Waislam, kwanini mnawafanya watu mediocre na laymen kuwa viongozi wa dini yenu tukufu?

Waislam, kwanini mnawafanya watu mediocre na laymen kuwa viongozi wa dini yenu tukufu?

Muislamu mjinga tu ndio atamsifia Dr Sulle

Mimi nimeanza kumkataa toka nipo form one niliposikia akidanganya kuhusu ukuta wa China kabla ya kujua udhaifu wake katika elimu ya dini na itikado yake.

Hao MaSheikh walikuwa wanakubalika zamani kipindi hiko Elimu ya dini kwa watu ni ndogo sana na watu hawasomi , sasa hivi popularity Yao imeshika sana hata Muislamu wa kawaida anajua kuwa Dr Sulle na wakina mazinge matapeli.

Kama ilivyokuwa kwa Wakristo Mwamposa , Tito , Zumaridi nk Wana wafuasi basi hata hao MaSheikh hawakosi wafuasi
Sulle ni Dr. Wewe usimchafue jamaa msomi na anajua sana maandiko
 
Nikiona waislamu wanavyomsifia shehe Sulle na jinsi alivyo na heshima kubwa kwao Huwa ndiyo nazidi kuchoka.

Jamaa ninmweupe na mwongo vibaya mno. Anasimulia jambo Huku confidence mlima Kilimanjaro lakini uongo mtupu.

Imagine siku Moja anawasimulia waislamu msikitini kuhusu habari ya Los Angeles na Las Vegas. Ilikuwa vituko yani hadi unaona aibu.

Ila ajabu watu wanashangilia balaa na kuita takbiiiiir na wakapata hadi confidence ya kuipakia ile video kwenye social media na akaendelea kusifiwa na waislamu wa mtanaoni!!!

Alooo nilichoka asee!!

Alafu Kuna huyu wa kuitwa Kishk

Sikiliza huu upupu.

Kwa heshima yake alitakiwa aongee hivi kweli? Na hii ilikuwa 2021 ila afande anazidi kudunda hadi Leo.
View attachment 3612664
😂😂😂😂
Hii ni maajabu.
Chanzo cha yote hayo ni Elimu Elimu Elimu
 
Ndugu zangu, Asalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Nimefuatilia mjadala huu kwa makini sana, na ni wazi kabisa umegusa mioyo ya wengi na kuibua maswali muhimu sana kuhusu uongozi wetu wa dini. Ni muhimu sana kama jamii kuweza kujadiliana masuala haya kwa uwazi na kwa lengo la kujenga.

Ni kweli, suala la uongozi ni nguzo muhimu katika jamii yoyote, na hasa katika dini yetu tukufu ya Uislamu. Kila mmoja wetu, bila shaka, anatamani kuona viongozi wetu wanakuwa mfano bora wa kuigwa, wenye elimu pana, hekima, na uwezo wa kuwakilisha dini yetu kwa namna inayoendana na hadhi yake.

Badala ya kukata tamaa au kuendelea kulalamika tu, labda tunahitaji kugeuza mjadala huu kuwa chachu ya mabadiliko chanya. Tuna Waislamu wengi sana wenye vipaji, elimu kubwa (ya dini na ya dunia), na weledi mkubwa. Labda changamoto ni jinsi gani tunawapa fursa na kuwahimiza kujitokeza na kuchukua majukumu haya muhimu.

Tunaweza kuanza kwa kuwekeza zaidi katika mifumo yetu ya elimu ya dini, kuhakikisha inatoa wasomi si tu wenye ujuzi wa Qur'an na Sunnah, bali pia wenye uelewa mpana wa masuala ya jamii na uwezo wa kujenga hoja zenye mantiki na za kistaarabu.

Pia, ni jukumu letu sisi kama waumini kuwapa sapoti viongozi wetu, na wakati huohuo kuwa na ujasiri wa kutoa maoni yenye kujenga pale tunapoona kuna haja ya kuboresha. Uislamu wetu ni mkubwa na unahitaji viongozi imara na wenye dira. Tuendelee kujadiliana kwa hekima na kutafuta suluhisho kwa pamoja, kwa lengo la kuinua hadhi ya dini yetu na jamii yetu kwa ujumla. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuchangia katika hili.
 
Upo sahihi Sana brother.

Nyie waislamu vijana na wasomi mnapaswa muokoe hili jahazi asee!

Hivi mfano wale jamaa waliokuwa wamepewa vipaza sauti kwenye press siku chache baada ya maandamano ya October wakijinasibu kuongea kwa niaba ya waislamu ukisikiliza tu yule ostaz aliyekuwa anaongea alivyo na jazba kwenye kuongea na maneno anayoongea unagundua hapa Kuna education barrier.

"Tutawakata vichwa"

"Kanisa tunazijua Mali zenu Huku mtaani. Tunazijua shule mnazomiliki, hospitals na taasisi zenu zingine...Nasemajee tutachoma moto nawaambia"

Na hawakuchukuliwa hatua.

Dini inaendelea kuzalisha maostaz wa aina hii Kila siku.

Vihiyo wanasimama madhabauni na kupewa kipaza kulisha watu neno la Mungu.

Siyo sawa.
Samuya na CCM wako nyuma yao
 
Yapu mkuu huea namuona mitaa ya buguruni yani ni choka mbaya.. ni wale wakushindankwenye mihadhara
Anapatikana sana pale Kariakoo gerezani kijiwe cha kahawa shule ya uhuru. Ni mfuasi mtiifu wa CAFU na Lipumba, yaan ukimkuta anajadiri mada za Dini au Siasa hadi anatokwa jasho. Ila mda wa kuondoka anaombaga nauli ya kwenda nyumbani. Anajitia msomi sana na mkongwe kwenye siasa kwamba alisomea siasa tangu kijana ingawa anaonekana anaelimu mbalimbali. Siku niliyomtoa maana ni siku alisema Tundu Lisu hawezi kumshinda yeye kwa hoja wakiwekwa meza moja kujadili jambo la kisiasa kwa sabab yeye alisomeshwa na CAFU mambo ya siasa na ameiishi siasa tangu kijana mdogo. Na uwasirishaji wake wa hoja ni kwa jaziba ila hoja zake ni nyepesi sana, jamaa ni mdini kwelikweli maana namuonaga mpaka kwenye mihadhara ya kina Mazinge.
 
Vile vijiwe vya kiwaki sana kuna mwanangu tulienda nae akawapangua kwa hoja..
Kumbe kati yao alikuwepo shehe mmoja maarufu wa kariakoo jina nimesahau ila hiwa anamtetea sana samia..
Bwana kidogo jamaa yangu atekwe na polisi kumbe kati anaondoka walikuwa wanafualtilia hadi bajaji aliyopanda hadi mitaa ya feri ndio kwenye purukushani anawatoka
 
Yaan shida ya waislam huwa ni kutumia logic kuchambua mambo 🤣 yaan lazima apate hasira na mihemko sijajua ni hapa tu Bongo au duniani kote.
Na nani sijui aliwaaminisha kwamba wanaweza kupigana 🤣 Jambo likitokea utasikia "eti waislam tukikiamsha hapa"
Ila jambo jema ni kwamba Millenium mna shida sana kuna mahala mlifanya ujinga na kubadilika kwenu ni changamoto. Kinakuja kizazi kipya kinachoweza kuchanganua mambo bila mihemko 🤣 Mambo ya dini yatatupwa kule
 
Na ndo maana kila mgogoro ukitokea wanaingiza udini ! Hata mgogoro wa Iran na USA walishaanza kujisemesha kwamba dini yao inapigwa vita 🤣 Maandamano ya 29 Oct wanasema wakristo hawamtaki Sa100, Juzi nimemsikia na mwanazuoni anasema wakristo hawataki Muungano 🤣
Isingekua Gen Z kuwa na akili tungefarakanishwa kishenzi hapa.
 
Nimewahi kukaa karibu na msikiti mmoja maeneo ya mjini ilikuwa ikifika mida ya Mawaidha Waarabu, Wahindi na baadhi ya matajiri huwa wanatoka wanaenda kwenye shughuli zao. Huku nyuma mahubiri yanayoendelea ni Tec wanapinga DP Word kwa sababu ni kampuni ya Waislamu, Hakuna kushiriki sikukuu za Wakristo ni makafir haramu.

Lile nginja la Wakatoliki hadi uwe kiongozi wa dini kama ulipanga uwe Padri utapeli watu lazima uteme bungo njiani.

Wenzetu process yao rahisi, kariri kuruani(sio kuelewa), ongea kwa ukali(ukali sio kujenga hoja) tayari wewe Sheikh.

Na hawaheshimiani hawa jamaa, utasikia huyo anaadhini vibaya, sheikh hapo anaswalisha vibaya. Ngumi nje nje.

Njooni mnipige nipo kwa Mtoro hapa.
😁😁😁😁

Soma mstari wa mwisho
Castle_Lite
secretarybird
 
Alafu Kuna huyu wa kuitwa Kishk

Sikiliza huu upupu.

Kwa heshima yake alitakiwa aongee hivi kweli? Na hii ilikuwa 2021 ila afande anazidi kudunda hadi Leo.
View attachment 3612664
hiyo kauli ya kishki aliyotoa kwa mihemuko haikuwa ya kubeza

Hii nchi ingekuwa ni Dola ya kikobazi Mpuuzii mmoja angemtenda kitu Sele

Na huyu Bwege angeamka asubuhi na kumshukuru Allah kwa kujibu ombi lake "Takibirr"

Kobazi wanzake "Allahusalimalee" imeeishaa iyo🤭
 
Ndugu zangu, Asalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Nimefuatilia mjadala huu kwa makini sana, na ni wazi kabisa umegusa mioyo ya wengi na kuibua maswali muhimu sana kuhusu uongozi wetu wa dini. Ni muhimu sana kama jamii kuweza kujadiliana masuala haya kwa uwazi na kwa lengo la kujenga.

Ni kweli, suala la uongozi ni nguzo muhimu katika jamii yoyote, na hasa katika dini yetu tukufu ya Uislamu. Kila mmoja wetu, bila shaka, anatamani kuona viongozi wetu wanakuwa mfano bora wa kuigwa, wenye elimu pana, hekima, na uwezo wa kuwakilisha dini yetu kwa namna inayoendana na hadhi yake.

Badala ya kukata tamaa au kuendelea kulalamika tu, labda tunahitaji kugeuza mjadala huu kuwa chachu ya mabadiliko chanya. Tuna Waislamu wengi sana wenye vipaji, elimu kubwa (ya dini na ya dunia), na weledi mkubwa. Labda changamoto ni jinsi gani tunawapa fursa na kuwahimiza kujitokeza na kuchukua majukumu haya muhimu.

Tunaweza kuanza kwa kuwekeza zaidi katika mifumo yetu ya elimu ya dini, kuhakikisha inatoa wasomi si tu wenye ujuzi wa Qur'an na Sunnah, bali pia wenye uelewa mpana wa masuala ya jamii na uwezo wa kujenga hoja zenye mantiki na za kistaarabu.

Pia, ni jukumu letu sisi kama waumini kuwapa sapoti viongozi wetu, na wakati huohuo kuwa na ujasiri wa kutoa maoni yenye kujenga pale tunapoona kuna haja ya kuboresha. Uislamu wetu ni mkubwa na unahitaji viongozi imara na wenye dira. Tuendelee kujadiliana kwa hekima na kutafuta suluhisho kwa pamoja, kwa lengo la kuinua hadhi ya dini yetu na jamii yetu kwa ujumla. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuchangia katika hili.
Naomba kukukumbusha chief....
Msingi wa elimu ya uislamu tangu hii nchi imepata kuwa nchi imesimama kwa kujitegemea na ndio maana ilishindwa kutengeneza mitaala ya kuisomesha kwa nyakati zile.

Ikumbukwe kipindi ilipofutwa EAMWS (East African Muslim Welfare Society) mwaka 1968.
Hapa ndipo ilikuwa kifo cha usimamizi mzuri wa uislamu ambao ulishindwa kujitengenezea misingi ya elimu endelevu.
Ni kipindi ambacho wenzetu wakatoliki wanapata pesa ya kuratibu elimu kwa kuboresha mashule na vyuo vyao vya dini kwa gawio la serikali jambo ambalo waislamu walishindwa sehemu ya kupata sapoti ya Nguvu pesa.

Na hii ilipelekea hata baadhi ya waislamu kutazama zaidi sehemu za kimaendeleo seqular ambako ni kwenye ajira na kuacha usomaji wa dini.
Wakati wenzetu wanatengeneza mwanafunzi from vidudu hadi Degree kasoma Seminari zao.

MITAALA KUENDANA NA MAKOLONI
Ikumbukwe pia endapo EAMWS (East African Muslim Welfare Society) na misingi walokajiwekea ya kujiunga na nchi za kiislamu basi pangekuwa na connection kubwa ya wahitimu wa kiislamu kwenda kuongeza elimu zao za juu kwenye nchi zenye mitaala yenye kushikamana na imani zao.
Mfano wa hayo ni kuwa kwa nyakati zote hapa Tz wasomi wengi waliofaulu kwa miaka ya nyuma walienda kusoma nje kwa kufuata mitaala tuliyoachiwa na wakoloni jambo ambalo lilikuwa haliwezekani ni kuukacha mtaala na kuanza kusoma Tahran kwenye lugha ya kiajemi.
 
Upo sahihi.

Ila nakukatalia hapo umesema "MaSheikh waliowahi kusoma dini Zamani wengi wamelisha sana watu matangapori"

Hawa wapo hadi Leo hivi tukiwa tunajadili hapa.

Hawa si ndiyo Huwa mnawaita maostazi na wanawafundisha watoto madrassa jioni wakitoka shule za kawaida?

Maostazi Bado ni weupe vibaya mno...Yani ni weupe Sanaa!

Miaka tu michache Kuna dogo wa miaka 6 alikuja ndani kwangu akakuta Nina play nyimbo za kwaya,ilikuwa jumapili baada ya kutoka kanisani...Aisee aliongea maneno mabaya sana baada ya kusikia kwaya inaimba kwenye redio. Tena kwangu!!

Imagine dogo wa miaka sita ananiambia "uncle,toa hizo nyimbo kwenye redio maana ni nyimbo za makafiri" nikamuuliza nani amekufundisha hivyo akajibu ostazi madrassa anawafundisha hivyo. Na dogo alishaanza kuwa extremist kwa kulishwa hayo maneno na "mwalimu wa dini".

Nilimtafuta yule dogo Ostaz nimjue nikaishia nkusikitika tu maana ni dogo mlala hoi tu anayejua Quran akakabidhiwa kundi la watoto wa kiislamu kama 30 we mwalimu.

Imagine hao watoto wanavyolishwa vichwani!!
Unaongeaga pointi.
Ila anaposema zamani haina maana kwamba wote wamebadilika haiko hivyo.
Ni kama uonavyo kwenye ukristo mbele ya elimu mnayoipigia kelele kuwa ndio muhimu ila bado kuna wachungaji ni zero kabisa.
Ila anachokusudia ni kuwa leo hii muumini anayo nafasi ya kufanya tafiti wapi akasome au wapi ampeleke mwanawe na hii inatokana na waumini kufahamu hapa tunapigwa na hapa ni sahihi..
Ila kwa zamani ilikuwa ni ngumu kuchuja Wewe utampeleka popote na chochote atakachokileta mtoto nyumbani kilionekana ni dini.
 
Muislamu mjinga tu ndio atamsifia Dr Sulle

Mimi nimeanza kumkataa toka nipo form one niliposikia akidanganya kuhusu ukuta wa China kabla ya kujua udhaifu wake katika elimu ya dini na itikado yake.

Hao MaSheikh walikuwa wanakubalika zamani kipindi hiko Elimu ya dini kwa watu ni ndogo sana na watu hawasomi , sasa hivi popularity Yao imeshika sana hata Muislamu wa kawaida anajua kuwa Dr Sulle na wakina mazinge matapeli.

Kama ilivyokuwa kwa Wakristo Mwamposa , Tito , Zumaridi nk Wana wafuasi basi hata hao MaSheikh hawakosi wafuasi
Kabisa mkuu, umenena vyema.
 
Mnashindwa kutofautisha baina ya masheikh Siasa na Masheikh wa Dini.
MASHEIKH DUNIA ni yoyote yule anayetumia umaarufu alioupata kwenye dini kwa njia yoyote ile iwe kwa mihadhara, Mijadala, Tiba za asili au ujanja janja...
Na hao ndani yao huwa wengi wao si wabobezi wa elimu ya dini isipokuwa kwa uchache sana na sehemu kubwa ni hao wa mijadala wengi kwenye uislamu kiundani hamna kitu ila kutokana na madhaifu ya kwenye biblia na lugha ya kiswahili imewapa fulsa wao kuogelea wawezavyo hapo ndio utawakuta akina Sule, mazinge, Bakozi na mfano wake ila wanasaidia kwa kiwango kikubwa kuwaleta wafuasi wa imani nyingine kwenye uislamu.

MASHEIKH DINI hapa utakuta wengi wengi wao si maarufu kwenye jamii na kwenye social media ndio nadra sana kuonekana na hawa hata ukikaa kuwasikiliza hujutii muda wako.
Na hata ukibaini kasoro utajua hii ni ya kibinadamu na si kielimu na hii haiuhusiani na tofauti za kiitikadi.
Kwenye JF wengi hupima hoja kwa milengo ya kisiasa basi pata muda fuatilia Video za uamsho Zanzibar kipindi cha akina Sheikh Mselem ukiwa hauna ushabiki utajua ni Sheikh wa aina ipi.
 
Back
Top Bottom