Just for your records, Bagamoyo port project negotiations was called off, hata sasa wanajaribu kuwaita tena China Harbours wake waendelee majadiliano but it's far too late.
I know kwamba China Merchant wameshakamata Berth nadhani sita hapo Lamu kwa ajili ya shughuli zao tu. Unajua Berth sita pekee ni karibu robo tatu na zaidi ya Dar Port pekee, hapo bado hizo Berth nyingine.
Hii project ilisimama Ila kwansasa imeanza kick off, tusijioe moyo. Ninaujua mradi wa Bagamoyo vizuri sana aisee sana tu. Kama China Merchant wakikubali kuendelea negotiations wallah hapa sasa ndio tutapigwa maana watahakikisha wanatubana haswa tofauti na mwanzo maana tumeonyesha njaa tayari.
Mind you, wawekezaji wakubwa wa bandari kwa dunia ya sasa ni wachina sababu ya teknolojia na wingi wa biashara na bidhaa nchini kwao so wanajenga bandari sababu Wana uhakika mzigo upo wa kutosha kutoka kwao so turn over hawatapata shida.
I know the project usiniukize nafanya kazi wapi.
Mkuu, mbona unajichanganya mwenyewe hapa!
Unasema "...it's far too late" kwa majadiliano na China Harbor; halafu hapo katikati unasema tena "...kama China Merchant wakikubali kuendelea negotiations...".
Unaweza kuwa unaujua mradi wa Bagamoyo, lakini hiyo haitoi ukweli kwamba Bagamoyo kwa njia moja au nyingine itajengwa tu, na sio lazima ijengwe na wachina. Hii ni bandari yetu, tutaamua kuijenga kwa manufaa yetu.
Nikuhakikishie kitu kingine, Lamu haiwezi kamwe kushindana na Bagamoyo itakapojengwa. Hapo ilipokaa Bagamoyo haiwezi kamwe kuogopa ushindani na bandari yoyote ile kufanya biashara zake.
Usipende sana kusikiliza kelele nyingi wanazopiga huko majirani zetu hawa kila wanapopata kimradi na kukikuza kuliko ilivyo halisia yake.
Lamu ina matatizo mengi sana pamoja na kwamba inacho kina kizuri cha kumudu meli kubwa. Hapo ilipo hapaipi mvuto kama ilionao Bagamoyo. Mfanya biashara yeyote anatafuta sehemu yenye unafuu wa kufanyia biashara yake, havutwi na kelele nyingi za kujiuza hata bila kuwa na sifa stahiki.
SAWA, mchina kwa sasa ndiye mwenye mvuto, hasa katika kazi hizi za ujenzi wa miundombinu, lakini sio peke yake anayeweza kazi. Kama hatukubaliani naye, si tutatafuta wengine?
Lakini la muhimu ni hili moja, kwamba Bagamoyo itajengwa, na si lazima tujisalimishe kwa mchina ndipo iweze kujengwa.
Teknologia anayotumia mchina siyo mpya wala 'unique', sasa sijui wasiwasi wako unatoka wapi.