Huyu bwana stahili yake ni kukuhoji kwa muda mrefu sana. Yaani kielelezo kimoja kinaweza kwake kikawa na maswali Zaidi ya 25. Ana utaratibu wa kuhoji mpaka kufikia muda wa kuhairisha ili siku inayofuata aje na nguvu mpya na mawazo mapya. Amekuwa sana na utaratibu huo ambao kwa kweli umekuwa ukiwachanganya sana mashahidi.
Shahidi wa leo Swila ambaye leo ilikuwa siku yake ya tatu kuhojiwa tayari ameshachoka sana kwani hakumbuki tena aliyoyaongea juzi wakati akihojiwa na mawakili wengine, leo amekuja tayari kishasahau kila kitu utafikiri hakufanya rehearsal, hii ni ajabu sana.
Baada ya kuona leo anazidi kulemewa ilibidi Wakili wa Serikali anayeongoza jopo lao amsogelee na kumwelekeza amwombe Jaji kuhairisha kwa ajili ya tatizo la kiafya - Shahidi mwenyewe inaonesha alikuwa ana uwezo wa kuendela lakini wakili wake kaamua kuingilia kati ili wakampe nafasi ya kujipanga upya kutokana na namna ambavyo ameshavurunga!
Kibata Mwenyezi Mungu azidi kukubariki sana. Hukumu ya Mahakama ikitofautiana na umma tunavyoona basi Jaji huyu atakuwa na roho ngumu sana.
Anyway Acha Ibaki Hivyo!