Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Katika ile video inaonekana askari wasiopungua watano (ikiwemo sauti za wengine kadhaa zikihimiza ile adhabu ikaziwe), kwanini watatu tu ndio waliosimamishwa?
Pia tunataka majina na picha zao ziwekwe hadharani.

Kuna namna hapa watu fulani wanataka kulindwa.
Nyie watu ni wajinga sana,hamueleweki mnataka nini mamlaka yoyote ifanye, taperi kafanywa vile ili funzo kwa Wengine, leo tayari taperi anaonekana ana haki kuliko wale askari, hapo mnatamani hata ikiwezekana aachiwe huru kabisa bila kupelekwa court
 
POSHO ZA WIZARA YA FEDHA MWEZI MARCH,APRIL NA MEI.

Tarehe 31/03/2021 Shilingi 251,000,000/= (kazi maalum)

Siku hiyo hiyo tena tarehe 31/03/2021 Shilingi 198,000,000/=

-Mwezi April ilikuwa balaa.

Tarehe 08/04/2021 Shilingi 44,500,000/=

Tarehe 13/04/2021 Shilingi 155,295,000/=

-Tarehe 30 April nayo ilikuwa balaa

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,900,000/= (kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 14,400,000/=
(siku ya wanawake)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,000,000/=

Mei mosi siku ambayo sio ya kazi.

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi asubuhi Shilingi 184,100,000/=

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi Mchana Shilingi 264,000,000/=

Tarehe 03/05/2021 Shilingi 146,500,000/=
(Kuandika mpango Kazi wa manunuzi watu 125 [emoji3])

Siku hiyo hiyo tena Shilingi 171,200,000/=(kuandaa nyaraka za bunge)

#WeMissYouJPM.
#Tunakukumbuka JPM.
 
Hivi mama Kamishna kweli hajui udalali uliopo hapo Kurasini kwenye hizo flem hasa zinazohusiana na Stationaries!?

Hivi ni kweli kwamba mama Kamishna hafahamu kuwa hao maafisa wa Uhamiaji huwa wanashirikiana na vishoka kuwapiga watanzania wenzao pesa ya Hati ya Kusafiria wakishirikiana na hao vishoka ambapo baada ya kazi hupitia asilimia zao kwenye hizo Stationaries!?

Hivi ni kweli mama Makakala hajui yanayoendelea kwa hao wanaojiita ni Mawakala wa kuwatafutia kazi wadada nchi za nje hasa nchi za Kiarabu namna wanavyodhulumiwa pesa zao na kutumika kingono!?
 
Lakn matapeli wanaumiza sana watu. Watu wamekufa kwa pressure watu wamejiua, wastaafu wanatapeliwa pension zao.

Mbaya zaidi hizi kesi za kutapeli zinapoteza muda tu mara nyingi wanaachiwa..
Hi nchi wapumbavu wengi ,Kwanza wale askari ili waliyokuwa wanampa sio adhabu kabisa,

Ilitakiwa aenyeshwe hadi mavi yamtoke!!, Angalia jinsi alivyonenepeana kwa ela za uhalifu
 
Nyie watu ni wajinga sana,hamueleweki mnataka nini mamlaka yoyote ifanye, taperi kafanywa vile ili funzo kwa Wengine, leo tayari taperi anaonekana ana haki kuliko wale askari, hapo mnatamani hata ikiwezekana aachiwe huru kabisa bila kupelekwa court
Huyo tapeli kishoka kapewa funzo
Tosha

Ova
 
Tapeli kaogeshwa maji na kugaragara chini ndo salama yake ingekuwa kakamatwa mtaani wangempiga vibaya hata kumuuwa.
Na huyo tapeli aache utapeli.
Ila hao jamaa wanazingua,binafsi niliona kama ni kweli jamaa ni tapeli alistahili ile adhabu ila kama walimsingizia hapo sawa,wezi wanaumiza na kurudisha nyuma wengi sana
 
Bwana KYAI ni tapeli sawa amepatikana na hatia ndani ya ofisi za wenye mamlaka ilifaa zaidi kumwajibisha kisheria kwa makosa yake ya utapeli/udanganyifu
Kumdhalilisha namna ile kumwogesha tope mithili ya kiboko siyo ubinadamu
 
Badala ya kutafuta pesa wao wanatafuta sifa,wakalee watoto wakisubiria uchunguzi hapo unakaa home miaka 2 kwa kitu kisicho cha faida.Wao wangemkamata wakamkabidhi kunako husika.
 
Hii kijeshi wanasema imeisha hiyooo, wanasubiria mwingine aingie kwenye kumi na nane zao wamnyongoroshe..........ile video ilirushwa strategically maana juzi tu mitandao ililalamika uhalifu umezidi.
Hasa vuta picha hiyo ni uhamiaji,ukiingia kwenye kumi na nane za polisi je? Na ukijifanya una haki huko mitaa ya jw je?
Mkipiga kelele wanadamka hasa msiwaambie Tena uhalifu umezidi maana watawaonyesha uhalifu unavyodhitiwa
Alex tulishtuka kumwona anaendesha shangingi tukajiuliza huyu kaajiriwa serikalini kwa elimu gani? Kumbe tapeli wa mjini.

Mzazi mkanye mwanao dola inatabia yakuwafurahisha adhara huku unaumia
Utawala wa sheria na katiba uko wapi ? Ikiwa kila mtu atumie mamlaka aliyo nayo kuadhibu? Tapeli alitakiwa apelekwe mbele ya sheria siyo kuadhibiwa kana kwamba alishahukumiwa na mahakama.
 
Askari hawajawahi kutumia akili, wao ni mabavu tu.
 
Hao matapeli waangalie na sehemu za kwenda maana unapoingia anga za kijeshi huwa hawapigi ni mahovyo hovyo then wanakuachia uende, huyu mhalifu baada ya tifu wangekuwa wamemalizana lakini sasa na yeye anakwenda mahakamani na akibainika ni safari ya jela, sasa si bora tifu la hapa na pale angejiondokea zake.

Tujifunze kuheshimu vyombo vya ulinzi na usalama maana unapowaprovoke wao wamefundishwa kudeal kijeshi jeshi tuu.
 
POSHO ZA WIZARA YA FEDHA MWEZI MARCH,APRIL NA MEI.

Tarehe 31/03/2021 Shilingi 251,000,000/= (kazi maalum)

Siku hiyo hiyo tena tarehe 31/03/2021 Shilingi 198,000,000/=

-Mwezi April ilikuwa balaa.

Tarehe 08/04/2021 Shilingi 44,500,000/=

Tarehe 13/04/2021 Shilingi 155,295,000/=

-Tarehe 30 April nayo ilikuwa balaa

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,900,000/= (kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 14,400,000/=
(siku ya wanawake)

Tarehe 30/04/2021 Shilingi 43,000,000/=

Mei mosi siku ambayo sio ya kazi.

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi asubuhi Shilingi 184,100,000/=

Tarehe 01/05/2021 Mei Mosi Mchana Shilingi 264,000,000/=

Tarehe 03/05/2021 Shilingi 146,500,000/=
(Kuandika mpango Kazi wa manunuzi watu 125 [emoji3])

Siku hiyo hiyo tena Shilingi 171,200,000/=(kuandaa nyaraka za bunge)

#WeMissYouJPM.
#Tunakukumbuka JPM.
Mbona aliyekuwa CAG prof Assad alipoibua ufisadi wa 1.5T haukupost wala haukushabikia??
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 30, 2021 Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mnamo Mei 27 mwaka 2021, Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli anayefahamika kwa jina Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini mkoani Dar es salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za pasipoti, aliyemtambulisha kama mkewe.

Aidha Dk. Makakala amesema baada ya mahojiano, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka, pia mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya askari hao" amesema Dk. Makakala.

Sambamba na hayo, Idara ya uhamiaji inatoa wito kwa Wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe katika ofisi za Uhamiaji, pia Uhamiaji wanawahakikishia kwamba idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weledi, uwazi na bila kutumia mtu wa kati ( Vishoka).

Aidha Idara ya uhamiaji imetoa onyo kwa yeyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa Afisa wa Uhamiaji au Afisa wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria, Pia idara hiyo imewataka Watanzania wote kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hiyo.

Pia soma; Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

Wamesimamishwa au wameachishwa?
 
Tatizo bado halijatatuliwa,utaratibu ufuatwe kwa wote sio akina fulani kisa wapo kwenye vitengo huko ndio watumie mwanya huo kutofata utaratibu ikibaki hivi vishoka hataisha kila mahali.
 
Watarudishwa tu Kiana ,wananchi ni sawa na watoto lazima baba yao uwaridhishe ili wafurahi wachape kazi tupate Kodi tusomeshe wanetu shule nzuri ,yule vizuri Sana wao wakila michembe na matoboro,wakiwa wanabanana kwenye daladala sie kwenye ma v8 yetu na ndio hao hao wanatununuliaga.na tunatumia hao hao masikini kudhibitiana ,Askari namlipa anamdhibiti masikini mwenzke kwa maslahi yangu na kidoshi wangu.
Ngoja kwanza niende Brazil nimemisi kufanyiwa na masaje na mtt wa Latin America ,huku kwenye mahaba akilalmika ki spanöla jamani Kuna raha duniani yaani nyie acheni tu.
Ukijua kumtumia wa chini ni raha Sana ,hata pmj alikuwa anajidai anateteaa wanyonge kumbe ndipo anawanyonga kabisa
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 30, 2021 Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mnamo Mei 27 mwaka 2021, Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli anayefahamika kwa jina Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini mkoani Dar es salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za pasipoti, aliyemtambulisha kama mkewe.

Aidha Dk. Makakala amesema baada ya mahojiano, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka, pia mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya askari hao" amesema Dk. Makakala.

Sambamba na hayo, Idara ya uhamiaji inatoa wito kwa Wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe katika ofisi za Uhamiaji, pia Uhamiaji wanawahakikishia kwamba idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weledi, uwazi na bila kutumia mtu wa kati ( Vishoka).

Aidha Idara ya uhamiaji imetoa onyo kwa yeyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa Afisa wa Uhamiaji au Afisa wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria, Pia idara hiyo imewataka Watanzania wote kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hiyo.

Pia soma; Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

Nawapongeza viongozi hawa kwa hatua walizochukua, kwa kweli jeshi la polisi limekuwa mstari wa mbele kutuhimiza raia kufuata sheria bila shurti,sasa inakuwaje wao wanavunja sheria?
Ni kweli huyo ndugu alifanya kosa la jinai japo mpaka sasa na mimi sina uthibitisho kama alifanya kweli,maana hawa watu ni wataalam wa kubambika kesi(si ajabu aliwatishia kuleta afisa wa takukuru,wakasema amejiita afisa wa takukuru) who knows?
lakini tuamini kuwa alitenda kosa. Najiuliza iko wapi sheria inayowazuia raia kufanya kazi ya mahakama( kuthibitisha kosa na kutoa adhabu),kitendo cha viongozi wa ngazi ya juu kuchukua hatua hii kinaturudishia imani kwa polisi wetu na vyombo vya dola.

Pia nashauri elimu isitolewe kwa raia tu,watumishi wa vyombo vya dola wapewe elimu na refresher couse za mara kwa mara ili wasimamie sheria wanazozielewa kikamilifu,hili litasaidia sana kutuondolea aibu inayolikabili taifa kupitia vitendo vya wachache wasiojielewa.
 
Back
Top Bottom