marrykate
JF-Expert Member
- Mar 4, 2012
- 733
- 443
wanaume
wanaume hawajasoma hiii post.wanavyopenda kua budiwa na kutreat wenzao bila huruma
Hili swala mume kufua na kupika naona ndiyo limekua kero kwa waume wengi!!
Waliolelewa familia za watoto wa kiume tu, nadhani hii siyo ishu sana. Lakini pia linaendana na tamaduni za makabila mbalimbali Mfano Wakurya, Wamasai (halisi) hawa ni ngumu sana kugusa kazi zinazoonekana za wanawake.
Tabu ni kwamba mambo yamebadilika!! Maswala ya kijinsia na majukumu yake yamekuwa ni maswala ya kiushindani na kubishana, mwisho wa siku hakuna tena maelewano na tunaishia kuachana!
Mmoja asipoona thamani ya mwingine katika familia, tabu huanzia hapo!! Kikubwa ni kila mmoja kuhakikisha thamani yake inaonekana pale anapoishi iwe ni mama wa nyumbani au mfanyakazi.
Kama wewe ni mvivu kAma mimi, nunua vifaa! Vacuum, dish washer na washing machine nA huku una rice cooker,deep frier ma pressure cooker umemaliza kazi za ndani 🤣🤣🤣🤣
Kuishi na watu ni kipaji!! Amini hili nawaambia!! Wengine tulioa wanawake wasiojua kupika wala kufua na watu wakazodoa mke gani mke gani lakini leo hii ndiyo mke bora kabisa na mama bora kwa familia na jamii inayotuzunguka.
Kwa sababu gani? Nilijua nataka ndoa ya aina gani, nikajua mke gani atanifaa, na nitampatia wapi! Na tangu mwanzo nilimjenga vile nataka kikubwa ni kwa heshima na kumpa thamani yake kama mke. Huwezi kuelekeza jambo mke kama unatoa order kwa wafanya usafi wa ofisini kwako.
Shida ni kwamba hata wewe unalea, je unamlea mwanao wa kike kuwa mke bora au kuja kuwa na maisha bora?? Unamfundisha kupika, kudeki na kufua? Unamfundisha kuheshimu mume? Au nawe ndiyo kama mie mtoto ana miaka mitatu ushampeleka boarding? Atayajua mambo ya familia lini?? Wapi? Unataraji atakuja kuwa mke bora?? Kwa nini uyabeze malezi ya mwenzio (malezi ya wakwezo)??
Kikubwa: Kuheshimiana na kupeana thamani kwa kila mmoja, kwa vile alivyo na kurekebishana. Kuchukulia mapungufu ya mwenzio as part of you.
Mwisho. Ndoa unai fold wewe unavyotaka iwe toka day one mnapokutana! Usitarajie mlikutana KFC mkafungia ndoa huko, miaka mitano ya mwanzo mnashindia take away za huko mwaka wa sita akuelewe ukimpa ugali ndondo!!
Haiwezekana, siku ya kwanza ya outing mpaka uchumba wenu mkeo akitaka kuchangia mnapokuwa na jambo unakataa kwa dharau halafu ghafla utake mishahara yake!! Utadai talaka tu, maana hawezi kukupa.
Akija kwako unafua na kudeki ye anacheki muvi ukimaliza unampanda viwili mnatoka outing! Then kesho keshokutwa unamuoa unataka akakupikie na kukufulia, umelogwa?
Narudia tena: Aina ya ndoa unayotaka unaijenga wewe mwenyewe toka day one, unapolazimisha ibadilike kwa nguvu baada ya miaka kadhaa ndipo mnavunja ndoa zenu.
NB: Chagua mke au mume unayeendana nae, usituletee tabu, ndoa tamu
wanaume hawajasoma hiii post.wanavyopenda kua budiwa na kutreat wenzao bila huruma