Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

📌
 
Nime-assemble hapa 'assembly point' nikiendelea kuishi kama nipo ndotoni kwamba nikiamka ntakuta mambo yamebadilika na kila mtu ameshika njia yake anaishi maisha yake.
 
Hela ya dharura ndio imeenda kutafutwa acha upumbavu basi! Sio kila mtu ni kama Mwigulu nchemba. Namuone huruma sana atakaejichanganya kuleta posa hapo kwenu
Hahahaaaaa mkuu anaweza akawa na dada zake wengine labda huwezi jua. Hii ya kusema utashangaa kama posa itapelekwa kwao sio sawa mkuu. Kwani wa kupelekewa posa kwao ni huyu tu?.
 
Hicho ni kizazi cha mwisho mwisho ambacho upendo ulikuwa bado wa moto. Hiki cha sasa upendo unazidi kupoa kwa kasi. Hizi ligi za kipumbafu ni matokeo ya Upendo kukata moto. Asante Yesu kwa kuja.
 
Dah kweli mkuu yani kuna vitu havi make sense! Nashukuru kabisa huwa mwanamke naangalia mengi yani asiwe mtu wa makundi yani[emoji28] nimefanikiwa kwa 90% ya vigezo navyotaka toka kwake!

Huyu Karma ningekuwa napiga kila siku hadi ujinga umtoke!
Kumpiga nako ni kupoteza energy tu.
 
Adabu ipi ndiyo uielezee hapo! Yaani lets say majukumu yangu yote nafanya vizuri tu sitaki ushike chochote ila pia pesa zangu hugusi hata uwe na shida gani hapo unanipigaje yaani kwa mfano ndiyo nataka unieleweshe hapooo!
Mtalumbana sana. Shida ni kile Yesu alichosema akiwa hapa duniani alisema "upendo wa wengi utapoa". Hayo maisha ya kuviziana ni matokeo ya kutokuwepo upendo. Kiini cha tatizo ndio kishughulikiwe.
 
Mwanaume wa hivi simtaki kwa kweli....yaani nirudi asubuhi ukae kimya? Mwanaume Bwege hapana kwa kweli.
Hapana,wanaume wa hivi wanaitwa "surprise". Wanaishi kwa kufanya mambo ambayo pengine hukuwahi kudhani kwamba anaweza kufanya. Ukiona umeanza kumuona zuzu aisee anza kujiandaa.
 
Hapana waoane tu ila waongozwe na upendo ili kuepusha ligi za kipumbafu.
Ligi hazijawai isha mkuu...

Vijana haraka ya ndoa Contena,,,wakati wana uvumilivu kiberiti,, Kiburi Dunia.

bora wasioe tu,,ndoa nyingi zimekuwa sio mifano ya kufundishia
 
Ligi hazijawai isha mkuu...

Vijana haraka ya ndoa Contena,,,wakati wana uvumilivu kiberiti,, Kiburi Dunia.

bora wasioe tu,,ndoa nyingi zimekuwa sio mifano ya kufundishia
Kama ndio wapo hivyo na hawataki kuacha hizo njia zao mbaya,kwa kweli wawe wapo wapo kwanza.
 
Vizuri sana, pia huwezi toka kazini uanze kumpa mtu unyumba wakati wote mmeenda kazini, housegiel ndo atafanya kazi hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…