Wakenya Tupeni Uzoefu Wenu Kuhusu Passport

Uongo sasa hivi watu wanajisomesha wenyewe hawasomeshwi na serikali

Wanakopa mikopo bodi ya mikopo,kwenye mabenki nk kujisomesha vyuoni ambayo watailipa wenyewe sio kuwa watalipiwa na serikali

Hiyo 90.% yako uongo mkubwa
Mfano mzuri ni Tanzania hakuna hiyo kitu ya uongo.wako watu wanajisomesha
 
So wasomi wote wameajiriwa hapa? Pili notion ya kwamba watu wanasomeshwa na serikali mnaioata wapi?
Serikali ya Tanzania kwa sasa haisomeshi.watu vyuoni wanajidomesha kwa mikopo ambayo watailipa

Huyo atakuwa ni wale vikongwe waliodoma enzi za Nyerere bure na ndio kikwazo kikubwa cha kuzuia watanzania kupata passport kirahisi

Wana mawazo mgando sana na wagumu kubadilika .Kola kitu ukisema utasikia kijana kaa mbali sisi tuna uzoefu toka enzi za Nyerere passport tunatoa tu mtu akiwa na safari .Untaniambia nini wewe.? Miaka yote tunafanya hivi hivi. waliosoma bure enzi Nyerere hata hawajui hata nchi tu inaendaje kuwa kwa sasa elimu vyuoni serikali haisomeshi bure tena ni wajibu wa mwanafunzi mwenyewe na mzazi au.mlezi watafute pesa za kusomea iwe kukopa au kokote
 
Nchi changa ni ipi? Labda South Sudan. Lakini zingine kama Tanzania, haziwezi kuwa changa. Nchi yenye umri wa miaka 62 haiwezi kuwa changa. Ni Rika moja na South Korea.

Vijana wataenda kufanya uhalifu nje? Kwani hizo nchi hazina vyombo vya usalama kiasi kwamba Tanzania inapaswa kuzilinda dhidi ya uhalifu? Kwa kuwa Tanzania ina vyombo makini vya dola, iwabaini wale wote wenye tabia za uhalifu ili isiwape passport. Wengine wote watakaosalia, wapewe, maadam tu wanahitaji.

Kama Serikali haikuwa makini wakati wa kutoa vitambulisho vya NIDA, basi ni rahisi hilo la raia wa nje KUPEWA passport ya Tanzania. Lakini kama zoezi lilienda vizuri, basi hilo haliwezi kutokea kwa sababu vitambulisho vya NIDA vilibainisha na uraia.

Kuhusu idadi ya wanaohitaji passport, ni kubwa sana kuliko unavyofikiri.
 
Mkuu, unaishangaza dunia kwa huo mtazamo. Ni North Korea pekee ndiyo inaweza ikakubaliana na mtazamo wako, kwa kuwa haipendi raia wake wajue jinsi Dunia inavyoenda. Kule watu "wanafugwa" na "kutumikishwa" kwa maslahi ya watawala.
 
Mkuu, inaelekea hata Kenya bado hujafika. Hakuko hivyo kama unavyofikiri. Ina wasomi wa kutosha na ziada, ndiyo maana Serikali yake inafanya jitihada kuwatafutia raia wake kazi katika mataifa mengine.
 
Nimekubali sera ya ujamaa na ukomunisti hupofusha fikra.
 
Nashangaa these guys wanasema tz unapaswa ku apply ukiwa unataka kusafiri
Sio kutaka kusafiri tu uonyeshe vithibitisho kama kweli unataka kusafiri among them barua ya mwaliko. Kinyume na hapo utumie madalali uhonge.
 
Ndio sababu Kenya is ranked poorly on security, Globally Tanzania is ranked position 54, while Kenya 125.
Kenya imekuwa ranked poorly kwa sababu inapakana na Somalia,
Somalia kila siku ni vita na mashambulizi ya al shabaab
 
Serikali haisomeshi, bali inatoa mikopo tena kwa baadhi tu.

Kuna wengine, wengi tu, walisoma kwa kujilipia au kulipiwa na wazazi au walezi wao.
 
Mkuu, inaelekea hata Kenya bado hujafika. Hakuko hivyo kama unavyofikiri. Ina wasomi wa kutosha na ziada, ndiyo maana Serikali yake inafanya jitihada kuwatafutia raia wake kazi katika mataifa mengine.
Sahihi serikali ya Kenya karibuni imeingia makubaliono na serikali ya ujerumani kupeleka wafanyakazi wakenya 250,000 kwenda ujerumani kujaza nafasi mbalimbali zilizo wazi ujerumani na wamekubakiana mafunzo ya lugha ya kijerumani yaanze Kenya ili kuwaanda watakaoenda kufanya kazi

According to President William Ruto of Kenya, an agreement between Kenya and Germany is in the works and may see Berlin welcome Kenyans to fill some of the 250,000 unfilled positions to help the European country's enormous labor need.
Chancellor Olaf Scholz of Germany and President Ruto of Kenya relayed the information during a joint news conference from the State House in Nairobi.
According to the deal, the European nation would take in more professionals, skilled workers, and semi-skilled Kenyans. Nairobi wants Berlin to reconsider and relax immigration restrictions so that Kenyans can work in Germany in order to make this possible.

Source: Media za Kenya
 
Serikali ya watu wanaojitambua.
 
Kama umesoma, katika harakati zako zote za kusoma kwako hadi level uliyofika, KUNA PAHALA ULIKUBALIANA NA SERIKALI KWAMBA UTAKUJA KUFANYA KAZI SERIKALINI BAADA YA KUSOMA KWA KODI ZINAZOKUSANYWA NA SERIKALI? Haya, serikali imekaa miaka mingapi haijaajiri mtu, wale wahitimu wafanyeje? Kuna wakati tuwe waharisia tuachane na nadharia..!!

BTW, siku hizi elimu kwa mkopo ambao unakuja kuulipa baadaye...!!!

Kuna makampuni, wakikupeleka baadhi ya training, hasa zenye gharama kubwa, unasaini mkataba kuwa ukitoka huko utafanya kazi kwao kwa kipindi fulani, say mika mitatu..!! Ukimwacha mtu huru ujuzi uliompa anaweza akaenda kuutumia kwingine...!!

Turudi huko kwenye serikali. Kama serikali ingekuwa inaajiri kila aliyesoma kwa kodi za serikali, kungekuwa na wasomi mitaani wasio na ajira?

Kukujibu swali lako na huyo msichan kuolewa na mtu mwingine, TATIZO LIPO KWAKO WEWE ULIYEMSOMESHA. UMEWEKEZA BILA KUJIHADHARI. HIVI UNADHANI KWANINI HATA MAKAZINI TUNA MIKATABA? KWANINI HATA KUTOA HELA YAKO ULIYOIWEKA BENKI LAZIMA UWEKE SAHIHI? HUKO KUTOCHUKUA TAHADHARI MAPEMA NDO HUPELEKEA WATU KUUWA..!!
 
Unazungumzia wasomi majobless? Yaani mtu amalize chuo leo, halafu amsubiri mwekezaji miaka minne bila ajira..!!!
YOU NEED TO CHANGE YOUR THINKING KWENYE JAMBO HILI..!!
 
Mkuu, nchi hii Kuna watu wengi wazuri wenye hekima, elimu na busara nyingi ukiwemo wewe...
Kumbe unafahamu hilo. Inawezekana na wewe uko kwenye system. Kama kuna mahali mmekwama, mseme msaidiwe. Kuna Watanzania wengi wenye mawazo mbadala na wako tayari kuyatoa bure, bila kudai malipo yo yote.
 
Unafahamu kuwa Tanzania kuna maelfu ya watu ambao tokea wahitimu Vyuo zaidi ya miaka kumi iliyopita, hawajapata ajira mpaka sasa?

Unafurahia unapowaona wakitembea na bashasha za khaki huku viatu vimeisha soli kwa kusaka ajira?
 
Unafahamu kuwa Tanzania kuna maelfu ya watu ambao tokea wahitimu Vyuo zaidi ya miaka kumi iliyopita, hawajapata ajira mpaka sasa?

Unafurahia unapowaona wakitembea na bashasha za khaki huku viatu vimeisha soli kwa kusaka ajira?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…