Waislam, kwanini mnawafanya watu mediocre na laymen kuwa viongozi wa dini yenu tukufu?

Waislam, kwanini mnawafanya watu mediocre na laymen kuwa viongozi wa dini yenu tukufu?

Mnashindwa kutofautisha baina ya masheikh Siasa na Masheikh wa Dini.
MASHEIKH DUNIA ni yoyote yule anayetumia umaarufu alioupata kwenye dini kwa njia yoyote ile iwe kwa mihadhara, Mijadala, Tiba za asili au ujanja janja...
Na hao ndani yao huwa wengi wao si wabobezi wa elimu ya dini isipokuwa kwa uchache sana na sehemu kubwa ni hao wa mijadala wengi kwenye uislamu kiundani hamna kitu ila kutokana na madhaifu ya kwenye biblia na lugha ya kiswahili imewapa fulsa wao kuogelea wawezavyo hapo ndio utawakuta akina Sule, mazinge, Bakozi na mfano wake ila wanasaidia kwa kiwango kikubwa kuwaleta wafuasi wa imani nyingine kwenye uislamu.

MASHEIKH DINI hapa utakuta wengi wengi wao si maarufu kwenye jamii na kwenye social media ndio nadra sana kuonekana na hawa hata ukikaa kuwasikiliza hujutii muda wako.
Na hata ukibaini kasoro utajua hii ni ya kibinadamu na si kielimu na hii haiuhusiani na tofauti za kiitikadi.
Kwenye JF wengi hupima hoja kwa milengo ya kisiasa basi pata muda fuatilia Video za uamsho Zanzibar kipindi cha akina Sheikh Mselem ukiwa hauna ushabiki utajua ni Sheikh wa aina ipi.
Uislam ni dini na taasisi kubwa duniani
Ni aibu kuona hao akina Sulle, Balozi ndo viongozi wa dini
Yaani unaona jitu ni zero brain ila liko kwenye mimbari linatoa hotoba kama mtoto wa chekechea
Wapo waislam Maprofesa, PhD, Degrees
Kwanini wasichukue hizo nafasi?

Ona waislam wenzenu wa Iran, Saudia, Oman kiongozi wa dini akiongea, unamuona mtu Smart na anajua mambo Kwa ukubwa
 
Dini ya uislam pamoja na kuwa na mafunzo mazuri ila Bado watu makini hawataki kuwa viongozi wa dini hiyo

Kwanini hao mashehe wasijielimishe ili kupata haiba na kutoa maoni yanayoendana na uelewa na ustaarabu

Jiulize
Muislam kama Bakhresa anakaa kwenye zulia anamsikiliza Shehe Mazinde😂 anayeona kuandamana ni fujo

Muislam makini kama Mzee Kikwete anakaa anamsikiliza mufti Zuberi😂 Mzee wa maridhiano na muandamo wa mwezi

Muislam makini kama Professor Assad anakaa massa 2 anasikiliza mawaidha ya Shehe Kipozoeo 😂

Chief Judge Ibrahim Juma anatulia anamsikiliza Shehe Sharif Majini

Jamani ndugu zangu waislam jaribu kufanya recruitment nzuri ya viongozi wenu wa dini

Viongozi wa dini wanabeba taswirq ya uislam

Sio hao mashehe wao wanaomba mapumziko siku ya mwaka wa mtume

Hao viongozi wenu wanaosifia mauaji ya oktoba 29, hawafai

Kuna waislam makini ambao binafsi nawaheshimu ila hawa viongozi hapanaView attachment 3612762
Kuna uhitaji wa kuweka sharti ili viongozi wa dini angalau wawe na elimu ya form VI au certificate ya circular education. Ni hatari sana mtu ambaye hajakanyaga darasani kupewa nafasi ya kuwa kiongozi wa dini.
Baadhi ya mafundisho ya dini yanahitaji kiwango flan cha elimu ya kidunia kuyaelewa na kuyafundisha kwa usahihi.
 
Nikiona waislamu wanavyomsifia shehe Sulle na jinsi alivyo na heshima kubwa kwao Huwa ndiyo nazidi kuchoka.

Jamaa ninmweupe na mwongo vibaya mno. Anasimulia jambo Huku confidence mlima Kilimanjaro lakini uongo mtupu.

Imagine siku Moja anawasimulia waislamu msikitini kuhusu habari ya Los Angeles na Las Vegas. Ilikuwa vituko yani hadi unaona aibu.

Ila ajabu watu wanashangilia balaa na kuita takbiiiiir na wakapata hadi confidence ya kuipakia ile video kwenye social media na akaendelea kusifiwa na waislamu wa mtanaoni!!!

Alooo nilichoka asee!!

Alafu Kuna huyu wa kuitwa Kishk

Sikiliza huu upupu.

Kwa heshima yake alitakiwa aongee hivi kweli? Na hii ilikuwa 2021 ila afande anazidi kudunda hadi Leo.
View attachment 3612664
Mambo ya dini hayana ushahidi, ni Imani. Sasa usipokomaa kutetea uongo utahojiwa utoe ushahidi ambao haupo.
 
Kama Baba yako tu aliwaokota watu wajinga akawa anawalisha matango pori na itikadi za kishirikina

Wewe maamuma. Humfikii mzee wangu al hadj we kidampa hata quran huifahamu. Huna elimu yoyote kiazi wewe maamuma.
 
Uislam ni dini na taasisi kubwa duniani
Ni aibu kuona hao akina Sulle, Balozi ndo viongozi wa dini
Yaani unaona jitu ni zero brain ila liko kwenye mimbari linatoa hotoba kama mtoto wa chekechea
Wapo waislam Maprofesa, PhD, Degrees
Kwanini wasichukue hizo nafasi?

Ona waislam wenzenu wa Iran, Saudia, Oman kiongozi wa dini akiongea, unamuona mtu Smart na anajua mambo Kwa ukubwa
Labda tatizo lako ni ufahamu.
Tanzania nimesema uislamu haukuwa na utaratibu huo na hiyo ilichagizwa na uchache na wasomi wa elimu ya dini ndio maana wale wachache waliosoma waliachiwa mimbari alafu nikasema watu kama akina Sule na akina bakozi hao sio masheikh kwenye usichokijua ni kuwa kwenye uislamu kuna madaraja ya kielimu ambayo nayo si ya kuzingatiwa saaana madaraja kama Sanaw, mutawasitwa, Doktowra...
Kwenye hiyo list ndio unakuta maana ya Diploma, Degree na Dokta....
Ila hao wanaokushughulisheni huko wengi wao hawana hata cheti kimoja kwa maana elimu zao ni za kuungaunga...
 
Kuna uhitaji wa kuweka sharti ili viongozi wa dini angalau wawe na elimu ya form VI au certificate ya circular education. Ni hatari sana mtu ambaye hajakanyaga darasani kupewa nafasi ya kuwa kiongozi wa dini.
Baadhi ya mafundisho ya dini yanahitaji kiwango flan cha elimu ya kidunia kuyaelewa na kuyafundisha kwa usahihi.
Duh yaani nyie jamaa mmechezewa sana bongo zenu.
Sasa elimu ya form 4 inamahusiano gani na elimu ya kiislamu.
Na hayo ni yaleyale tuyaonayo mnampima elimu kiongozi wa dini kwa kumuelizea panzi alivyo.
Kwenye uislamu Seqular nafasi yake ni finyu sana ila uislamu huo huo unafundisha hadi udaktari sema kwenye hizi nchi zetu mitaala haitutambui.
 
Ukiwa msomaji mzuri wa hivi vitabu vya dini ni rahisi sana kuwatambua matapeli ya dini.
N
Ndugu zangu, Asalamu Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

Nimefuatilia mjadala huu kwa makini sana, na ni wazi kabisa umegusa mioyo ya wengi na kuibua maswali muhimu sana kuhusu uongozi wetu wa dini. Ni muhimu sana kama jamii kuweza kujadiliana masuala haya kwa uwazi na kwa lengo la kujenga.

Ni kweli, suala la uongozi ni nguzo muhimu katika jamii yoyote, na hasa katika dini yetu tukufu ya Uislamu. Kila mmoja wetu, bila shaka, anatamani kuona viongozi wetu wanakuwa mfano bora wa kuigwa, wenye elimu pana, hekima, na uwezo wa kuwakilisha dini yetu kwa namna inayoendana na hadhi yake.

Badala ya kukata tamaa au kuendelea kulalamika tu, labda tunahitaji kugeuza mjadala huu kuwa chachu ya mabadiliko chanya. Tuna Waislamu wengi sana wenye vipaji, elimu kubwa (ya dini na ya dunia), na weledi mkubwa. Labda changamoto ni jinsi gani tunawapa fursa na kuwahimiza kujitokeza na kuchukua majukumu haya muhimu.

Tunaweza kuanza kwa kuwekeza zaidi katika mifumo yetu ya elimu ya dini, kuhakikisha inatoa wasomi si tu wenye ujuzi wa Qur'an na Sunnah, bali pia wenye uelewa mpana wa masuala ya jamii na uwezo wa kujenga hoja zenye mantiki na za kistaarabu.

Pia, ni jukumu letu sisi kama waumini kuwapa sapoti viongozi wetu, na wakati huohuo kuwa na ujasiri wa kutoa maoni yenye kujenga pale tunapoona kuna haja ya kuboresha. Uislamu wetu ni mkubwa na unahitaji viongozi imara na wenye dira. Tuendelee kujadiliana kwa hekima na kutafuta suluhisho kwa pamoja, kwa lengo la kuinua hadhi ya dini yetu na jamii yetu kwa ujumla. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuchangia katika hili.

Umechangia hoja kihekima sana. Kwa kweli viongozi wengi wa dini ya kiislam ni aibu kubwa. Ni kutokana na uwezo wao mdogo wa uelewa, ndiyo maana hata viongozi wa CCM wenye dhamira mbaya huwatumia viongozi wa waislam, hasa walio chini ya BAKWATA. Wale wa Shura ya Maimamu, kwa sababu wana uelewa, hawawagusi.
Kwanza kile kitendo cha serikali kuanzisha BAKWATA, halafu kuwapa waislam na kuwaambia kuwa hii ndiyo taasisi yenu, ilikuwa ni aibu na dharau kubwa kwa waislam.
Taasisi yoyote inapoanzishwa, ili kupata usajili, huwa ina mwongozo ulioandaliwa, sasa mwongozo wa BAKWATA uliandaliwa na viongozi wa serikali! Ndiyo maana CCM imeifanya BAKWATA kuwa jumuia zake katika uhalisia lakini kiubandia, inatajwa kuwa ni taasisi wakilishi ya waislam wote, upende usipende.

Bila waislam kuinuka na kuwakata mashekhe bandia wa BAKWATA, na kuikataa BAKWATA, na kisha kuanzisha taasisi wakilishi wao wenyewe yenye kuweka mwongozo wa namna na sifa zinazohitajika mtu kuwa kiongozi wa kiimani wa waislam, hawa mashekhe bandia wasio na upeo, wataendelea kuudharaulisha uislam.
 
Wewe maamuma. Humfikii mzee wangu al hadj we kidampa hata quran huifahamu. Huna elimu yoyote kiazi wewe maamuma.
Mzee wako Allaah amsamehe , alichanganya dini na mambo ya ushirikina watu wakamdhania Shekhe kumbe hamna kitu na hao ndio MaSheikh wa zamani walioharibu dini kwa kuleta mambo mengi ambayo sio ya dini , walikubalika sababu kipindi hiko watu hawakusoma na hawana exposure.

Umeona wapi kama sijui Qur'an ?
 
Duh yaani nyie jamaa mmechezewa sana bongo zenu.
Sasa elimu ya form 4 inamahusiano gani na elimu ya kiislamu.
Na hayo ni yaleyale tuyaonayo mnampima elimu kiongozi wa dini kwa kumuelizea panzi alivyo.
Kwenye uislamu Seqular nafasi yake ni finyu sana ila uislamu huo huo unafundisha hadi udaktari sema kwenye hizi nchi zetu mitaala haitutambui.
Uislam unafundisha hadi udaktari😂
Ile nyie kobazi
 
Nikiona waislamu wanavyomsifia shehe Sulle na jinsi alivyo na heshima kubwa kwao Huwa ndiyo nazidi kuchoka.

Jamaa ninmweupe na mwongo vibaya mno. Anasimulia jambo Huku confidence mlima Kilimanjaro lakini uongo mtupu.

Imagine siku Moja anawasimulia waislamu msikitini kuhusu habari ya Los Angeles na Las Vegas. Ilikuwa vituko yani hadi unaona aibu.

Ila ajabu watu wanashangilia balaa na kuita takbiiiiir na wakapata hadi confidence ya kuipakia ile video kwenye social media na akaendelea kusifiwa na waislamu wa mtanaoni!!!

Alooo nilichoka asee!!

Alafu Kuna huyu wa kuitwa Kishk

Sikiliza huu upupu.

Kwa heshima yake alitakiwa aongee hivi kweli? Na hii ilikuwa 2021 ila afande anazidi kudunda hadi Leo.
View attachment 3612664
😅😅😅
 
Labda tatizo lako ni ufahamu.
Tanzania nimesema uislamu haukuwa na utaratibu huo na hiyo ilichagizwa na uchache na wasomi wa elimu ya dini ndio maana wale wachache waliosoma waliachiwa mimbari alafu nikasema watu kama akina Sule na akina bakozi hao sio masheikh kwenye usichokijua ni kuwa kwenye uislamu kuna madaraja ya kielimu ambayo nayo si ya kuzingatiwa saaana madaraja kama Sanaw, mutawasitwa, Doktowra...
Kwenye hiyo list ndio unakuta maana ya Diploma, Degree na Dokta....
Ila hao wanaokushughulisheni huko wengi wao hawana hata cheti kimoja kwa maana elimu zao ni za kuungaunga...
Ndo maana nimesisitiza mashehe wawekewe kiwango cha elimu kama qualifications muhimu hata degree 1.
Unaona kama wakatoliki wana watu smart yaani Padre au Askofu akiongea unaona tofauti na mashehe ubwabwa.
 
Ukishakumaliza haja tumia pia na maji kujisafisha
Kobazi ndo maana watu makini tunawadharau
Yaani mtu mjinga unasikiliza na kufanyiq kazi ya Shehe Kipozoeo na Sulle utakuwa na akili kweli
 
Kobazi ndo maana watu makini tunawadharau
Yaani mtu mjinga unasikiliza na kufanyiq kazi ya Shehe Kipozoeo na Sulle utakuwa na akili kweli
Sulle kamtoa nduki Pastor wako Ndacha Sasa anasema utatu Mtakatifu ni ushoga 😝😝😝
 
Mleta mada anaeleweka mbona,mkuu

Anapotaja "viongozi wa kiislamu" hamaanishi cheo cha kitaifa au kwenye dini kwa ujumla ila anamaanisha kuwa Hawa ni viongozi tuliowakabidhi madhabau alafu sisi tukakubali kuwa waumini na kuhubiriwa.

Ngoja nikupe mfano.

Wakati nakua mitaa ya Temeke kule Kuna dogo Rika langu kipindi hiko alikuwa ni mtu wa dini sana. Yeye ni swala Tano na ni mtu mzuri sana.

Ila alikuwa na tatizo Moja la msingi.... Amesoma Quran na akapewa darasa awe anafundisha madrassa watoto..mnaita Chuo si ndiyo? Ila hakubahatika kwenda shule ya kawaida nadhani aliishia la tatu au la nne. Yani Hana elimu hata ya darasa la 7.

Miaka imeenda na sasa jamaa cheo kimepanda kutoka kuwa ostaz hadi kuwa Shehe anayesimama madhabauni kuswalisha na kutoa mawaidha.

Huyu mtu ndiyo tumfanye kuwa ni benchmark.

Ana influence katika dini kwenye eneo lake.

Akiongea anasikilizwa kama kiongozi.

Kama Kuna mgogoro wa kidini baina ya waumini wa kiislamu na wa dini nyingine pengine tunatarsjia atakuwa kwenye panel ya maamuzi.

Mfano miaka ya 2011 au 2012 Kuna yule dogo (wa kikristo ) kule mbagala aliyegombana na mwenzie(wa kiislamu) kisha mtoto wa kiislamu akamwambia kama wewe mwanaume kojolea hiki kitabu(ilikuwa juzi ile wanayofundishia maostaz) na kweli dogo akakojolea ile juzuu...waislamu waliposikia ile story ya "hear and say" wakaandamana mbagala barabarani kumtafuta MTU 'aliyechoma Quran" bila kufanya reasoning Wala kutaka kujua nini kilitokea kabla ya tukio na huyo aliyechoma siyo mtu mzima Bali ni mtoto na ilikuwa katika kugombana,na hajachoma kitabu cha Quran.

Polisi ikabidi waingilie kati.....Sasa swali mkuu,

Shehe wa aina hii anaweza kuwa na diplomasia ya kutatua mgogoro kama huu?

Ndiyo unakuta watu kama Hawa wanaongea upupu na hata wakiwa kwenye mikusanyiko ya kijamii yenye kutoa maamuzi hufanya mambo ya ajabu sana.

Si unaona baada ya matukio ya October jinsi mashehe wanavyotoa maboko hadi wanaumbuliwa na waislamu wenzao mitandaoni?

Ukiangalia shida kubwa ni elimu tu na Wala siyo kingine.

Wengi wao ni weupe sana kichwani.
Unlike Wakristo waisilamu tunaswali mara 5 na tuna misikiti kila sehemu, probably kuna misikiti mingi kuliko hata Shule, so kuna uhaba pia wa hao maimamu na walimu wa Chuo, MTU anayekabidhiwa Chuo haimaanishi ni kiongozi wa waisilamu. Kuchukua random mwalimu wa madrasa kwenye mskiti mmoja Kati ya maelfu ya misikiti na kumhusisha na uongozi wa Uisilamu ni tatizo lako.

Wakristo wengi mna tatizo kubwa la kuchukua standard zenu na kuona wengine wote wanafuata Standard kama zenu.
 
Back
Top Bottom