Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

Wakili Kibatala anajua sana alifanyalo. Ni lazima akuchanganye tu

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Huyu bwana stahili yake ni kukuhoji kwa muda mrefu sana. Yaani kielelezo kimoja kinaweza kwake kikawa na maswali Zaidi ya 25. Ana utaratibu wa kuhoji mpaka kufikia muda wa kuhairisha ili siku inayofuata aje na nguvu mpya na mawazo mapya. Amekuwa sana na utaratibu huo ambao kwa kweli umekuwa ukiwachanganya sana mashahidi.

Shahidi wa leo Swila ambaye leo ilikuwa siku yake ya tatu kuhojiwa tayari ameshachoka sana kwani hakumbuki tena aliyoyaongea juzi wakati akihojiwa na mawakili wengine, leo amekuja tayari kishasahau kila kitu utafikiri hakufanya rehearsal, hii ni ajabu sana.

Baada ya kuona leo anazidi kulemewa ilibidi Wakili wa Serikali anayeongoza jopo lao amsogelee na kumwelekeza amwombe Jaji kuhairisha kwa ajili ya tatizo la kiafya - Shahidi mwenyewe inaonesha alikuwa ana uwezo wa kuendela lakini wakili wake kaamua kuingilia kati ili wakampe nafasi ya kujipanga upya kutokana na namna ambavyo ameshavurunga!

Kibata Mwenyezi Mungu azidi kukubariki sana. Hukumu ya Mahakama ikitofautiana na umma tunavyoona basi Jaji huyu atakuwa na roho ngumu sana.

Anyway Acha Ibaki Hivyo!
 
Ana upeo mkubwa sana, akikuuliza swali lake usipojibu anavyotaka atakuongezea part B,C, na D ndani ya muda mfupi bila shahidi kutegemea mpaka aingie kingi.

Huyu mtu ni mbaya sana kwa hawa jamaa zangu waliokaririshwa majibu ya kutoa mahakamani, kwa hali hii wataugua sana bora wakubali yaishe.
 
Ana upeo mkubwa sana, akikuuliza swali lake usipojibu anavyotaka atakuongezea part B,C, na D ndani ya muda mfupi bila shahidi kutegemea mpaka aingie kingi.

Huyu mtu ni mbaya sana kwa jamaa zangu waliokaririshwa majibu ya kutoa mahakamani, wataugua sana bora wakubali yaishe.
I wish I could be Kibatala!
 
Wameone aibu hawa askari wengi wamefoji hata vyeti
 
Ushahidi wa kujifunza dawa yake ndiyo hiii...ni lazima ujichanganye tu na ndiyo maana mawakili wa Serikali wanakuwa na objection nyingi kujaribu kuokoa mtiririko wa ushahidi mzima wa kesi usiharibike.

Ila washashindwa..hamna kesi humo, TZ hatuko serious, wastage of our nation resources sababu tu za kukomoana kisiasa.
 
Leo mpaka wameamua kutoa mpira uwanjani kwa kuweka kwapani
 
Kwani utaratibu wa kumhoji shahidi ni muda gani - nusu saa au saa moja? Kuna shahidi wa Jamhuri wakili wa serikali alimhoji kwa siku mbili na hukusema kama ni muda mfupi au mrefu.

Katika kutafuta haki na kwa nature ya mashtaka na ambapo kama pande zote mbili haziko makini - watuhumiwa wanaweza wakafungwa bila haki au wakasepa bila haki.

Ndiyo maana unaona mchuano huo wa kisheria. Lengo la upande wa mashtaka ni kuthibitisha bila shaka kwamba watuhumiwa walitenda makosa wanayotuhumiwa nayo. Upande wa utetezo una lengo kwa kuonyesha matobo yanayojitokeza kwenye ushahidi kisheria au kiuhalisi.

Pande zote hizi mbili zikiwa zina lengo la kumsaidia jaji anayeendesha kesi aone haki iende upande gani. Kama kufanya hivyo wewe unaona ni shida kwako, then hilo ni tatizo lako binfsi.

Kuna aphorism ya kisheria inasema "heri kuwaachia huru watuhumiwa 10 kuliko kumtia hatiani mtuhumiwa mmoja asiye na hatia." Na aphorism hii chanzo chake ni Kitabu cha Mwanzo (Genesis) 18:23–32.
 
Kwani utaratibu wa kumhoji shahidi ni muda gani - nusu saa au saa moja? Kuna shahidi wa Jamhuri wakili wa serikali alimhoji kwa siku mbili na hukusema kama ni muda mfupi au mrefu. Katika kutafuta haki na kwa nature ya mashtaka na ambapo kama pande zote mbili haziko makini - watuhumiwa wanaweza wakafungwa bila haki au wakasepa bila haki.....
Kama vile unanishambulia bila kunielewa! hebu nisome tena msomi wewe!
 
Huyu bwana stahili yake ni kukuhoji kwa muda mrefu sana. Yaani kielelezo kimoja kinaweza kwake kikawa na maswali Zaidi ya 25. Ana utaratibu wa kuhoji mpaka kufikia muda wa kuhairisha ili siku inayofuata aje na nguvu mpya na mawazo mapya. Amekuwa sana na utaratibu huo ambao kwa kweli umekuwa ukiwachanganya sana mashahidi.
Shahidi wa leo Swila ambaye leo ilikuwa siku yake ya tatu kuhojiwa tayari ameshachoka sana kwani hakumbuk tena aliyoyaongea juzi wkt akihojiwa na mawakili wengine. leo amekuja tayari kishasahau kila kitu utafikiri hakufanya rehearsal, hii ni ajabu sana.
Baada ya kuona leo anazidi kulemewa ilibidi Wakili wa Serikali anayeongoza jopo lao amsogelee na kumwelekeza amwombe Jaji kuhairisha kwa ajili ya tatizo la kiafya - Shahidi mwenyewe inaonesha alikuwa ana uwezo wa kuendela lakini wakili wake kaamua kuingilia kati ili wakampe nafasi ya kujipanga upya kutokana na namna ambavyo ameshavurunga!
Kibata Mwenyezi Mungu azidi kukubariki sana. Hukumu ya Mahakama ikitofautiana na umma tunavyoona basi Jaji huyu atakuwa na roho ngumu sana. Anyway Acha Ibaki Hivyo!
Sio shahili yake ni staili yake

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hii ni mbinu sahihi kabisa na imefanywa makusudi kwa sababu hizi;
1. Urio ndio alikuwa mtoa habari mkuu wa kesi nzima.
2. Mkaguzi Swila ndiye aliyekuwa mpelelezi wa kesi hii. Yeye ndio aliyefungua kesi, kupewa maelekezo na Kinga, kuomba vyombo vya uchunguzi kufanya kazi zake na hata kumhoji mtoa taarifa na hata kuandika maelezo ya Kingai.

Baada ya watu hawa, kesi itakwenda haraka sana ili utetezi nao ulete mashahidi wao. Ninahofia kuwa kutakuwa na mashahidi wa utetezi wengi waliohusishwa na Kaaya, Urio na kesi ya ugaidi kuliko Mbowe. Nina dhana kuwa uchunguzi dhidi ya makomandoo inatokana na zile mambo za Kibiti - Mbowe aliingizwa tu baada ya kuona amewasiliana na Urio ambaye alikuwa na kazi ya kuchoma makomandoo wote wasio kazini!!
 
Back
Top Bottom