Wakenya Tupeni Uzoefu Wenu Kuhusu Passport

Sasa tutajuaje dhumuni la safari yako Kama hatutodhibiti katika kutoa "exit visas?, Kumbuka Passport ndiyo "exit visa". Kama tunadhibit "Entry visa", kwanini hutaki tudhibiti "exit visa?", Unachekesha Sana.
 
MTanzania anaishi Karatu na Ngorongoro iko 14kilometer kutoka hapo lakini hajawahi kufikia

MTanzania hapakui Kenya, Rwanda, Burundi n. k (East Africa)

MTanzania anaishi Dar es Salaam miaka 10 hajafika kwao Sumve Misungwi(Mwanza)

MTanzania hana uelewa wa biashara kati ya nchi na nchi karibu wananchi kwa 90% na hata mitaji ya kufanya hivyo, hata kwa waKenya au baadhi ya nchi za kiAfrica wanafanya kama sehemu ya haki tu kwa watu lakini hawana safari zozote kati ya nchi na nchi

Nchi yoyote Duniani, watu wanao safiri sana ni wafanya biashara na watumishi wa maofini hasa ofisi za mashirika ya kimataifa, nao ni wale wenye ngazi za juu.
 
Unafahamu kuwa Tanzania kuna maelfu ya watu ambao tokea wahitimu Vyuo zaidi ya miaka kumi iliyopita, hawajapata ajira mpaka sasa?

Unafurahia unapowaona wakitembea na bashasha za khaki huku viatu vimeisha soli kwa kusaka ajira?
Ajira wapate wapi kwa maofisi gani? Chukulia chuo kimoja kati ya vilivyopo kwa mwaka vinatoa wasomi wangapi? Ni wengi[emoji3581] na ni kila mwaka, hizi ni nchi ndogo na masikini watatosha ktk ofisi zipi? Elimu imejaa misingi ya kigeni, misingi tegemezi... Yaani umezaliwa na kukua ukijua mafanikio yanategemea nguvu na juhudi zako halafu unataka tena mtu mwingine ndiyo akupe hayo mafanikio kutoka wapi? Jaribuni ku-think big
 
Nitajie hizo Serikali, ukiacha Tanzania, zinazodhibiti utoaji wa passport kwa raia wake kama unavyosema, kama hutaona kuwa hakutakuwepo hata na Serikali Moja ya watu wanaojitambua yenye ukiritimba wa hovyo kama huo.
Mkuu, toka uliko ujaribu kuzunguka Dunia ujifunze mambo, Passport sio kitu Cha mchezo duniani kote, Wacha kusikiliza maneno ya wakenya, wakenya ni watu waongo Sana, hata Kenya wanaidhiti Sana passport Yao, tatizo Kenya ni Rushwa iliyotamalaki, mifumo yote ya nchi inekufa, Kila kitu linafanyika kienyeji Kama Nigeria.
 
Rwanda je mbona nao hutoa passport kirahisi tu.kwa raia wao tenda ndani ya siku tatu tu

Mtoto tu akizaliwa ruksa.kupewa cheti cha kuzaliwa na passport.

Na kule Rushwa hakuna
 
You have stepped on the right point..!!
Nakunukuu..
Achaneni na mawazo ya kitumwa kwamba Kila aliyesoma lazima apate kazi ya kuajiriwa.
Sasa unapotaka msomi aajiriwe na serikali kwamba asiende huko "Botwana", ulimaanisha nini wakati hapa unasema tuache kuwaza kitumwa kwamba kila aliyesoma lazima apate kazi ya kuajiriwa?? Yaani ni kama umetoka nje ya topic uliyoianzisha.!!!
 
Kiongozi, una uhakika kwamba ninawashangaza watu? Are you serious?

No reference, no right to argue!!! Kwa nini kuandikia mate na wino ungaliko?

Itisha kura humu jukwaani kubaini kati yangu na wewe ni nani watu wanamshangaa.

Wataacha kushangaa na kuanza kukustaajabia!!!
 
Wacha kudanganya watu mkuu, inamaana pale "Freedom square" alipohutubia Mandela alipotoka kifungoni ambako Kuna kituo Cha vibasi vidogo(daladala), huwaoni wale watanzania walivyojazana, tena wanazungumza Kiswahili tupu?, wengi ni mateja na vibaka.

Nenda Durban useme wewe ni mtanzania, sifa yao kubwa ni kusubiri familia zimeenda kazini, wao kazi yao ni kuruka ukuta na kuiba, Durban kazi kubwa ya watanzania ni wizi wa kuvunja Nyumba za watu. Johannesburg ni kuuza dawa za Kulevya.

Sasa Kama Marekani Kuna huo upuuzi wa kijinga, ni haki na halali na sisi tuuruhusu tusifanye jitahada za kuzuia, mbona USA wameruhusu ushoga lakini sisi tunaukataa kwa nguvu zote?
 
Ukisoma kwa mkopo wa serikali ndio kusomeshwa na serikali, hivi serikali ikiacha kutoa mikopo Kuna mtu ataweza kwenda kupata mikopo Bank na kujisomesha?. Kwa hapa Tanzania 98% husomeshwa na serikali kwa kupitia mikopo.
Ukilipa huo mkopo, unakuwa bado umesomeshwa na serikali? AU tuseme, akina marehemu Samwel SItta AU ndugu Pius Msekwa ambao walisoma bila kukopeshwa, na wewe ambaye umesoma na ukallipa deni, nani amesomeshwa na serikali? Wote tuliosoma after 1994 (kama sijakosea mwaka) tulisoma kwa mikopo, kabla ya hapo serikali ililipa na haikuwa inarudishiwa. Sasa wa 1993 kurudi nyuma na wa 1994 kwenda mbele unasemaje wote wamesomeshwa na serikali wakati mwingine halipi na mwingine analipa..?? Hivi anayekopa unga, mchele, sukari etc, kwa Mangi au Muha na akalipa deni, huyo mkopaji familia yake inakuwa imelishwa na mangi au huyo muha?

Mwamba unajitahidi sana kutetea uongo wako..!!
 
ILa unajitahidi..!! 😂 😂 😂 😂
 
Serikali inatoa wapi hela kama siyo kwa wananchi wake? Serikali kuwadumia raia wake si fadhila, ni wajibu. Pesa iliyopo Serikalini ni ya wananchi.
Na raia kutumikia nchi yake sio fadhila ni wajibu, kumbuka maneno ya rais wa zamani wa Marekani J.F. Kennedy:

"Usiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe imeifanyia nini Marekani?"
 
Unafaa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje au wa Mambo ya Ndani!!!
 
Mbona Ethiopia haina tatizo la kiusalama Kama Kenya wakati imepakana na Somalia Kama Kenya?, Wacheni kutetea "failed states Kama Kenya.

Hivi mkuu, ukiwa na jirani yako anafuga mbuzi na anaziachia kwenda kuharibu mazao kwenye shamba lako, wewe utamchukuliaje huyo jirani yako?. Kuweni wakweli punguzeni ushabiki.
 
Na raia kuidimia serikali sio fadhila ni wajibu, kumbuka maneno ya maneno ya rais wa zamani wa Marekani J.F. Kennedy:

"Usiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe imeifanyia nini Marekani?"
Raia analipa kodi, ndo kikubwa nachoifanyia serikali..!!! Mengine ni vitu kama kutokuwa visadi, mwizi wa mali za ume etc
 
Raia analipa kodi, ndo kikubwa nachoifanyia serikali..!!! Mengine ni vitu kama kutokuwa visadi, mwizi wa mali za ume etc
Sasa hiyo Kodi itapatikanaje Kama watu wenye elimu kubwa waliyoipata kwa pesa za wavuja jasho wanaamua kwenda kufanya kazi nchi zingine?, nani abaki nchini Ili kuwatibu hao walipa Kodi Kama madaktari wataamua kwenda kufanya kazi katika nchi tajiri?
 
Unasema uongo kwa manufaa ya nani?
 
Acha uongo passport ni haki yako regardless what?,mtaendelea kuburuzwa na royal families kwa generations zote hapa ni push back tu
Kama huna safari achana nayo usije ukaipoteza bure ukauponza
 
Taifa gani halina wezi ughaibuni?
 
Mbona Ethiopia haina tatizo la kiusalama Kama Kenya wakati imepakana na Somalia Kama Kenya?, Wacheni kutetea "failed states Kama Kenya.
Unachoongea unakijua ? Ethiopia kuna.usalama? Wanatwangana mabomu.na mavifaru na wapigamaji wa Tiigray daily.

Pili tatizo la Ethiopia na Tanzania kwenye ugumu wa kutoa passport wanafanana
Ndio maana Tanzania kutwa tunakamata wa Ethiopia kibao wanatoroka kupitia njia za hatari kutafuta maisha nje ya.nchi hasa South Afrika

Sisi kutwa tunawadaka kwa kuingia nchini bila passport hivyo kuhesabika wameingia kiharamu wakati wao hapa wanapita tu .
 
Mkuu, soma alama za nyakati, jaribu kupima kina kabla ya kuvuka mto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…