KERO Wafanyakazi wa Elements Club (Masaki) kuweni na adabu. Mna madharau na kiburi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hamna ndugu yangu mimi nimeenda Sehemu nyingi. Nakupa mfano mdogo Nairobi kuna Strip Clubs za level tofauti tofauti. Kuna ambazo unaingia kama elements na kuna ambazo kuingia inabidi uwe na 29 years na inabidi uonyeshe passport hata kama mkenya. Niliuliza nikaambiwa ni mbinu ya kujua level ya uchumi ya mteja. Wakikagua passport wanajua huyu mteja wa level yetu. Nilikutana na watu walionifundisha mengi. Ndugu yangu yaliyotokea element chukulia kama fundisho, kwamba inabidi upunguze starehe na uongeze utafutaji.
Hao ni washamba, Kuna watu hawana passport na wana pesa chafu. Passport ni travel document Sasa kama mtu haendi popote nje ya nchi passport ya nini? Passport ni laki na nusu tu kwahiyo 150k ni tajiri?
 
Biashara huwa Kuna kupanda na kushuka, club element wasipofanya mapema reform ya wafanyakazi basi Ile club haishuki inaenda kudondoka na kufa kabisa

Nimeamua niandikie leo japo ni tukio lililonitokea mwezi Jana. Sio mara yao ya kwanza kunitreat unfairly imekuwa ni tabia yao.. Tulienda pale na rafiki angu saa tano usiku tukalipa buku ten ya kiingirio tukaenda moja kwa moja kukaa meza moja ilikuwa empty

Muhudumu akaja akasema hii meza reserved, tukamwambia tuonyeshe pa kukaa, akaja baunsa kututoa kwa nguvu mpaka nje, kuulizia nn shida wakasema sisi wasumbufu. Tukasema watusamehe hatukujua but walikataa

Ivi kuulizia tu tukae wapi tayari ni kosa? Yani wana viburi, huduma mbovu wanathamini mastaa na matajiri tu mana hata ukienda na Gari ya IST au Vitz hupew parking, walahi yule mmasai hakupi pa kupaki. Ila wakiona LC 300 hapo wanakupokea na magoti

Mbaya zaidi ukionekana umeenda na bodaboda au bajaji umekwisha, hatihati wasikuruhusu. Lile baunsa lenye upara why lisitoleweee mbona jeuri saana afu Lina miaka mingi kweli pale sijui wanalibembeleza la nini
View attachment 3067133
Sasa ticha Mpwayungu Village, hela ya kusahihisha mock tu ya form two wilaya unataka kwenda kutisha Element Club? Bora walikutoa nje utwo tuhela angalau ukadundulize vigae kwa Mhindi! 😁😁😁
 
Ungezungusha jack Daniels Kila meza wangejua tu kuwa wewe si mtu mdogo
😂😂😂 Mkuu mm kinywaji changu ni windhoek nikikosa hii narudi kulala, hata kama windhoek itauzwa 20k mm nakunywa, ila jackdaniel, Hennessy na jaggarmaster hata zikiuzwa buku sinunui kwasababu situmii

Muulize poshy quuen nje ya safari anakunywa nn
 
Hao ni washamba, Kuna watu hawana passport na wana pesa chafu. Passport ni travel document Sasa kama mtu haendi popote nje ya nchi passport ya nini? Passport ni laki na nusu tu kwahiyo 150k ni tajiri?
Unasema washamba lakini haujatembea ndugu yangu.Element haiwezi kufa ndugu yangu. Kuna hotel inaitwa Ledger Plaza Bahari Beach haina watu wengi lakini mpaka kesho ipo. Ndugu yangu sio kuwa na passport tu wanaikagua wanajua huyu mtu yupo level fulani. Usilazimishe kuruka hatua na kutaka kuishi level ambayo haujaifikia. Ukiona unaenda club na kiingilio kinakuuma badili club. Kwa ulichoandika level zako ni za kunywa liquor store (fremu zinazouza pombe). Huu ni ushauri ndugu yangu nilishawahi kuwa hapo ulipo. Wewe imekutokea Element mimi ilinitokea Hongera baa pale Ustawi. Baada ya hapo ndio nikaja kujua inabidi nikazane. Nashukuru Mungu sasa mambo yamebadilika. Mkuu usiumie wala kusikitika we komaa ndugu yangu.Hapo Element sio kwenu au kanisani kwamba ni lazima uende.
 
Nenda Maison au Havoc /Tips
Sio lazima Elements... au zimefungwa hizo hapo daslam?
ILa mambo ya Reserve ni kawaida tushanyanyuliwaga Cape town tukaambiwa meza iko reserve ilihali hawakua wameweka utambulisho! Sema muhudumu alitubebea vinywaji akatupeleka pa kukaa tukakaa kwa raha kuliko kule..
Walichokosea wangerudisha 10 zenu pia kudhalilishana. Ukienda Sehemu za Daslam unajutahidi kuwa mpole mpole
 
Kwenda club na laki Tatu mfukon ni ndogo? Kwahiyo inabidi niende na begi la pesa kwenye fuko la shangazi kaja au vipi
 
Hapana hao wanaodai passport ni washamba maana hata sisi madereva malori wa transit tunazo kwaiyo tushahama level?
 
Sasa wanakagua wanaangalia umesafiri Kongo ndio utaingia ? Watu wamesafiri nchi mbali mbali wanaangalia umesafiri wapi ? Aisee ukikaa Nairobi wiki utajifunza mengi sana.
 
Mnaleta masikhara mm nipo serious
Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru na jamhuri mwaka 1962, mawaziri wa kwanza kwanza kwenye Baraza la Mawaziri la Mwl. Nyerere Lawi Sijaona na Bibi Titi Mohamed walienda pale Palm Beach Hotel wakati huo ikiwa "Whites Only" kupata huduma. Wahudumu waligoma kuwahudumia. Wakamuita meneja (Mzungu) akawaambia kuwa hawastahili kupata huduma pale kwasababu wao sio "wazungu"!

Walivyojibiwa vile na meneja (Mzungu) wakaondoka kwa hasira hadi Msasani kushtaki. Mwl. Nyerere aliposikia alicheeeeeeka kisha akawauliza nanukuu, "Kwani Magomeni, Kinondoni au Buguruni hakuna sehemu mnaweza kukaa hadi kung'ang'ania kwenda Palm Beach?" Mwisho wa kunukuu. Ahahahahaha!!!
 
Nenda Maison au Havoc /Tips
Sio lazima Elements... au zimefungwa hizo hapo daslam?
ILa mambo ya Reserve ni kawaida tushanyanyuliwaga Cape town tukaambiwa meza iko reserve ilihali hawakua wameweka utambulisho! Sema muhudumu alitubebea vinywaji akatupeleka pa kukaa tukakaa kwa raha kuliko kule..
Walichokosea wangerudisha 10 zenu pia kudhalilishana. Ukienda Sehemu za Daslam unajutahidi kuwa mpole mpole
Nimekuelewa dada angu! Hapakuwa na notification yoyote kwamba meza ni reserved, tungeona tusingekaa. Tuliuliza tu Sasa tukae wapi? Basi baunsa akaja kututoa kwa kutumia nguvu ya mkono. Saizi naendaga zangu wavuvi camp wapo vzr, nikikosa hapo ni samaki samaki basi
 
Kwenda club na laki Tatu mfukon ni ndogo? Kwahiyo inabidi niende na begi la pesa kwenye fuko la shangazi kaja au vipi
Ndugu laki tatu sio hela ya kwenda elements na kuwa treated vizuri.Ukitumia laki tatu element haupo hata kwenye kumi bora ya wateja waliotumia hela nyingi hapo. Kuna Baa nyingi unaweza ukaenda ukala nyama na bia zako then ukarudi nyumbani kulala.
 
Nimekuelewa dada angu! Hapakuwa na notification yoyote kwamba meza ni reserved, tungeona tusingekaa. Tuliuliza tu Sasa tukae wapi? Basi baunsa akaja kututoa kwa kutumia nguvu ya mkono. Saizi naendaga zangu wavuvi camp wapo vzr, nikikosa hapo ni samaki samaki basi
Ndo mana hapo nmekwambia sisi pia hatukukuta hio Reserved ..
SAmaki Samaki sijuagi ubaya wao mana nakaaga na watu wanaojiweza kwahiyo sionagi tofauti...
SEhemu pekee nnazoona hudumua ziko poa ni Restaurants
 
Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru na jamhuri mwaka 1962, mawaziri wa kwanza kwanza kwenye Baraza la Mawaziri la Mwl. Nyerere Lawi Sijaona na Bibi Titi Mohamed walienda pale Palm Beach Hotel wakati huo ikiwa "Whites Only" kupata huduma. Wahudumu waligoma kuwahudumia. Wakamuita meneja (Mzungu) akawaambia kuwa hawastahili kupata huduma pale kwasababu wao sio "wazungu"!

Walivyojibiwa vile na meneja (Mzungu) wakaondoka kwa hasira hadi Msasani kushtaki. Mwl. Nyerere aliposikia alicheeeeeeka kisha akawauliza nanukuu, "Kwani Magomeni, Kinondoni au Buguruni hakuna sehemu mnaweza kukaa hadi kung'ang'ania kwenda Palm Beach?" Mwisho wa kunukuu. Ahahahahaha!!!
Hayo mambo hatuyataki, hii Tanzania ni yetu sio wazungu. Basi waweke wazi kuwa waafrika hatutakiwi hata hivyo wateja asilimia tisini na tisa wa element ni watanzania. Wale wahudumu hawatakiw kujaji kwa kiwango cha pesa za mteja, wao watoe huduma hata mteja akiagiza Fanta orange mpaka asubuhi apewe huduma yake kwani kosa lipo wapi?
 
Sasa wanakagua wanaangalia umesafiri Kongo ndio utaingia ? Watu wamesafiri nchi mbali mbali wanaangalia umesafiri wapi ? Aisee ukikaa Nairobi wiki utajifunza mengi sana.
Watabaki kuwa washamba wala hakuna la kujifunza kwa hao na je kama nisafiri gulf kwenda kuwa beki tatu
 
Back
Top Bottom