Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Haha wabongo bhana wasipokuelewa tu unapewa jina USALAMA,wakati nipo advance kuna mwamba alikuja kusoma akiwa umri umesogea kidogo na akawa mkimya sana,watu wakawa wanatangaza eti jamaa usalama hadi walimu wakawa wanamuheshim.
 
Mafanikio yanaleta heshima,tuzidi kupambana sana mkuu,mwanaume sifa yake kazi na kutokata tamaa.
 
Mkuu Gairo chaka gani ulikuwa unachukua maharage

Sent using Jamii Forums mobile app

Rubeho pana solo kubwa la maharage ila kutokana na kulima huko yanapotokea mwanzoni nilianza kwa kuyatoa huko ndani ndani napeleka rubeho nauza kwa ndoo ila baadae nikawa napeleka town kbs nauza kwa kupima kg na hapa ukiwa umeyachukulia huko ndani faida take utaiona vzr sana yaan super normal
 
Asante Mkuu

Kwa hiyo yapo mengi, yaani mtu unaweza kuchukua mzigo mkubwa hata wa kuhifadhi store?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mwaka nilipigika sana, nikawa naenda mitaa ya uhindini (Mbeya) kwa Bojan, Tanesco,kwa George town Mbeya Retco mpaka maeneo ya TRA (mitaa ya PAMODZ) pale nasubiri watu wakipaki magari naanza kufuta vioo, kuna waliokuwa wananitoa, wengine walikuwa wananikazia na maneno ya kejeli juu. Kuna siku nipo mitaa ya Bojan pale nasugua tyre mwalimu wangu (Mwasalanga) aliyenifundisha Accountancy advance akapita akaniona nilifedheheka sana.
 
Mkuu Rubeho msimu wa maharage huwa ni mwezi wa ngapi mpk wa ngapi? Vipi bei yake huwa inakuaje ?
Pole kwa kupigwa na upepo wa drop shipping.
 
Miaka kadhaa iliyopita baada ya kumaliza masomo; nikiwa nimepigika; yaani naishi kwa bro; kula kulala; mwishowe nikachoka kulelewa, nikakosa uvumilivu na kuondoka Dar na kwenda Mwanza; nikajisemea sitaenda home wala kwa ndugu; nikaishi kwa rafiki yangu, ikawa inafika kipindi hata chakula tu kukipata inakuwa shida. Siku moja nikajisemea basi nikatafute hata kibarua cha kufua nguo kwa wenye maisha bora pale Isamilo. Ila sikufanikiwa kupata.

Leo hii nipo Ulaya nchi mojawapo hapa Scandinavia; angalau napata chochote kukidhi maisha na kubakisha saving kidogo. Huko nyuma sikuwahi kuwa na saving, yaani pesa inaisha kabla hujaipokea mikononi. Nimejifunza katika maisha ukimtegemea Mungu na kuwa na juhudi; then shida zilizopo huwa ni suala la muda mfupi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujatuambia jinsi ilivyohustle mpaka ulaya!
 
Hujatuambia jinsi ilivyohustle mpaka ulaya!
Ulaya nilifika kwa njia za masomo, bado nipo masomoni naendelea. Sikuja kwa njia za kuzamia. Nadhani hii itakuwa ni njia ya kujinasua kutoka kwenye dimbwi la dhiki na karaha kwa kutumia fursa vizuri na kuangalia ni njia gani ya kuendea na namna gani ya kufika mahala fgulani, though mpanga rizki ni Mungu, ambaye hujua nani atakuwaje na lini, lakini naamini kuwa Mungu humpangia mambo mema kiumbe wake na wala siyo shida.!
 
Kongole kwa Mjomba. Tunawashukuru wajomba wote wanaowapenda wapwa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetaja mitaa yangu hiyo mkuu,alienilea alikua humo ndani TRA kwa miaka kama 7 hivi namimi pia niliwahi piga fild apo pia mwaka 2016
 
Ni kweli mkuu katika mambo yote lazima Kumtegemea Mungu.Hongera kwa kuwa majuu mkuu
 
Aloo una ujasiri sio wa kawaida, naskia Congo imejaa misitu hatari.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aise umenikumbusha kiwanda cha mo dewj nilibebeshwa cement, mbolea mafuta vindoo vidogo mnabeba vinne kwa pamoja kushoto 2 kulia 2 kazi ilinishinda sku ya kwanza tu nikadanganya dam zinatok puan ela skupewa nikarud hom sku ya pili mgongo unauma balaha sikurud tena aya maisha oneni tu
 
Pare oyeee🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…