Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Warioba alimthibitishia kuwa barua ya kujiuzuru ni yake
 
Ukweli ni kuwa barua ya kujiuzulu Chimbi hajaandika yeye bali imeandikwa na wasiojulikana na ndo hao wanajua alipo mpaka sasa. Inasikitisha watanzania tumetulia tuli kama hakuna kilichotokea
Msikilize Sinde Warioba aliyeongea naye kuhusu kujiuzuru
 
Vitapatikana utakapoambiwa uviweke kama ni kwa katibu, mlinzi au mtu yeyote atakayeagizwa avichukue.

Halafu kwani mtu akifa ghafla huwa vinapatikanaje ??
Ukifa ghafla hakuna mambo ya kukabidhiana, kwani hata kamq kuna mapungufu marehemu hawezi jibu. Ukiwa hai lazima ukabidhi ofis/mali za watu
 
Kwa nini sio Bunge. Swali linalo thibitishwa na hii hatua ya Pili baada ya kuona ya Kwanza imeshindwa kufanya kazi.ndiyo ikawekwa , ya kufukuzwa Chama.
1. kuhusu kwanini si bunge , swali hili linaweza kua gumu kama hakuna uainishwaji wa wazi kuhusu makamo --- kwasababu pia mtu mwingine anaweza akasema kwanini taarifa hiyo ya makamu wa rais kujiuzulu asimpe Spika , kama ambavyo Rais akijiuzulu taarifa anampa Spika


2. kuhusu kwanini wameamua kumfukuza chama , tunaweza lipima katika muktadha kadha wa kadha

kwanza kwa maelezo ya katiba suala la kujiuzulu halihitaji ruhusa au mtu yeyote kuridhia

sura ya kumi ya katiba MENGINEYO

149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kaziyoyote iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kaziya Waziri, Naibu Waziri au Mbunge, isipokuwaMbunge ambaye ni Mbunge kwa mujibu wamadaraka ya kazi yake), aweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiwa sahihi kwamkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo:


mpaka hapo tunaona kwamba kujiuzulu kunahitaji wewe mshika dhamana kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiwa saini yako katika sehemu husika , ni taarifa na sio kuomba kujiuzulu

sasa makamu anampa nani hapa kwa kweli inategemea na tafsiri ya maneno kwani

149. (1) -
(a) iwapo mtu huyo aliteuliwa au alichaguliwa na mtu mmoja, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu; atawasilishakwa mtu huyo aliyemteua aukumchagua, au iwapo aliteuliwa au alichaguliwa na kikao cha watu, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ata iwasilisha kwenye kikao hicho;

swali hapa ni je makamu wa rais anaingia kwenye maneno hayo? kama ndivyo basi taarifa yake atampa Rais.
Kama sivyo wajuzi wasaidie maana vifungu vinavyofata ni

(b)iwapo mtu huyo ni Rais, basi taarifahiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwaSpika;
(c)iwapo mtu huyo ni Spika au NaibuSpika wa Bunge, basi taarifa hiyo yakujiuzulu ataiwasilisha kwenyeBunge; na
(d)iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilishakwa Spika.

ikiwa katiba inatambua kwamba makamu wa rais anaweza kujiuzulu na kwenye mambo ya kujiuzuu yenyewe ni mambo ya kutoa taarifa tu --- naona ni easy win kwao , Nani anathibitisha hizo taarifa ? labda tutafute kanuni

pili , wamemfukuza labda waliona wanachelewa sana kungoja sept 4 , kama ambavyo taarifa ya katibu mkuu kiongozi ilivyosema rais amepokea barua ya ombi la kujiuzulu makamu kuanzia sept 4

tatu, kumkomoa tu nadhani maana ile taarifa kwa umma kupitia kurasa za mtandaoni ilisema amemuandikia barua mheshimiwa rais kumjulisha kua ameamua kustaafu siasa na utumishi wa umma hivyo atajiuzulu nafasi ya makamu. --- wordings zimekaa kitaarifa zaidi na sio kwamba kapeleka ombi.

ila taarifa ya ikulu inasema rais karidhia ombi la kujiuzulu
 
Msikilize Sinde Warioba aliyeongea naye kuhusu kujiuzuru
Wariaoba alizungumza naye Kwa Njia ya Simu, na baadaye Warioba alipopata Taarifa ya kufukuzwa Uanachama akawa anampigia Simu na hazikupokelewa.. Huenda Warioba alizungumza na Nchimbi mwenyewe mwanzoni, Huenda pia hata hiyo Mwanzoni alizungumza na Mtu mwingine bila kung'amua...
 
Msingi wa cheo chake ni kuchaguliwa, kama Mbunge na Raisi, ambapo taarifa zao zinaenda Kwa Spika, je Makamu wa Raisi hayupo katika kundi Hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…