Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

1.Kukariri Quran sio dhambi
2. Quran ina tafsiri yake wapo waliokariri pamoja na tafsiri yake (hapo hauwezi kusema kuwa haelewi kinachosomwa )
3.Kutafsiri Quran pia ni fani kama fani zingine kwenye dini kuna ambao wana umahiri wa juu na wengine umahiri wa wastan pia wapo ambao hawajasoma madrasa hivyo hawajui tafsiri hata ya sura moja
 
And you are a black man whose defence mechanism kicked in to protect arabs.
Hapana this is not about proctecting arabs tunajibu maswali kama yanavyokuja ila ukiangalia mtiririko wa mada ni kwamba mada ilivyoanza na inavyoendelea ni kama sion hoja za msingi yaan likijibiwa hili linazuka jingine
 
Hayo mashindano hayana maana yoyote ikiwa wanaoshindana na wanaoandaa , na wanaohudhiria mashindano hawaelewi maana. Nguvu nyingi ingetumika kuwafundisha waislam waielewe Quran na waitumie kama muongozo wa dini
Wa ku judge kwamba hayana maana hauwez kuwa wewe kwa kuwa sio mlengwa as long as yapo bas walengwa wameona maana yake ni kama vile muislam aseme kina Mwamposa na Kiboko ya wachawi wafungiwe hawana msaada kwa jamii.
 
Kutokuwa na maana haimaanishi kwamba yafungiwe, unaweza tu kuwaacha watu waendelee na mambo yao ya kujifurahisha ilimradi hayana madhara kwa wengine na pia kwa ajili ya kutunza amani.
 
Hakuna tatizo kukariri Qur'an bila kuielewa
Ila ni mbora ambaye ameikariri Qur'an na kuielewa na kuifanyia kazi na kuifundisha
Kiarabu kama mtu anapojifunza lugha nyingine yoyote uelewa wa watu uko tofauti wengine wanazungumza kiufasaha zaidi wengine wanajitahidi na wengine hawajui kabisa
Ila kwa kuangalia hayo yote kujifunza kusoma Qur'an ni jambo la lazima maana kuijua kuisoma Qur'an ni muhimu katika ibada za muislam, na pia mtu anaweza kuijua kuisoma Qur'an na kuielewa pasi na kuwa mtaalamu wa lugha ya kiarabu na ALLAh anajua zaidi.
 
Mh
Quran imeandikwa kiarabu ila kiarabu si Quran maandishi ya kiarabu yanatofautiana na ya kwenye Quran kwa kuwa huwa hayana irabu(aeiou) kwa hyo anaesoma Quran tupu hawez kusoma kiarabu unless amesoma kiarabu ama kwa lugha nyingine kiarabu kinasomwa kwa kujua maana na muundo wa maneno.
Mngoni
 
Sasa unauliza ya nini kama ukifahamishwa hutaki? nenda huko ambako unajua utapata majibu ya watu unaowataka kama ya JF hutaki..

Nyie nia yenu ni kuukashifu Uislamu tu hamna lolote

Dini yenu imewashinda mnahangaika na Uislamu..

KWA TAARIFA YENU SISI SIO MAKONDOO MTUACHE NA DINI YETU
Huna hatimiliki na dini na pia hapa sio msikitini au kanisani kwamba kila kinachosemwa na muumini wa dini husika ndivyo kilivyo hakiwezi kuhojiwa zaidi au kuonekana hakina mashiko.
 
Kutokuwa na maana haimaanishi kwamba yafungiwe, unaweza tu kuwaacha watu waendelee na mambo yao ya kujifurahisha ilimradi hayana madhara kwa wengine na pia kwa ajili ya kutunza amani.
Ndo maana nikasema wa kusema hayana maana hauwezi kuwa wewe kwa kuwa sio mlengwa siku walengwa wakona hayana maana watayaacha ama kuyaboresha kwa sasa hili kwako ni kama ile pilipili ya shamba yakuwashia nn
 
Bado sijaelewa unatofautisha vipi Kiarabu na lugha iliyoandikwa quran,
Japo sipendagi kushiriki hii midahalo ila hili swali ni la kijinga ! Ila ntakujibu as a polyglot
Old English inafanana na English ya saivi?
Kiarabu kuna Modern standard arabic na classical arabic. Huwezi kufananisha Arabic ya karne ya 6 na arabic ya sasaivi.
Qur-an ni classical Arabic sio hii Arabic ya saivi, unaweza kusoma classical Arabic and still barely communicate with the natives! Hata ukisoma MSA bdo kuna baadhi ya native Arabic speakers ukashindwa kuzungumza nao! Mbona ni kawaida sana kwenye lugha mkuu?
 
Hata usiende mbali huko mtafute huyu huyu mpe Interview ya Harry kane kama clip ya dakika moja halafu aseme kaelewa maneno mangapi, bila subtitle.
 
Swali ni Hili ni wangapi wanaongea kiswahili fasaha katika sisi watanzania? Jibu unalo, ninachojua lugha ni kuelewana mkielewana imeisha hiyo, huo ufasaha tuwaachie wanaotafta mavyeti, zingatia kabla hujauliza ufasaha kwenye Kiarabu au kizungu ni wangapi wanaweza kiswahili fasaha?
 
Kitu ambacho wakristo wengi hawaelewi.
Busara ya kuacha Qur-an katika lugha yake ya asili ni kuepuka maandiko kupotea, huwezi kufasiri exactly kitu kutoka kwenye lugha moja kwenda kwenye lugha nyingine lazima kuna maana itapotea. Na ndio mana hata Qur-an imebaki kwenye classical Arabic ambayo hakuna anayezungumza kwa sasaivi! Kama ilivyokuwa old English au latin. Ingekuwa rahisi basi ungeona Qur-an imeshafasiriwa kwenda kwenye Modern Standard Arabic lakini la hasha, huwezi kukuta hiko kitu. Eti Qur-an ya kiswahili, au kihaya NEVER. Mwenyezimungu aliapa kukilinda hiki kitabu kitakatifu na kitabaki kama kilivyoshushwa haijalishi itapita miaka mingapi

saivi ukijaribu kuifasiri Qur-an kutoka kwenye classical arabic (lugha iliyokomaa kimsamiati) ukaleta kwenye kiswahili bila kupoteza maana! Haiwezekani
Na hii ndiyo inayofanya bible kupoteza muundo wake kadiri miaka inavyoenda (No hard feelings) hata sisi waislamu tunaamini katika Zaburi, Injili na torati lakini sio hii iliyopinduliwa pinduliwa!
 
Japo sipendagi kushiriki hii midahalo ila hili swali ni la kijinga ! Ila ntakujibu as a polyglot
Old English inafanana na English ya saivi?
Kiarabu kuna Modern standard arabic na classical arabic. Huwezi kufananisha Arabic ya karne ya 6 na arabic ya sasaivi.
Qur-an ni classical Arabic sio hii Arabic ya saivi, unaweza kusoma classical Arabic and still barely communicate with the natives! Hata ukisoma MSA bdo kuna baadhi ya native Arabic speakers ukashindwa kuzungumza nao! Mbona ni kawaida sana kwenye lugha mkuu?
Kwamba wanaosoma madrasa wanafundishwa na wanaelewa classical Arabic ndio maana hawawezi kuwasiliana katika modern standard Arabic bila kujifunza tena kiarabu cha kisasa?
 
Hapana this is not about proctecting arabs tunajibu maswali kama yanavyokuja ila ukiangalia mtiririko wa mada ni kwamba mada ilivyoanza na inavyoendelea ni kama sion hoja za msingi yaan likijibiwa hili linazuka jingine
Mtoa mada alijaribu kusugarcoat maelezo hakutaka kwenda direct.
Hoja yake ilikuwa wazi sana sema tu ile watu kuwa watetezi wa kitu wanachoamini ndio maana unaona yanazuka mengi. Na utetezi wa wengi umebase kwenye vitu vya kufikirika.

There is nothing worth of defending bro.
I speak As a pro black man not under any religious group.
Hivi huwa mnajisiaje mkuu mnapobishana kutetea dini zenu?
 
Imeletwa mada na tumejibu ulitaka tufanyaje? Inaonekana furaha yako ni kuona tumeshindwa kujibu au tunajibu kwa hasira ila bahati nzuri tunawapa majibu kiungwana tu wala hatupaniki
 
Mkuu unadhihaki basi tu ila deep inside unajua wazi kabisa Mkristo aliyesoma Kingereza Biblia anasoma vizuri tu na hata lugha anaongea na kuelewa japo sio kwa asilimia mia ila mawasiliamo yanafanyika vizuri.

Fanya homework mtafute Muislamu aliyesoma Kingereza mpe Bible uone kama atashindwa kusoma na kuelewa. Akimaliza mpe gazeti la kiarabu halafu leta mrejesho.
Sasa kitabu ukikisoma kinafahamika kirahisj kitabu hicho mwandishi akina atakuwa Nyerico Nyenyere . Kitabu kilichoandikwa kitaalam ufahamu wake pia unahitaji utulie ili ukifahamu
 
Kwamba wanaosoma madrasa wanafundishwa na wanaelewa classical Arabic ndio maana hawawezi kuwasiliana katika modern standard Arabic bila kujifunza tena kiarabu cha kisasa?
Unachotakiwa kufahamu! Lugha ya kiarabu ina lahaja nyingi kama Maghreb, hasaniyya, egyptian, syrian, na kadha wa kadha. MSA ni standardized version ya kiarabu hata natives wengi (isipokuwa wasomi) pia hawaongei ijapokuwa kwa kiasi flani mnaweza kuelewana, na ukienda nchi zinazozungumza kiarabu only wale educated ndo unakuta wanazungumza MSA.
Kuna classical arabic, msa na colloquial (hii sasa ndo inayozungumzwa na iko tofauti kulingana na eneo hapa ndo unakutana na hizo hassaniyya, maghrebi, egyptian etc).
Pale madrasa wengi hufundisha MSA (Modern Standard Arabic) ijapokuwa kwa namna flani ni rahisi kuelewa classical Arabic baada ya kusoma MSA and vice versa. Kusoma MSA haimaanishi kwamba wewe utakuwa rahisi kwako kuwasiliana na native Arabic speaker, kwasababu utkuwa na misamiati anatumia huijuwi na halikadhalika kuna misamiati unatumia yeye haijuwi
 
Badilisha simu yako kwenda arabic, halaf mpe aitumie kama ataweza
Utagundua wengi wanakariri lakini si kuelewa lugha yenyewe

Ni wachache sana wanao elewa hiyo lugha
Ukisoma madrasa unafundishwa na lugha ya kiarabu ili ukijue vizuri inabidi usiishie njiani na usome zaidi nje ya madrasa
 
Back
Top Bottom