Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Kuna point zinachekesha sana kwenye huu uzi.

Mkishasikia tu mwanamke anafanya kazi, tayari mnasema anahusika kwenye mambo ya uchumi wa familia, hehehehe!

Babilai, anaweza kufanya kazi na usione hata shilingi mia kwenye matumizi ya familia. And ofcourse sio lazima umuulize maana as a man, ni majukumu yako kuwa provider. Ila shida kubwa ni moja....!!!!

Kama mwanamke hachangii chochote kwenye uchumi wa familia at least awe submissive. Kwa sababu akiwa na kiburi equation haiwezi kubalance kamwe. Mwanaume huwezi kujitoa ku provide kila kitu kwenye familia halafu mwanamke hataki ku bow! You women, it will never work..!!

Ila Mwanaume kama na wewe umekubali Mama awe anachangia pesa ya kula hapo ndani na gharama zingine kama ada za watoto unamuachia alipe, My Friend, usije kulalamika huku. Hatutakusaidia kitu. Hapo umesha sign 50/50 rule automatically. Kwaiyo zamu yako ya kuosha vyombo ikifika nenda tu kaoshe, tena ving'ae.

Poleni wote mliokosea kuoa/kuolewa. By the way sisi ni Binadamu bhana, kukosea ni kawaida.Tujipange upya : )

Cheers!
📌
 
Nime-assemble hapa 'assembly point' nikiendelea kuishi kama nipo ndotoni kwamba nikiamka ntakuta mambo yamebadilika na kila mtu ameshika njia yake anaishi maisha yake.
 
Hela ya dharura ndio imeenda kutafutwa acha upumbavu basi! Sio kila mtu ni kama Mwigulu nchemba. Namuone huruma sana atakaejichanganya kuleta posa hapo kwenu
Hahahaaaaa mkuu anaweza akawa na dada zake wengine labda huwezi jua. Hii ya kusema utashangaa kama posa itapelekwa kwao sio sawa mkuu. Kwani wa kupelekewa posa kwao ni huyu tu?.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Dah mkuu umetoa povu mno.
Muheshimu mama yako huyo licha ya mapungufu yake yote.



Mimi nimekulia maisha ambayo wazazi wote wawili wanatafuta na mama anacontribute kwa kiwango kikubwa..yaani kuna muda unakuta mzee hana basi mama ndiye anaendesha familia na kusomesha watoto.
Alitoa kwa moyo na hakuwahi kuona kama anaonewa.

Kazi zilifanywa kwa kusaidiana...baba anaamka anakamua maziwa na kufagia uwanja,mama anafanya usafi wa ndani,anaandaa chai na chakula.
Wote wanaenda kazini.

Hata ikifika jioni mzee akiwahi,basi mtakuta amewasha moto,mama anakuja kuendelea.
Baba alifanya kwa moyo na hakuwahi kuona kama ni adhabu.

Kipindi mama amesafiri tukiwa wadogo basi mzee alikuwa anatupikia.

Sasa ninashangaa huu utaratibu ambao watu wamejiwekea wa kutaka kukaa tu kama walemavu.
Kiufupi sikuwa na wazazi wavivu.
Hicho ni kizazi cha mwisho mwisho ambacho upendo ulikuwa bado wa moto. Hiki cha sasa upendo unazidi kupoa kwa kasi. Hizi ligi za kipumbafu ni matokeo ya Upendo kukata moto. Asante Yesu kwa kuja.
 
Adabu ipi ndiyo uielezee hapo! Yaani lets say majukumu yangu yote nafanya vizuri tu sitaki ushike chochote ila pia pesa zangu hugusi hata uwe na shida gani hapo unanipigaje yaani kwa mfano ndiyo nataka unieleweshe hapooo!
Mtalumbana sana. Shida ni kile Yesu alichosema akiwa hapa duniani alisema "upendo wa wengi utapoa". Hayo maisha ya kuviziana ni matokeo ya kutokuwepo upendo. Kiini cha tatizo ndio kishughulikiwe.
 
Mwanaume wa hivi simtaki kwa kweli....yaani nirudi asubuhi ukae kimya? Mwanaume Bwege hapana kwa kweli.
Hapana,wanaume wa hivi wanaitwa "surprise". Wanaishi kwa kufanya mambo ambayo pengine hukuwahi kudhani kwamba anaweza kufanya. Ukiona umeanza kumuona zuzu aisee anza kujiandaa.
 
Ligi hazijawai isha mkuu...

Vijana haraka ya ndoa Contena,,,wakati wana uvumilivu kiberiti,, Kiburi Dunia.

bora wasioe tu,,ndoa nyingi zimekuwa sio mifano ya kufundishia
Kama ndio wapo hivyo na hawataki kuacha hizo njia zao mbaya,kwa kweli wawe wapo wapo kwanza.
 
Siwezi kutoka kazini nimechoka huko eti nianze kuosha vyombo, kupika Hadi saa nne kisa mume never on earth instead ya kutafta mtu afanye nihangaike tu Hadi nizeeke kwa kweli hapana, wote tumetoka tumeenda kazini nirudi nihangaike na yote hayo?
Maisha ni mafupi kujichosha na kazi mara kupika pika jamani Ili kufuraisha binadamu asiye na shukrani
Vizuri sana, pia huwezi toka kazini uanze kumpa mtu unyumba wakati wote mmeenda kazini, housegiel ndo atafanya kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom