amu! Hilo ndilo Tatizo la siku hizi. Kijana less than 30 years unakimbilia ndoa ili iweje? Tulipokuwa vijana, tulielezwa kuwa kabla ya kuoa lazima ujipange! Hata ukimuoa Samia lazima ujue kuwa wewe ni provider. Lazima ujipange kiuchumi na kijamii. Kuoa maana yake ni mwanaume kuwa head of household (angalia definition ya sensa ya mwaka kesho). Huwezi kuoa wakati wewe si head of household (yaani mwanamke anakuzidi elimu, kipato, umri na madaraka) huko si kuoa bali ni kuolewa. Utaoaje uishi katika nyumba ya mkeo - hapo yeye ndiye head of the household. Hii hali ndiyo
cariha anasema inachochea inferiority complex kwa wanaume hasa wanaolelewa.
Kingine acheni mawazo ya kizamani. Ukiwa unafanya kazi na mkeo anafanyakazi na anachangia pato la familia! Hapo uhead of household mnaugawana. Nyote ni wanaume ndani ya nyumba, hawezi kutoka job ati akupikie, never! Lazima muwe na housemaid na si ajabu mkawa pia na housegirl kwa ajili ya watoto. Kupika mama atapika siku anajisikia bwashee! Lazima umuone kama mwanaume mwenzio. Nitatoa mfano, mke analetwa na STL V8 nawe unaingia na Passo yako! Umwambie akuwekee maji ya kuoga? Jiongeze ili aone umuhimu wako. Ndoa tamu kabla ya kupata mtoto ila ni chungu baada ya Kupata watoto 3. Mwanaume ukioa jipange kujiongeza ili asije akakupita ukawa marioo