Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

wanaume
Hili swala mume kufua na kupika naona ndiyo limekua kero kwa waume wengi!!

Waliolelewa familia za watoto wa kiume tu, nadhani hii siyo ishu sana. Lakini pia linaendana na tamaduni za makabila mbalimbali Mfano Wakurya, Wamasai (halisi) hawa ni ngumu sana kugusa kazi zinazoonekana za wanawake.

Tabu ni kwamba mambo yamebadilika!! Maswala ya kijinsia na majukumu yake yamekuwa ni maswala ya kiushindani na kubishana, mwisho wa siku hakuna tena maelewano na tunaishia kuachana!

Mmoja asipoona thamani ya mwingine katika familia, tabu huanzia hapo!! Kikubwa ni kila mmoja kuhakikisha thamani yake inaonekana pale anapoishi iwe ni mama wa nyumbani au mfanyakazi.

Kama wewe ni mvivu kAma mimi, nunua vifaa! Vacuum, dish washer na washing machine nA huku una rice cooker,deep frier ma pressure cooker umemaliza kazi za ndani 🤣🤣🤣🤣

Kuishi na watu ni kipaji!! Amini hili nawaambia!! Wengine tulioa wanawake wasiojua kupika wala kufua na watu wakazodoa mke gani mke gani lakini leo hii ndiyo mke bora kabisa na mama bora kwa familia na jamii inayotuzunguka.

Kwa sababu gani? Nilijua nataka ndoa ya aina gani, nikajua mke gani atanifaa, na nitampatia wapi! Na tangu mwanzo nilimjenga vile nataka kikubwa ni kwa heshima na kumpa thamani yake kama mke. Huwezi kuelekeza jambo mke kama unatoa order kwa wafanya usafi wa ofisini kwako.

Shida ni kwamba hata wewe unalea, je unamlea mwanao wa kike kuwa mke bora au kuja kuwa na maisha bora?? Unamfundisha kupika, kudeki na kufua? Unamfundisha kuheshimu mume? Au nawe ndiyo kama mie mtoto ana miaka mitatu ushampeleka boarding? Atayajua mambo ya familia lini?? Wapi? Unataraji atakuja kuwa mke bora?? Kwa nini uyabeze malezi ya mwenzio (malezi ya wakwezo)??

Kikubwa: Kuheshimiana na kupeana thamani kwa kila mmoja, kwa vile alivyo na kurekebishana. Kuchukulia mapungufu ya mwenzio as part of you.

Mwisho. Ndoa unai fold wewe unavyotaka iwe toka day one mnapokutana! Usitarajie mlikutana KFC mkafungia ndoa huko, miaka mitano ya mwanzo mnashindia take away za huko mwaka wa sita akuelewe ukimpa ugali ndondo!!

Haiwezekana, siku ya kwanza ya outing mpaka uchumba wenu mkeo akitaka kuchangia mnapokuwa na jambo unakataa kwa dharau halafu ghafla utake mishahara yake!! Utadai talaka tu, maana hawezi kukupa.

Akija kwako unafua na kudeki ye anacheki muvi ukimaliza unampanda viwili mnatoka outing! Then kesho keshokutwa unamuoa unataka akakupikie na kukufulia, umelogwa?

Narudia tena: Aina ya ndoa unayotaka unaijenga wewe mwenyewe toka day one, unapolazimisha ibadilike kwa nguvu baada ya miaka kadhaa ndipo mnavunja ndoa zenu.

NB: Chagua mke au mume unayeendana nae, usituletee tabu, ndoa tamu

wanaume hawajasoma hiii post.wanavyopenda kua budiwa na kutreat wenzao bila huruma
 
Wrong. Alpha males don't marry they sleep with many women because the attract alot of attention plus they don't and can't keep.

Simps do that ...... Simps settle down.
Ni kutokujua tu.......tabia nyingine Alpha males ni kuwa super-dominant halafu wanakuwa hawana hela na wanapenda kulelewa na wanawivu na wakorofi sana kama Uchebe wa Shishi
 
hahaha

nawaza hapa watoto wa corporate ladies wanakuja kuishi/kuolewa na watu wa aina gani? corparate men? 🤣😂
Corporate men wanaotoka wapi?

Kizazi hiki cha leo watakaokuja kuoa ni mafundi magari na seremala wengi tu! 😅

Unless otherwise hao watoto muwaachie urithi wa viwanda na biashara kubwa ila kama unategeme degree itamtoa mwanao 20 years to come utashangazwa😀!!!
 
But not all women do that.

Kuweka campain ya kuwafanya hawa wanawake wenye elimu zao na ndoa zao hawafai kuolewa ni kosa kubwa.

Ina impact kubwa sana katika maisha ya baadae. So mabinti wasisome, wasifanye kazi.... si tutarudi Stone Age na Bango la a woman's place is in the kitchen?
They rather be in kitchen atleast walikuwa na muda wa ku deal na watoto na family issues!
 
Hakuna mwanamke asiyependa kumdekeza mumewe apatapo nafasi, ila inategemea kwa mama mfanyakazi kama atapata muda jioni ni vizuri kupika na kumtengea mume ila ikitokea amechelewa kurudi labda , mume amuelewe na asicomplicate maisha kama dada yupo basi atasaidia kupika, ila mimi sitopenda dada amsevia mume wangu chakula ntajitahidi nimsevie mwenyewe ama ajisevie mwenyewe.

Ila on weekends kupika ni lazima mama mjengo nioneshe maujuzi jikoni harufu nzuri nyumba nzima hadi baba mjengo aseme leo kaingia mama mwenyewe jikoni rahaa.😀

Ila wanaume nyie mnadeka sana eti tuwatengee chakula, maji ya kuoga wakati mlivokua single mlikua mnasugua hadi sufuria na michanga na kubeba madumu ya maji, ila ghafla umeoa basi umegeuka mtotoo huwezi hata kusogeza maji ya kuoga bafuni🤪. Ila fresh tu tunawapenda hivo hivo watoto wetu.
Wewe uko matured ndiyo maana unajitambua.....sasa kama huwezi kuingia jikoni hata jmosi au jpili au ukipata nafasi..mimi nikuoe wa kazi gani kama kugegeda naweza kugegeda popote?
 
Nimesoma malalamiko ni mengi humu! Nimeoa hao wasomi level ya masters nani mtumishi wa shirika fulani la serikali nani boss kwenye ilo shirika namaanisha ni wale wakuendeshwa na v8 ma safari kibao lakini niwe mkweli, msichana kiumri ni mdogo ana 32 mimi 36 na mimi sina elimu kama yake ni kijana wa form 6 na nina biashara zangu hapa mjini lakini naweza kusema huyu mke ana nizamu sijawai kuona... Tuna dada wa kazi na mtoto mmoja lakini anaamka sa 11 anandaa chai na cha mchana ndo anaondoka kwenda kazini na jioni lazima aulize mume unataka kula nini....

Tukiachana na hayo sijawai kuona hatimizi wajibu au kinivunjia heshima na ndoani huu ni mwaka wa7!!! Nafikiri kabla yakuoa chunguza uyo mwanamke na anapotokea yani familia yake... Kuna kitu tunasahau nacho ni ushamba! Usiombe kukutana na mwanamke hajui alafu ajifanye anajua au mwanamme wa style hiyo na Hawa ndo wanaitwa wajuaji kwenye ndoa lazima pawe pamoto....!!! Maisha ya ndoa haya husiani na elimu zenu au kipato ila mmoja akiwa vizuri anamuinua mwengine na maisha yanaenda safi!!! Men achana na kuwaza visenti vya hawa wakina mama maana unakuta kamshahara ni ka million 1.3 ila iyo jeuri ni balaa...

Tafuta Pesa yako kama mwanaume tunza familia kama baba kuanzia mke mpe pesa za shopping yake na watoto nyumbani vyakula viwepo vyakutosha sio maharage tu jaza nyama, samaki, kuku weka vile vyakula wanavyopenda nyumbani kwako na ukipata time weekend ingia jikoni mwambie mke leo nyie pumzikeni jumapili napika mimi baba andaa chakula kula mle vyombo dada atamalizana navyo....

Jioni aga mke naenda kuangalia mpira mama nitachelewa kidogo ndo time yakujiongeza sasa hope nimeeleweka hapo!!!!... Hutokaa usikie kelele tatizo hawa tunataka kuwafanya kama beki 3 na ilo ndo tatizo ila mimi pamoja na yeye ana kibunda ila anajua akifika kwangu mimi ni mume na anakuwa na adabu zote
kwa kuwa wewe ni Marioo hii imewezekana kuingia jikoni na kupika ... lakini umezidisha chumvi kwamba naye anajishughulisha kiasi hicho mara akishashuka toka kwenye V8......hapo unagongewa live au ni chai
 
Wewe cariha inaonekana ushapigwa matukio mengi na hujawahi kua na mahusiano yenye amani kaa chini jiulize..! Hayo yote unayo ongea hum kuhusu wanaume kamwe huwezi pata Mwanaume wa hvo ..! Kama utampata wa hvo inabid ustuke atakua na mapungufu..! Sio unyanyasaji Ni uhalisia wa Mambo
Huyo cariha bado mtoto hawezi kuelewa hizi mambo
 
Nkamu wanaume wa JF huwa wananishangaza!!

nimetoka huko nimechoka nianze kuhangaika na masufuria, kwa kweli mimi sipiki weekdays.

Ila Jumamosi na Jumapili naingia jikoni vizuri tu.

Kikubwa funga ndoa na rafiki yako, funga ndoa na mtu anaekuelewa na unaemuelewa...mbona ndoa utaiona tamu.
sasa wenzenu hawataki kabisa kushughulika hata weekends....halafu mnawatetea humu,,,,muda wote kwenye TV,iPad nakuongea English ndeefu za ki corporate kwenye simu
 
Big up Karucee ni ajabu mwanaume kulia lia eti amekosea kuoa, mwanaume mwenye akili timamu hawezi kukose akuoa
endelea kujifariji lakini nawausia vijana ambao hawajaoa kuna wanawake si wakuwaoa hasa Corporate ladies,,mtakuwa veeery disappointed!unless uwe tayari kwa mashindano yasiyoisha au uende kulelewa..lakini kama unajiweza na unajielewa ...BIG NO!....hawa ni wa kuwapitia tu na kuwatupia kule
 
[emoji23][emoji23][emoji23] unajua tuanzishe kampeni ya kusaidia Hawa wanaume wetu hata kwa michango maana Wana vunja ndoa Kwa vitu vya kijinga kweli kweli kisa uchumi duni tu, Hali inayowapa makasiriko mengi
Hakuna mwanaume anayejiweza atakaye kuoa wewe kama hata chai huwezi andaa,kitanda huwezi kutandika hata siku za Jumapili ,...sawa kuna vitu vingine ataweka vya kurahisisha kazi kama washing mashine nk sawa lakini tatizo mnataka kushindana na wanaume wakati mnakojoa mkiwa mmechuchumaa...mambo mengine ni ya kimahaba zaidi
 
Baba yangu hakuwahi kuishi kama mlemavu.
Nawashangaa watu humu mnaishi kama walemavu.
Hili ni kosa kubwa lingine hasa kwa mafirst born daughters......kila kitu atafananisha na alivyokuwa baba yake kwamba alikuwa anapiga pasi mwenyewe,kufua,kudeki nk.......hapo ndoa lazima iichungulie kaburi
 
Wanaume wa kiafrika tu ndio wanafikiri wana haki ya kuwapiga wanawake. Inabidi tuchukue sheria mikononi. Imagine, niko na very beautiful daughter. Sijawahi kunyanyua mkono wangu kumpiga hata siku hii moja. Halafu arudi nyumbani na red aye? Oh my boyfriend did this. I think I'm going to shoot your ass
bora arudi na mimba🤣😂
 
Hivi mi nimbully a real gentleman kweli si nitakuwa mwehu!
One of my boyfriend was so cool and humble, yaan ilikuwa hata nikifanya kosa huko naona kabisa moyo unaniuma kwa hicho kitendo, ntaomba huo msamaha na ntahakikisha sirudii tena!

Mwanamke akikutana na mwanaume mstaarabu huwa anajistukia sana!amini nakwambia
Bila ya yeye kuwa na Hela utambembeleza hivyo?
 
Ukiwa na pesa moyo una furaha hukasiriki mkuu, na sio kumalizia wake stress
unazungumzia gheto style love life....lakini siyo kuishi chini ya paa moja kama wanandoa, ...yaani we mke unayesubiri kugegedwa tu? wakati papuchi zipo kila mahali?
 
Back
Top Bottom