Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Leo Mei 3, Mawakili wanaomtetea mshtakiwa Tundu Lissu wanazungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari.
Kibatala: Intelijensia inayotumika kuthibiti maandamano ingetumika kuepusha kushambuliwa kwa Padre.Kitima na Mdude
Kibatala: Akizungumza na watanzania kupitia waandishi wa habari, amesema kwamba Mawakili wa Tundu Lissu wanaungana na wadau wengine kulaani, matukio mbalimbali ya uvunjifu wa haki ambayo yametokea hivi karibuni nchini.
Ambapo ametaja matukio hayo kwamba ni pamoja na kushambuliwa kwa Katibu wa TEC, Padre Kitima pamoja na kuchukuliwa kwa nguvu kwa Mdude.
Amesema kwamba wanalitaka Jeshi la Polisi lioneshe intelijensia yake na ufanisi ambao wamekuwa wakidai kuwa nao kwenye kuthibiti matukio mengine ikiwemo 'maandamano' au matukio ya Chadema, amesisitiza kwamba interijensia hiyo ingetumika kuthibiti matukio ya kushambuliwa kwa Kitima pamoja na
Mdude.
Kibatala
Amesema kwamba kumekuwepo na upotoshaji kuhusu mashtaka yanayokabili mteja wao Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi mbili ikiwemo ya uhaini.
Kibatala amesema wameamua kuzungumza na waandishi wa habari ili kuwaeleza watanzania uhalisia wa masuala mbalimbali kuhusu kesi hiyo.
Kibatala : Nani alibadili amri ya Mahakama? ghafla tukaambiwa Kesi ya Lissu itasikilizwa kwa Mtandao
Awali hatukukubaliana juu ya utaratibu wa Kesi ya Lissu kusikilizwa kwa njia ya Mtandao, lakini tulishangaa badae tunaambiwa utaratibu huo.
Amesema kwamba walishangazwa na jambo hilo kwa kuwa wao hawakushilikishwa mapema na hawakufikia makubaliano, kwa kuwa tarehe April 10 walikubaliana mtuhumiwa ataletwa mahakamani tarehe 24, April 2025.
Kibatala anadai kwamba April 23, 2025 ndipo walipata ujumbe kwamba Kesi hiyo itasikilizwa kwa Mtandao, jambo ambalo amesema wanahoji "Ni nani alibadili amri? na je ilikuwa sahihi"
Amesema kwamba kwa mujibu wa Sheria ilitakiwa washirikishwe suala hilo kwa taarifa siku saba kabla ili kufikia makubaliano ya pamoja.
Kibatala: Mawakili tulienda kuwasiliana na Lissu tukakalishwa masaa matatu nikaruhusiwa mimi lakini tulinyimwa haki ya faragha
Amesema kwamba Tundu Lissu amegoma kesi hiyo kusikilizwa kwa njia ya Mtandao kwa kuwa hajapata nafasi ya kutosha kuwasiliana na Mawakili wake.
Amesema kwamba baada ya kupelekwa kwenye Gereza la Ukonga, Mawakili wa Lissu walifika kumuona lakini walikutana na vizuizi, ambapo baada ya kukaa takribani matatu aliruhusiwa yeye ambaye alienda kukutana naye katika mazingira ambayo sio rafiki kuweza kufanya mawasiliano.
Anadai kwamba walinyimwa haki yao ya faragha kuwasiliana na mteja wake jambo ambalo liliwapelekea kuanza kutumia lugha ya kingereza.
Aidha amedai kwamba siku ya Ijumaa kuu mteja wao Lissu alikataliwa kwenda kushiriki Ibada huku washtakiwa wengine kwenye Gereza hilo wakiruhusiwa, lakini pia amesema kwamba hata siku ya Jumatatu ya Pasaka alikataliwa kwenda kusali.
Lissu kuanza kugomea kula chakula Gerezani
Tunaendelea kupigania haki za watanzania kwenda mahakamani kushiriki kesi ya Tundu Lissu (phiscally)
Lakini amesema anatoa taarifa rasmi kutoka kwa mteja wao kuwa Lissu amenatarajia kuanza rasmi kugomea kula chakula mpaka haki itakapotendeka.
Wakili Jebra Kambore : Waandishi wa habari wanapozuiwa Mahakamani kwenye Kesi ya Lissu, wananchi watapata taarifa wapi?
Amesema kwamba wanasikitishwa na matendo ya kukamatwa na kupigwa kwa Watu wanaofika mahakamani kufuatilia kesi ya Tundu Lissu.
Ametoa mfano, kwamba waandishi wa habari wanakamatwa na kupigwa jambo ambalo anadai kwamba linawanyima Wananchi haki ya taarifa.
Amesema vitendo vya kuwakamata, kuwafukuza, kuwapiga waandishi wa habari pamoja na kuwapangia vitu vya kuripoti wanapofika mahakamani kufuatilia kesi za Lissu vinawaweka wananchi katika mazingira wananchi kukosa taarifa za mwenendo wa kesi husika kwa kuwa wananchi wamekuwa wakivitegemea.