Nimekuwa nikijiuliza hili swali tangu nikiwa Sekondari na sijawahi kupata jibu.
Wakoloni walikuwa wanahusisha baadhi ya jamii kwenye elimu, Biashara, Uongozi, Kueneza Dini, Ulinzi, n.k. lakini inashangaza kuona wasukuma ambao ni kabila kubwa zaidi hawakuhusihwa, why ?
Ni kwamba nje ya kuwatumisha kwenye kazi za nguvu na kutumia viongozi wao kukusanya kodi hawakuwa na potential, mkoloni aliogopa wingi wao, au ni sababu ipi hasa ?
Hii ni baadhi ya mifano ya jamii zilizotumika na wakoloni
Wachaga walihusishwa kwenye Elimu, Dini, Utawala na biashara hasa kwenye cash crops.
Wahaya walihusishwa kwenye Dini na elimu kwa lengo la kumsaidia mkoloni kazi za ofisini *civil service
Wanyakyusa walihusishwa na elimu, kilimo na uenezaji wa dini hasa Moravian na Lutheran. Lakini kuanzia 1980s, makanisa ya kilokole yenye mizizi ya Zambia na Malawi yalienea zaidi.
Wakuria waliwekwa kuwa askari wa jeshi na vikosi vya usalama sababu ya ujasiri, discipline na miili
Wahehe na wangoni walitumika kama waajiriwa wa jeshi na walinzi wa kati, pia walihusishwa kwenye dini hasa Roma na Anglikana