Mnakoseaje kuoa wakati Mwanzo mlipendana,
mnapigiana simu usiku wa manane,
mnapostiana status na nyimbo za mapenzi.
mnaitana bebi,hakuna kama wewe duniani 🤣🤣
Mnaulizana kwa nini sikukupata mapema 🤣🤣
mnaitana majina yote Laaziz,ini mkalia nyong'o
Mnaleteana zawadi,kadi
Mnatoka out,mpk tunasema kweli wamependana na harusini tukaja,na michango tukatoa
Saiv mnalia lia mlikosea kuoa/kuolewa haya mambo hayataki mbwembwe oooh.Au Mlikua mnaigiza nini?Mambo ya kukimbilia kuoa bila kutulia yana madhara yake,
Ndoa nyingi za watu waliochelewa kuoa/kuolewa hua zimetulia sana
Ndio maana Mwanamke akiniacha hua simbembelezi arudi,Alieandaliwa na Mungu yupo.
Haya mambo Yanamhitaji Mungu zaidi kupita jambo lolote
Ndio maana mm mapenzi ya kupostiana postiana status naonaga ni ujinga 🤣🤣🤣🤣🤣
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Yaani watu wanataka ndoa/kuoa/kuolewa kuliko maisha halisia ya ndoa yenyewe,Mwisho wa siku kilio na kusaga meno
Wengine walioa au kuolewa ili kufurahisha au kukomoa watu
Ambao hatujaoa/kuolewa tumtafute Mungu sana na tutulize akili sana