Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Unahisi angekosekana ingekuwaje?.asingefanyiwa MRI?

 Hospitali kuna Medical attendants kazi hiyo wangeifanya fresh tu..kuvuliwanguo nayo ni ishu kubwa kweli??.
Haya ndiyo umejipeleka pale sijui na Uber au na driver wako upo kwenye foleni kusubiri vipimo ujisikie kwenda haja kubwa niambie hapa huyo medical attendant umeingia nae makubaliano saa ngapi akusafishe mavi?

Nasisitiza ni utoto tu ninyi actions za maisha hamjazijua na nijibu ni wangapi ktk nyie mnaweza kumlipa mtu 500K awafanyie huduma zenu za msingi?Kapuku wa Tanzania wanaiga maisha ya Elon Musk bilionea wa dunia wakati kula yao kwa siku inawapiga chenga,kueni kwanza acheni utoto.
 
Watu wanasema mtu asipooa akiugua ataona cha moto..yes kama mtu huyo ni hoehae.

Mtu mwenye hela utapata nursing service yoyote unayoihitaji.

Kwa wangapi hao wazee wa kibongo hawa hawa .wachache mno wengi hulelewa na watoto wao wakizeeka wengine huzunguka tu na kuzurura hovyo
 

Waambie hao kuwa na familia karibu na kuipanda tokea zaman ni muhimu,lakin et unazaa tu watoto huishi nao wanakuwa wanakuona wa kawaida tu ,wazee wengi ambao hawateseki ni wale walolea familia zao na wake zao pamoja hata wakiumwa hutunzwa,huyo nurse atakupa dawa tu na sio kuKusimiamia kama mkeo au mtoto
 
Mimi nachotaka watu waweke exception kwenye hili..kuwa sio kila ambaye ataacha kuoa atateseka.
 

Yaleyale ya kuamini kuwa mwanaume ndo atatangulia kufa nayaona kwenye hii comment yako.

Kuumwa uzeeni hakuwezi kuwa sababu firm ya kumfanya mwaname aoe, mara kuchambishwa, kuvuliqa nguo aiseeeh 😂.

Kwahiyo imeshajulikana moja kwa moja kuwa mwanaume ndiye atakuwa hajiwezi huko uzeeni?
 
Mkeo akifariki kabla yako nani atakuwa anakuchamba?
 
Kama utajaribu kufikiria kwa makini zaidi, utagundua kuwa:-

Kinachomsumbua huyo sio uzee ni kukosa fedha.
Hapo ndipo unajidanganya kudhani fedha ni kila kitu.Utakuwa na fedha.Sawa.Ila utakuwa in terms of purchases!Kwenye kununua lazima upigwe tu.Kwa nini usijiandalie upendo wako wa kudumu?Haya,endelea kutafuta wachukue kiulaini uanze kujiliza eti "golddigger" kakukomesha.😂😂😂😂
 

Mnaongea vitu utafikiri mtaan hamuyaoni
 
Bajeti ya kuchakata ni kubwa kwa sababu kila unayemchakata ana gharama zake na hakupi huo utamu bure kama kwenye ndoa unakula muda wowote ukihitaji. Kingine ni uwezokano wa kupata watoto wengi wenye mama tofauti. Labda bachela akae bila kuchakata wala kuwa na mpenzi maisha yake yote
 
Mimi nachotaka watu waweke exception kwenye hili..kuwa sio kila ambaye ataacha kuoa atateseka.
Mimi nakwambiaje!!!

Hilo kwa mazingira ya Tanzania haliwezekani na siyo Tanzania tu ila nchi yoyote maskini especially hizi za kwetu za kusagiana kunguni ndiyo hatari zaidi,kwanza elewa kitendo cha wewe kuwa na muda maalum wa kutoka na kuingia malaloni kwako (nyumbani) ni njia moja kubwa ya kujijenga kisaikolojia kwanza kujitunza afya yako ya mwili na akili.

Ukiwa huna control ktk hili (msela) hutaona umuhimu wa kupanga nyumba au kujenga maana unaweza kuingia ofisini na ukaenda kukesha bar nguo ukaacha kwa dobi maisha yakaenda tatizo utakapozeeka au kipato kuyumba kiota chako kitakuwa wapi?

Usije ukaona chizi wazee au wale wanaofia kwenye baraza za nyumba za watu ukadhani wamelogwa hao baadhi huwa walibonyeza skip button za baadhi ya mambo ya msingi kwenye maisha kama haya mnayokataa hapa ikawa janga kwao.
 
Watoto wadogo wana-discus maisha kimzaha mzaha dizain kama wapo kwenye vilabu vya pombe chafu hawajui maisha hayataki masihara.

Ni wadogo bado tuende nao taratibu wataelewa.
 
Mkuu nimesoma Maoni yako kwa kiasi kikubwa nimegundua uwezo wako wa kufikiri ni Mdogo sana. Jaribu Kujiboresha. Msome sana Saint. Augustin.
 
Unazidi ku-sound kitoto na toka huko juu nimekwambia wewe bado mtoto.

Ktk maisha wote tunabahatisha hakuna aneyejua atafikisha umri gani,ajali zipo maradhi yapo serikali yako kila siku inatoa tathmini magonjwa yasiyoambukizwa yameongezeka unasemaje hakuna kutojiweza ktk maisha?na siyo wanaume hata wanawake inawahusu
 
Mimi mwaka wa kuoa mje mnichinje ninayaona mengi sana Jirani yangu mpangaji mwenzangu amezalia mtoto nje ya ndoa anapata shida sana na mke wake Nachoshangaa jamaa yupo vizuri kiuchumi lakini bado pesa zake hazija msaidia kitu. Ningekuwa mm ningefukuza ile paka asubuhi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…