Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Jamaa amedhihirisha anajua kazi yake
 
Mungu wetu yu mwema, jana, leo, kesho, na hata milele. Kupitia kwa Mawakili wa upande wa utetezi tunauona utukufu wake
 
Kuna suluhisho zaidi ya kuweka mawakili mahakamani ili kuhakikisha kesi inaendeshwa kwa haki? Hii njia yako nyingine ni ipi? Alafu unaposema wanafurahia, kwani hawa wana Jf ndio waliomfunga Mbowe. Busara nzuri na kama kweli unamuonea Mbowe huruma, ongea na waliomtubumu waondoe kesi mahakamani.
 
N
Ukiona shahidi anahojiwa hadi anapata homa mahakamani ujue hapo hamna kesi!
Na likely, anadanganya.

Kila shahidi ana haki ya kuaminiwa, ila kuaminiwa kunapunguzwa na hali zao kisaikolojia mfano kusahau alichokisema awali, na kikubwa zaidi kushindwa kusimamia kwenye point ya msingi yaani kujichanganya. Kuumwa kichwa n.k
 
Kiukweli huyu jamaa anasababisha nijiulize kwanini sikusomaga Law yani dah! lakini basi ntaendelea kumuelewaga sana tu, PK yuko vizuri zaidi ya kawaida na sana
 
Wote tunajua kwamba wakitaka kumfunga kivyovyote vile watamfunga bila kujali mmeweka utitiri wa mawakili, hayo ndio mazingira halisi tuliyonayo na hakuna asiyejua ila tizama ni nini sasa kinaendelea? Jibu ni kwamba ndio kwanza mnafurahia maswali ya Kibatala, Mbowe akifungwa mtakuja mtapiga kelele humu mwishowe litapita kama yalivyopita mengine kama ya akina Lissu na tutasubiri tukio lengine. Halafu mtu anauliza sasa tufanye nini? Utajua cha kufanya pale utakapochoshwa na yanayoendelea ila kwa sasa tuendelee tu kukoshwa na maswali ya Kibatala.
 
Mkuu we huburudishwi na maswali ya Kibatala? Utakuwa unakosa burudani, nashangaa Mbowe anakonda kule wakati huku watu huku wanaongeza siku za kuishi kwa furaha wanayopata kwenye maswali ya Kibatala. Hakika Kibatala anatoa burudani.
 
Ifike mahali waweke kigezo cha kuwa askari lazima kuwe kiwango cha elimu atlist Degree moja, sasa hawa darasa la saba wanatusumbua sana
Acha kudharahau darasa la 7, Mahita alisema ana Elimu gani? Jumanne na Kingai? Elimu na uongo vinaingilianaje?
 
Kwahiyo unashauri watu wafanyaje ili mbowe atoke?
Mbowe kutoka tu sio suluhisho la tatizo lilipo, yashatokea mengi na yataendelea kutokea mengine.
Sasa kama tunaona akitoka Mbowe kwa hayo maswali ya Kibatala ndio suluhisho basi sawa tuendelee kufurahia maswali ya Kibatala.
 
Hii ni nchi yetu sote,haijalishi una wadhifa gani muhimu wote ni waTanzania.

Nimekuwa nikifiatilia kesi ya ugaidi inayoendelea katika mahakama chini ya majaji watu katika nyakati tofauti tofauti na sababu mbali mbali.

Wakili Kibatala anastahili lawama,aina ya maswali ambayo amekuwa akiuliza mashahidi upande wa Serekali hayakustahi kuulizwa. Mashahidi wana familia,wana ndugu jamaa na marafiki kisa cha kuuliza maswali magumu,chokonozi na dadisi ni nini ?

Nashauri mamlaka husika ikiwezekana au hata kulazimisha goal za mkono Wakili Kibatala afutwe Uwakili.

Mashahidi wanaomba Ruksa za kujisaidia hovyo hovyo.Mashahidi wanakasirika bila utatatibu, mashahidi wanaugua magonjwa ambayo hata WHO hawayajui.

Naomba kuwasilisha.

Ngongo kwasasa Mwembekiuno.
 
Tena kama inawezekana mahakama itoe amri ili aww anawapa maswali yake kabla ili waandae majibu. Maana si kwa kujinyea kule. Yule bwana shahidi ndie alikuwa mtesi wa ndugu luteni na wenzake lakini leo kageuka kituko.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sheria zina udhaifu sana kwenye hilo swala wakili anaweza kuongea maneno makali na ya kuudhi na ikawa sawa tu.
 
Mawakili waserikali wamegundua polisi shahidi anazidi kupotea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…