Waishio milimani Jijini Mwanza watakiwa kuondoka kupisha mwekezaji

Ulivyo Soma ni sahihi kabisa wala hujakosea. Ndohabari ya mjini, zile nyumba zote zilizopo kwenye mountain inabidi zitoke jamaa wa Brazil aje ajenge na Familia yake...
Uwekezaji ni muhimu, Mwanza umejengwa ovyo ovyo sana. Mji upangwe na barabara zipanuliwe na hizo apartments zitasaidia kupunguza tatizo la makazi.

Watu waondoke milimani na hivyo shacks za milimani zivunjwe haraka sana, tunaingia uchumi wa kati huku tuna makazi duni. Zijengwe apartments za bei rahisi na wananchi wetu wajifunze kulipia. Hakuna njia ya mkato kwenye maendeleo.
 
Shamte analipa alichomfanyia baba yake.Baba yake alikuwa waziri mkuu Zanzibar akapinduliwa na kutiwa kizuizini halafu yeye Baraka akajiunga na ASP Kisha CCM.
 
Mradi unaonekana utaupendezesha jiji la Mwanza, wasiwasi wangu tu wananchi wanyonge walipwe stahiki zao kabla ya kuhamishwa na haki itendeke ktk tathmini ya mali za watu, maana jiji lisije onea watu ktk kutoa fedha zao kulingana na thamani halisi ya mali zao.
 
Ya ngorongoro yanakuja mwanza. Mioyo ijiandae tu kuyapokea
 
Kwanini hao wawekezaji hawaendi kujenga kule Chato kwa lihayati ma(ya)janga
 
Wakigoma itumike loliondo style
 
Mbona hii kitu ilikuwepo toka awamu ya nne jameni? Kigoto kuliwekwa beacon, Kiseke mlima wa Hali ya hewa, Igogo na Isamilo.Mwenda zake alijua huu mchongo na ndio uliompa kura Kanda ya Ziwa 2015 kwa kuchukua tatizo Hilo kuwa fursa kwake nakumbuka tukiwa CCM Kirumba ktk kampeni Wananchi wa maeneo husika walizirai na kulia akasema hakuna mtu kuguswa, so it's just a matter of time waje na Buzuruga
 
Mbona zanzibar hawauzi ila wanakodisha maeneo kwa wageni?
 
Mods badilisheni title ya mtoa mada imekaa kichochezi….Hata uwanja wa ndege wa kimataifa terminal two watu walihamishwa Sasa hivi kuna airport ya kisasa so sio ajabu
 
Kama ni kwaajili wa kuboresha madhari ya jiji naunga mkono hoja..tunaomba tu hiyo master plan yao tuione.

Mwanza ni jiji liendane na hadhi hiyo...pia wabakize baadhi ya vilima vipandwe miti ili kuleta hali nzuri ya hewa katikati ya mji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Buzuruga mlima upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…