Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Dah sikuhizi Hali imekuwa vice versa wanaume wanapenda kulelewa na wanawake wengi wana jishughulisha kutafta hela wanaume wao ni mwendo wa kubet tu, kwetu hata mtu ukitaka kuolewa wazazi wanauliza huyo mtu ana shughuli ya kumuingizia kipato halali na ni mzima kichwani, but unfortunately sikuhizi wanaume hawafanyi kazi na mahari hulipiwa na wanawake Sasa ukichangia na kutokujiamini kwa kukosa hela basi wanaume wanageuka toxic na kuanza kunyanyasa wanawake kila jambo basi Inakuwa dhambi kubwa
 
Shoga ukiona utumwa utasaidiwaaa
Me yoote tusaidiane lakini swala la usafi wake, kunyoa na K nitayafanya hadi kufa hata niwe nimechoka.
Weuweeee!!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji28][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji7]
 
Kuna wanawake wanalipa mpaka ada, wananunua chakula, hospitali matibabu ila mwanaume amekaa na tumbo anataka kuwa mwanaume awekewe maji.... SIJUI SERIKALI IWASAKE WAUWAWE. [emoji35][emoji35][emoji35]
Hapo ndo taabu bin balaa linapoanza,huyo me atagongewa,atadharuliwa n.k[emoji28]
 
Kabisa
 
Kwani mkienda kwa wadangaji mnapendwa basi?? Ndo maana ww uwe mchafu uwe msafi yeye anachojua kukuchojoa kuzamisha unlike chake....ila sijui hamuoniiii? Mabaharia mnafeli sana.
Haha... Ni nature tu mama, siyo kupenda kwetu. Sisi tunapenda wanawake wawajibikaji kama wewe, ila ndiyo hivyo hata tukiwapata nature inazingua.
 
Hukumpenda kweli toka moyoni ulimpendea hela na connection baada ya kuingia ndoani ukajua kuwa ndoa ni zaidi ya hela, ikiwemo bond and chemistry hapo ndio ukachaganyikiwa.

Pole na move on with life maana inferiority ilikuwa inakusumbua
Binafsi kupenda nilishasahau huwa naishi na mwanamke kwa ajili ya kulea watoto tuu ila in most cases sina mda na mtu ko mwanamke ndio anahangaika maana hata simfuatiliagi 😀😀..

Huyo jamaa anazingua ukikuta yamekushinda si unajitoa sasa usisubirie kesi wewe jitoe mapema mlee watoto.
 
Kwani wanaume "wanaofanya kazi" hawapendi wanawake wanaowajibika kwa kulea familia?
 
Duuhhh Pole sana , Wote wawili mlichemka.

Wewe ulichemka kwenye Kuprov uanaume wako, ukidhan Pesa au Kipigo ndio kinachomtuliza Mke ( nahili ulilikosea Toka mwanzo wa Uhusiano wako.



Kosa la Mwanamke "Kujifanya mtafutaji kiasi chakusahau Nafasi yake ndani ikoje ".



.. wanawake wa aina ya aliyekua Mkeo, ni wale ambao " Nina Pesa ,naweza kujimudu ,so what?"...IVO WEWE MWANAUME UNATAKIWA UUPELEKE MBALI ZAIDI UANAUME WAKO.

ILI AWE VILE UNAVYOTAKA AWE.


Mwisho...YANN MALUMBANO??? UKIONA HAKUFAI, ACHAAA
 
Ni kwa sababu hamjaamua kuishi kwa kufuata nature:
• Mwanaume ampende mkewe na kuhudumia familia
• Mwanamkee amtii mumewe na kulea familia
• Watoto wawaheshimu wazazi wao

Mkiishi hivyo ndoa itakuwa sehemu ya amani na ustawi, licha ya upungufu na udhaifu wenu.
 
Yeye ndo alikosea kuolewa na wewe.

Corporate women are not for the weak men.

Only Alphas can and believe me, a man can change a woman only if he is man enough.
Hao Alpha ndio wanaojiliza kwenu au wenye pesa? Maana hata akiwa na pesa godown Zima na mwanamke akawa mwalimu tuu kama ni jeuri hapo hakuna alpha na omega ataacha kuiona 😄😄
 
Kwani wanaume "wanaofanya kazi" hawapendi wanawake wanaowajibika kwa kulea familia?
Kila mtu anapenda responsible partner ila sikuhizi wanaume mnapenda kitonga na kulelewa sana, Sasa mtu akulee, akupe kila kitu wewe kazi yako kugegeda tu na yet akitoka kazini apinde mgongo kukufuraisha huku umechoka na unajua tu kazi huchosha, Kuna vikao vingi, kuandaa ma report plus stress mara za maboss yet akirudi nyumbani unataka ASI relax aanze kupika kukufulia na mikono eti Ili umuone ndio mke Bora, hayo maisha ya ujima na u primitive yaliisha baada ya vita viwili vya dunia.
I advise my fellow women kutafta wanaume wanaoendana kielimu na hata wanaojua mziki wa kazi jinsi ulivo maana, ukijfanya umeolewa na mwanaume umemuzidi elimu, huku yeye ni darasa la saba au machinga lazima hyo ndoa ife kifo Cha mende
 
Hapo kwenye kumpenda utafanyiwa kama Samsoni wa Delila na Adamu wa Hawa.

So long as kwa aina hii ya maisha sipungukiwi kitu kwangu naona ni raha tupu.Maana kuna familia naziona yaani mwanamke ni kukaa tuu na kula mwanamke ni kuhangaika mda wote si Kazi za nyumbani za uchumi wala kitaani
 
Mwanaume gani anaependa kitonga? Binafsi sitaki tuhela twa mwanamke ila nikitumia huwa narudisha but nataka nae awajibike kwenye vitu vidogo vidogo
 
"Pata hela tujue tabia yako"

Huyo mkeo hajabadilishwa na hela,position yake wala elimu yake,hiyo ndio tabia yake aliyokua nayo hata kabla hujamuoa ila aliificha tu ndio maana ulikua hujaiona,kuna watu wakipata pesa ndio unaziona tabia zao za asili,hata mtu akilewa hua anakua mwenyewe hasa,akianza matusi au kupigana sio kwamba anafanya coz amelewa,hapana ile ndio tabia yake ila hua anaificha but akisha lewa anakua out of self control.
 
Hata ukienda kwenye bucha ya samaki ukawaambia watoe matumbo na magamba bado yapo yanayobaki ya kwenda kumalizia nyumbani unapowaosha kabla ya kuweka kwenye sufuria. Hakuna bucha ambayo wanatengeneza samaki wa kufika tu na kuweka kwenye chungu.
Jamaa yangu huyo ni aina ya wanaume tunaopenda kukosoa na kutafuta makosa zaidi kuliko kusamehe na kuchukulia poa yaani ni smart man sasa hii huwa ni shida so ajitahidi kuchukulia poa.

Hata mimi Niko hivyo ila nimejigundua ,huwa naona baadhi ya mambo ambayo ndoa zingine wanaishi na kuridhika nayo huwa nasema mimi siwezi kwa hiyo huwa naona bora hata huyu wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…