanapeana jeshini, huyo jamaa wangeishia kumuua. Hakuna namna ya kumshtaki huyo mtu au kumwekea sanctions...
 
Mbona wanajeshi nao wanawasulubu watu but viongozi wao huwezi ona wako kinyume nao.Rejea chadema kupigwa segerea,kichapo wakatizao bahati mbaya maeneo ya jeshi, vijana wavaao nguo za jeshi la nje mfano kofia,nk
 
Wataje majina ili na wao watu wao wa karibu wajue
 
Sawa,ila hao vishoka wamezidi
Acha wapate fundisho

Ova
Kweli kabisa . Hatahivyo, ni vyema wakapata fundisho kali kwa utaratibu sahihi. Askari wakiachwa wakaamini wanawajibu wa kutoa mafundisho kitu ambacho si kazi yao, siku watakupa tuhuma ya uongo na mafundisho juu..
 
Kila nikifikiri naona hii serikali na sheria zetu nizakiboya sana..
Inawezekana vipi mtu tapeli yaani mnyanganyi wa kiakili au mnyonyaji wa riziki za watu kuhenyeswa kidogo tena sana na hata damu hazijatoka afisa aliyehenyea ajira asimamiswe kazi kiyaiyai kama hivyo...is not fair!!!!

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Sema hao Uhamiaji wameshindwa kutumia fursa pesa imejileta yenyewe hioveti unaipiga tifu upate sifa badala ya kuikamata na kuipa kesi bila milioni 3 Hakuna kufuta kesi.Sema hapo hakuwepo mchaga tu asingeachia hio takukuru feki bila pesa.Wenzetu police wanajua kuzitumia fursa hizi kachezee police watakupa chumba bure kutoka ni lzm ulipie.
 
Mtuhumiwa bonge ,mle hakosi pressure angewafia je...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yale yale ya yule Dereva aliyevutwa kwenye Gari akaaga dunia wakaishi kumsukumia lawama Marehemu.

Hivi hata kuheshimiana utu tunahitaji Mwalimu atoke taifa jingine aje kutufundisha?.

Ni aibu kubwa maana hili sasa litaonekana popote Duniani na tutaonekana taifa lenye Watu wasiohesimiana.
 
Lengo lilikuwa jema lakini wakatumia approach ovyo kabisa. Hauwezi tumia adhabu za kijeshi kwa raia. Raia wana sheria zimetungwa kwa ajili yao na si vinginevyo. Sasa yamewageuka.....wamelikoroga lazima walinywe.
 
Ni jambo jema sana maana kujichukulia sheria mkononi kuna madhara mengi kwa raia na ni precedent mbaya kwa watu kama watendaji wa serikali wanaopaswa kutenda jambo lolote 'with the authority of the law'. Kinyume na hapo ni kutenda 'arbitrarily' na watu hawatanyamaza kupaza sauti zao na mara nyingi kwa msaada wa mitandao ya kijamii mambo yaliyokuwa yakimalizwa kimyakimya leo hii ukiyafanya tu yanaonekana hadharani. Jidanganye kutumia ubabe kutumia madaraka au ofisi yako vibaya, utaonekana na utakuwa na kesi ya kujibu. Kuna njemba mmoja nilichangia jana kuhusu jambo hili, nikisema kujichukulia sheria mkononi siyo ustaarabu kabisa maana serikali imeweka utaratibu kwa mtu yeyote anayedhaniwa au anayeonekana kuwa mhalifu na inabidi ufuatwe, lakini huyo njemba akaniita 'idiot'. Sasa nadhani atajua nani kati yangu na yeye ni 'idiot in practice'.
 
Hiyo taarifa ya uhamiaji haisemi kuwa wamewasimamisha au mimi sijui kusoma kiswahili?
 
Aliyewarekodi wakiwa wanatoa Etra drill ndio amewaonza.
Jwtz ndio jeshi lenye nidhamu aende akatapeli huko. Hakuna clip itaruka lkn atasomba maji kujaza pipa kutumia ndevu[emoji23]
 
Lengo lilikuwa jema lakini wakatumia approach ovyo kabisa. Hauwezi tumia adhabu za kijeshi kwa raia. Raia wana sheria zimetungwa kwa ajili yao na si vinginevyo. Sasa yamewageuka.....wamelikoroga lazima walinywe.
Taarifa mbona haisemi wamesimamishwa?
 
Askari mnateteana kwa mambo ya kikatili...sasa mahakama zipo za kazi gani?.

Hata aliyeua huna haki ya kumuhukumu kabla ya kumfikisha Mahakamani.

Na kama hizo ndio adhabu mnazotamani kuwapa Wengine basi mfanye utaratibu ziwe sehemu ya sheria za nchi ili Mahakama ikishahukumu muanze kuwadhalilisha Watu.
 
Yale yalikuwa mazoezi Wala sio adhabu nadhani Kuna shida pahali.

Kuna zile njemba za .... KJ au hata Hawa wa PT kule mziki wake n mwingine aisee

Hao uhamiaji binafsi naona Yale n mazoezi tuu kwa mtu alieikosea adabu taasisi ya kijeshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…