Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Unazidi ku-sound kitoto na toka huko juu nimekwambia wewe bado mtoto.

Ktk maisha wote tunabahatisha hakuna aneyejua atafikisha umri gani,ajali zipo maradhi yapo serikali yako kila siku inatoa tathmini magonjwa yasiyoambukizwa yameongezeka unasemaje hakuna kutojiweza ktk maisha?na siyo wanaume hata wanawake inawahusu

Shida ni kwamba unataka kusikia unachokiamini wewe ili nionekane sio mtoto.

Ila kuoa kwa kwa kigezo cha kwamba utasaidiwa uzeeni ni upumbavu na utoto wenyewe, unless kuwepo na sababu nyingine firm.

Yani nioe kwa kuugopa uzee? Mascular men hawawezi kuifanya hiyo kuwa sababu, labda SIMPS.
 
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuleta uzi hapa ni jinsi gani ndoa ni scam, ni jinsi gani ndoa iko pale kumnufaisha Mwanamke.

Siku za karibuni kumezuka matukio kadhaa ya mauaji ya wanandoa, au wanandoa kujiua sababu kubwa ikiwa mifarakano ya ndani ya ndoa.

Kwa Muktadha huo nazidi kushikilia ule msimamo wangu ya kwamba Maisha ya Mwanaume ili yawe Marefu kwa zama hizi aachana na hizi ndoa. Hutoua/Kuuawa/Kujiua.

Je wale wenzangu Lifetime Bachelors tupeane Mbinu zipi katika maisha yetu ya ubachela?

Uzi tayari!

cc: Liverpool VPN
Huyo Liverpool mbona ameoa, Au ndo hua anawadanganya
 
Hii ni sample ndogo sana kuweza ku-justfy issue ya ”umuhimu wa mwanaume kuowa au kutokuowa”.

Kuowa ni kama kutafuta kazi,utapata kazi ina mapungufu kadhaa mwengine anapata kazi inampenda kila siku anapanda vyeo so ni bahati ,siyo sababu kazi siyo nzuri tuseme tusifanye inabidi tu-face realty huo ndiyo uanaume hata baba yako kuishi na mama yako alitumia mbinu hizi hizi.
Hata sababu yako ni ndogo sana na haitoshi ku-justify ulazima wa mwanaume kuoa.

Kuuguzwa? Kwamba bila mwanamke siwezi kuuguzwa? Watakuelewa simps&cucks tu.
 
Mnaongea vitu utafikiri mtaan hamuyaoni

Sio kwamba hatuyaoni mtaani.

Wanaume wengi wanaokufa wakiwa na umri mdogo ni wale walioendekeza ndoa, na ndio maana wajane ni wengi mtaani. Yanu kwenye ndoa nyingi mwanaume hutangulia, sio burebure ni madhara ya kukumbatia ndoa.

Hilo tu linatosha kuonyesha kuwa hasara za kuoa ni nyingi kuliko zile za kutokuoa.
 
Pia mimi nina mfano

Kulikuwa na mgonjwa X kwenye hospital X hapa Tanzania, alikuwa ana 26yrs ameoa na anawatoto wawili.

Baada ya kuumwa sana, mke akawa anamuuliza kuwa nguvu za kiume anazo tena. Maana tatizo lake alihisi litakuwa limeathiri nguvu za kiume lakini si kweli.

Kilichofuata mke ni kumkimbia mume. Yule jamaa aliteseka sana , mwisho alifariki lakini kifo chake hakikutokana na ule ugonjwa alioupata bali ni hizo stress zilizotokana na mke wake.
Mimi mwenyewe na mshkaji wangu anaumwa hoi mguu unaoza mke kakimbia na watoto, jamaa alikuwa vizuri economically ila now anasaidiwa na wasamaria wema[emoji24][emoji24]
 
Wanataka kujiaminisha watazeeka ni matajiri wakati utajiri pia ni watu wa damu yako

Mwanaume mwenye uchumi mzuri hateseki uzeeni na wala hawezi kuwa mpweke uzeeni (kikubwa awe na watoto tu).

Ikiwa tu kwenye ujana wenu wengi hamna cha ku-offer kwenye mahusiano zaidi ya utelezi, huko uzeeni ambako mwanaume hahitaji sana utelezi mtakuwa na lipi la maana?

Msitake kujioa umuhimu msiokuwa nao kwa wanaume, NDOA ni mradi wa mwanamke na familia yake, na mara nyingi anaeteseka ni mwanaume mpaka atakapoingia kaburini.
 
Una miaka 60 labda hivi..utaoa pia na hapo tayari una wajukuu?..

Aibu gani hii?..ili tu upate wa kukuchamba..kudadadeki
Hahaha huyo hajui halafu hajui kama hajui, ndio maana anaandika upuuzi akiwa na confidence.

Mimi nimesema nitauona umuhimu wa ndoa kama ataleta sababu nyingine za msingi, si hizi za kutafuta mtu wa kuchambishwa nae.
 
Hahaha huyo hajui halafu hajui kama hajui, ndio maana anaandika upuuzi akiwa na confidence.

Mimi nimesema nitauona umuhimu wa ndoa kama ataleta sababu nyingine za msingi, si hizi za kutafuta mtu wa kuchambishwa nae.
Halafu tukipangua hoja anatuita watoto..

Tuletewe sababu za maana za kuoa..siyo hii ya kusaidiwa kuchambwa ukiwa mgonjwa.

Mapadri ambao hawaoi nani huwa anawafanyia haya wakizeeka?..
 
Wanasema kwa kizungu "LIVE YOUR LIFE" kwa hiyo sitakiwi kukushangaa wala kukupangia uishije mleta mada,
Ila ntazungumzia kwa mimi kwa maisha niliyopitia ya kuwa alone kulinganisha na sahivi nipo na wife na watoto.
Kwanza nilipokuwa single sikuwa najua hata lengo langu hasa kuzaliwa mwanaume ni nini yani pesa inakuwepo unakula, unalala unapotaka na kufanya upumbafu wote kama kijana lakini kuna kitu kilikuwa nakikosa kabisa nafsini, hata furaha unapopata inakuwa kwa muda mfupi tu kesho unarudia yale yale ya jana tena angalau ufurahi..
Baada ya muda sana nimejikuta tu nipo na huyu wife, yani ni process iliyokuwa automatic tu tayari tupo wote na tuna mtoto wa kwanza kipindi hicho, hapo sasa ndiyo nikaanza kujifunza na kuona maana halisi ya kuwa mwanaume kimajukumu na maamuzi ambayo niliyapitia na ninayapitia.
Sahivi napata amani na nguvu/motivation natafuta pesa zinatumika na watoto na wife watu ambao wakifurahi basi na mimi napata amani kubwa kuliko, automatically hata marafiki fake na mambo ya kujirusha ishakuwa history.
Inshort Ni mambo mengi nimejifunza na bado najifunza sahivi kwa kuwa na familia/KUOA NA KUZAA ila jambo kubwa zaidi NI KUACHANA NA ROHO YA UBINAFSI/U MIMI ambayo nadhani ndiyo tatizo kubwa la Vijana wengi kukataa kuoa na si jambo jingine.
 
Hapo ndipo unajidanganya kudhani fedha ni kila kitu.Utakuwa na fedha.Sawa.Ila utakuwa in terms of purchases!Kwenye kununua lazima upigwe tu.Kwa nini usijiandalie upendo wako wa kudumu?Haya,endelea kutafuta wachukue kiulaini uanze kujiliza eti "golddigger" kakukomesha.😂😂😂😂


Kwani mke hawezi kuwa gold digger? Nyinyi wanawake mnanini cha ku-offer kwenye ndoa zaidi ya utelezi huku mkitegemea kuwa provided kila kitu? Mnatofauti gani na magold digger?

Nimekataa na nitaendelea kukataa:-

Ukiwa na uchumi mzuri, kisha ukawa na watoto wako uliowajali vizuri, HAUWEZI kuteseka uzeeni kwa namna ambavyo mnajaribu kuyakuza mambo humu.

Uliona wapi mwenye uchumi mzuri akakosa watu wa kuwafuga kwenye familia yake? Huo upweke unatoka wapi?

Nyinyi wanawake hamna umuhimu huo mnaojaribu kujipa kwenye maisha ya wanaume, zaidi ya kuzaa watoto (ambao mwanaume anaweza kuwapata bila ndoa)
 
Yaani watu manajazana hofu uoga wasiwasi na mambo mengine mengi ambayo hayapo, kama mtu anaoa ili uzeeni apate wa kumchamba siyo sahihi kwa sababu hiyo ni pressure ya kutokujuwa yatakayotokea huko..Yaani wewe ukijikuta huku Duniani juwa tu upo katika mawindo, usipowinda wenzako watakuwinda, hofu ya nini?

Ishi jinsi unavyotaka sababu maisha ya binadam ni mafupi mno, sasa ukiendekeza maneno ya walimwengu utaishi kubahatisha maisha yako yote na hata siyo marefu, wakati uliotakiwa kuufurahia duniani uliutumia kuwaogopa watu wanatanisemaje nisipooa/sipoolewa,

Kila mmoja yuko safarini lakini safari hizo hazifanani hata kidogo.
 
Back
Top Bottom