Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

NGOJA MIMI NITOE YANGU

Nakumbuka wakt namaliza chuo 2010 nilipigika sana..Nilipitia sana mateso na dharau za kila namna kutoka kwa majirani zangu(esp wazee)

Bahati nzuri nilikuwa na sehemu ya kujihifadh kwa hyo sikuwa na hofu ya kulipa kodi wala nn

Nakumbuka ilibidi nitumie hela niliyobaki nayo(masalio ya boom) kutengeneza mkokoteni wenye uwezo wa kubeba madumu 10

So nikawa nanunua maji dumu sh 100..naenda kuuza maeneo ya mbali na pale nilipo(kama kilomita 8 hv) kwa shilingi 400-500

Hii kazi ilikuwa ngumu sana ila nikawa napata kafaida kazuri tu ka kuweza ku-sustain mahitaji ya hapa na pale

Sasa pata picha hii kazi unaifanyia mtaani kwako na watu wote mtaani wanajua umemaliza chuo alafu unasukuma mkokoteni wa maji...aisee nilipata tabu sana...dharau zilikuwa nyingi sana ila ambayo sintaisahau ni ya demu mmoja kunitolea shombo kali sana baada ya KUMTOKEA..alinipa SHIT ambazo zilinifanya NIUMIE sana

Nashukuru baada ya kama miaka 2 hv tangia nimalize chuo nilipata chance flan hv ambayo imenifanya kdg niwe mtu katika watu na yule manzi alienidharau alianza kuniletea SHOBO zake siku nimerudi mtaani na USAFIRI mmoja wa maana..yeye alizalishwa huko na janaume moja likakataa mimba sa hv yupo tu nyumbani hana inshu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole mkuu,
watu wanakosea sana kumkataa mtu kwa sababu ya khali yake kiuchumi wakati uo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina kazi ila mshahara [emoji17]mdogo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
nisha fanya biashara ba mchizi aka lala na hela yote mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JINSI NILIVYO INGIA KWENYE KUSAFIRISHA MIRUNGI BILA KUJUA

Msi mind mwandiko

Ilikuwa kipindi niko kitaa tu sina hili wala lile nilikuwa mtu wa mishe za town hasa katika maswala ya kuchukua order za kuku kwenye ma super market naenda kutafuta wale wazito kwa bei ya 6000 nakuja kuuza kwa 6500. Kwa week nilikuwa niko poa tu.

Sasa majanga ni pale siku manager alikuja kujua deal kamili kuhusu upigaji wangu kibarua kikaota nyasii.

Nikaa anza kusota mtaani na kuangalia njia nyingine, kama unavyo jua vijana kipindi hicho nilikuwa ni mtu wa kujichanganya kiasi sio sana so nikawa ni mtu wa tungi sana na kila siku zinavyo zidi kwenda ndo kabisaa nazidi kuwa pierre, sasa kuna jamaa alikuwa akija sehemu ninapo kula tungi huwa hakai sana akija na demu wake ni dakika mbili wanaagiza nyagi wana ongea anaingia cha fasta gesti na wanaacha tungi mezani wanasepa zako. Nilikuwa nawaona mara kwa mara nikienda pale.

Siku nimekaa sina hili wala lile niko na glass yangu nimetulia na ki nokia torch changu naona jamaa kaingia na aka kaa akawa kama ana msubiri demu wake akanipa hii tukasalimia fresh.
Mara akaanza kutoa lawama pale kuhusu mademu kuchelewa na amemuambia tokea kitambo sana kuwa aje nikachangia mada kiasi nikaona kasogea tuka piga story.

konyagi ndogo yake ikawa imeisha akaagiza akanichukulia na mimi safari na jogoo 2 fresh.
Basi jamaa akaniuliza ishugani nafanya nikamwambia sina mishe basi akaniambia kwa mwonekano wako mzee unafaa kabisa kuungana na mimi nikamtania kumwambia nini kuuza bangi au akasema hapana akadai kuwa anasafirisha mizigo kutoka boda mpaka arusha na huwa hailipiwi kodi so ni kama magendo hivi akadaii atakuwa ananipa nauli pamoja na deliver salary.
Nikasema hii deal basi nikampa number pale nikawa na sikilizia.

Siku napigiwa akaniambia dogo vaa vizurii kuna ishu unapelekea leo naona mzigo ni mwingi sana. Basi nafika akanichukua na gari tukaenda maeneo flani ndanii hukoo kuna nyumba ina fensi safi tukaingi na kulikuwa hapaishi mtu wakati nyumba ni kubwa tu.

Wakanipa beg nikasikia harufu ya mirungi mzee niliogopa sema nikajikaza wakanipa moyo wakadai wewe kazi yako ni kupeleka na kufikisha basi. so acha wasi wasi.

Wakafunga wao waka pack kwenye gari lao aisee kwa staili ile hakuna mtu anaweza jua.
Wakasema ni pande mabasi makubwa ya kutoka x kwenda x ndo salama nikapanda na hapo nyuma walinipiga unyunyu mkali sana ili ninukie kuepusha harufu ya mirungi asikwambie mtu ilikuwa natetemeka balaa mtu akiniangalia tu nahisi amenishtukia gari ikisimama najua ni mimi yani nilikuwa sina amani kabisa.

Thank god nikafika eneo lenyewe nikashuka nikapiga simu nikaa ambiwa kuwa ni subiri kumbe bwana wanakaa mahali wanakuangalia kwanza kisha wanakupigia simu kama mara 2 au 3 ndo wanakuja.

jamaa kafika pale akanipokea kisha nikamfata kwa nyuma tukawa tunaenda kama tuna panda gari stend njiani akanipa buku 15 akaniambia kuwa wewe sepa tusha malizana.

Dhaaa aisee niliona nimetua mzigo nikafanya kama mara 8 hivi wakanitema maana nilikuwa najiamini kuliko wao.
Na kuna mmoja alidakwa faini yake ni zaidi ya milioni 8 na kama boss wako masikini basii jua ndo tuna kusahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Noma sana
 
Mkuu Gairo chaka gani ulikuwa unachukua maharage
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haso la maana
 
Pole sana mkuu,yani ulivyomtaja tu huyo jamaa apo nikajua tu lazima aliwaliza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…