Ndo utumwa na dhuluma zenyewe. Wafungwa wanalima Vyakula lakini awapewi chakula cha kutoshaGereza la Songwe ni gereza la kilimo na linamiliki mashamba makubwa sana ya mahindi na maharage, kwanini wanapewa chakula kidogo?
Maafande wanayauza kimagaham.Gereza la Songwe ni gereza la kilimo na linamiliki mashamba makubwa sana ya mahindi na maharage, kwanini wanapewa chakula kidogo?
Mume/mke akienda jela aliyeachwa ana haki ya kuomba talaka. According to roman catholic. Ukikuta kakuvumilia basi shukuru munguView attachment 2143225
Hizi jela zetu zimekuwa sehemu ya mateso na sio sehemu ya kumrekebisha mtu tabia.
Mfano hapa jela ya Mbeya Mjini watu wanafanya kazi asubuhi hadi saa nane mchana, chakula ni saa tisa mchana yani chakula ni ugali maharage ambao haufikii hata nusu sahani.
pia unyanyasaji wa vipigo ni wa hali ya juu, nakumbuka rais Magufuli alitoa amri Wafungwa wafanyishwe kazi usiku na mchana na wapigwe mateke
Pia kwa wale waliooa, wakiingia jela ndoa huwa zinaharibika moja kwa moja, mtu ukiingia jela huwezi kuwa faragha na mke wako mpaka umalize kifungo, ni wanawake wache sana wanaweza kuwa waaminifu katika hi hali.
Hii hali sio hali aisee.
Hilo la wafungwa kulipwa pesa na kuwekwa kwnye ACC zao ni ngumu sn kwa Tanzania.Kuwafanyisha Kazi wafungwa bila kuwalipa ni utumwa na ni dhuluma pia ni kinyume na Sheria ya maadili ya kazi.
Inatakiwa mfungwa akifanya Kazi alipwe awekewe kwenye account yake Ili akitoka jela apate cha kuanzia.
Sio sahihi kuwatumikisha wafungwa maana biashara ya utumwa ilishakufa.
Jela ni kuteswa .Gereza la Songwe ni gereza la kilimo na linamiliki mashamba makubwa sana ya mahindi na maharage, kwanini wanapewa chakula kidogo?
Kwa hiyo mfungwa anaondolewa uhuru wa kuchangamana na wengine tu, na serikali au waliomfunga wanatakiwa kumgharimia kwa kila kitu bila yeye kujishughulisha kufanya kazi yoyote ile, wataalamu wa sheria kujeni kutoa udadavuzi zaidi..........Mfungwa kufanya Kazi ni makosa ni kinyume na sheria za Kazi
Mfungwa atungishe mimba, nani atalea huyo mtoto? Wewe uko tayari kutoa binti yako akatungishwe mimba na mfungwa? Kumbafu wewe.Ipo haja ya jela watu waruhisiwe kushiriki mapenzi na wake zao, mfano sabaya unamfunga Miaka 30 bado kesi zingine still ni kijana hana mtoto kwann asipewe haki ya kutungisha mimba Ili akitoka jela akute watoto wake ni wakubwa wamfae uzeeni.
Kuna mshua mmoja alishawahi kuwa uko,aliwahi kuniambia ukisikia siku nduguyo amekamatwa palepale akiwa mahabusu ya polisi jitahidi kumtoa kwa kumpa dhamana yoyote hata nyumba yako weka rehani kisha akiwa nje fanya mipango yoyote ile kesi iishie ukuuku chini kabla ya kufika mahakamani,mpaka hapo kuna cha kujifunzaJela za Tz ni mateso.
Duuh pole yakeYuko jirani yangu hapa Kimara B alikwenda kurushia kanisa la walokole usiku wa manane kisa wanampigia makelele hawezi kulala. Asubuhi polisi wakaja kumbeba, utani utani kaja mtu mmoja kumuwekea dhamana , policcm wakasema wanataka wadhamini wawili, kisa mchungaji aliwapa ubani. Ilikua ijumaa, kufumba na kufumbua mshikaji Yuko gerezani.
Amesema kule kula kwa foleni, ugali na Maharage, siku ya kwanza walimpa Maharage 17 siku ya pili 14. Kujisaidia haja kubwa unasimamiwa na kijana mdogo na unaambiwa UFANYE haraka.
Kulala ndio ishu, maana mnakabana Kama mihogo na joto hili. Vidirisha viko juu kabisa haviingizi hewa.
Ameapa hata Kama walokole watapiga mziki mpaka saa Tisa usiku. Hatowagusa.
Serikali wanasema wanaogopa kupata watoto wengi wa mitaani (Machokoraa)Wafungwa wote kwann wananyimwa haki ya kuzaa?
Cheo kinamzuzua huyo waziriKuna waziri wa Mambo ya ndani mzanzibar aliwahi kuulizwa bungeni
1. kwanini wafungwa wanakula Mara moja?
Waziri. Wanakula Milo mitatu Ila ili kuokoa muda wanaopewa hiyo Milo kwa wakati mmoja.
2. Kwanini wafungwa wanafanyana mapenzi kinyume na maumbile huku serikali ikilifumbia macho?
Waziri.
Kwani huku uraiani hakuna mashoga na mabasha?
Mzungu alileta jela,mwafrika akazirithi na sheria zake za kutesa watu.Waafrija akili duni sana, wazungu walisha boresha sheria za jela huko kwao wameruhusu mpaka kulala na mke anapokuja kukutembelea jela sisi wafungwa ni kufi $&rana tu halifu eti tunapinga ushoga huku ushoga ukiendelea kwenye majela.