Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

kwani baba yake analala nae? yani ufananishe status ya baba na mume mbona jua na mwezi
Kwani kale kaujumbe ka kuwa utaachana na wazazi wako na kuambatana na mumeo huwa hamkaelewi vyema!

Baba anaposema amekukabidhi binti inakuwa ina maana tofauti ama? Kama utakaimu majukumu yote ya baba kuna tofauti gani?
 
Kwa attitude yako utaendelea kuwapata Mamarioo, ila wanaume wakubeba majukumu yao kuanzia kwenye uchumba mpaka kwenye familia wapo ila WEWE SI TYPE YAO ,unawe kukutana nayo ila ndio mwendo wa kusuuza rungu na kupigwa chini.
[emoji23][emoji23][emoji23]maneno ya kujifariji tu hayo kila mtu hupata mtu wa type yake tena kusuuza rungu ka wote tuli enjoy no problem at all, wewe ukila mua na kutupa maganda yake hyo inakuwa furaha kwa chungu ku enjoy, tafuteni wanawake mnao wa mudu, wewe dhaifu kila idara unatafta strong woman aliyekuzidi kila kitu, kuanzia akili, hela hadi dhambi Matokeo yake ni kulia lia humu JF
 
Wanawake wakogo hvyo wakshakalili kitu mpaka waje wabadilike ni muda sana.

Mfano unakuta mwanamke hajui kukadilia maji ya ugali ukimweleza atumie vikombe kupima hatak,familia ikipungukiwa watu bado ugali atapka kama kuna watu kibao
 
Ukiongelea hili unawaumiza wenzio ambao bado hawajaolewa aisee na hao watu kuwapata sio rahisi kama unavyoongea humu😅
 
kwa jinsi unavyoongea umri wako unaweza kuwa 40+ na kama sio hivyo basi makuzi yako ni kumuweka mwanaume mbele kuliko hata afya yako. kitu ambacho si kibaya ila leo hii mama zetu hawa hawa ukiwauliza kama ni kweli walipenda kusugua sufuria 24/7 jibu huwa ni hapana.
 
Wapo wanaume hawana shida mke akimzidi kipato.

Wanaume wanaojielewa...wanaojiamini...na wanaojua kuwa wao ni kichwa always......

Kuna wanaume wanapambana kuhakikisha si tu ndoto zao zinatimia...bali hata ndoto za wenza wao zinatimia....wanakuwa huru kwenye kipato


Ila kama ni hawa wanaume tia maji tia maji...hawajiamini...watataka always mwanamke asiwe na kipato....asiwe na kazi na kama anayo iwe ya kipato kidogo....hawa ambao hata kufua nguo hafikirii namna ya kubadilisha maisha anujue hata mashine ya kufulia... hawa ambao binti wa kazi akimwandalia chai tu anahisi binti anajua ratiba yake kuhusu mkewe.....

Itateseka sana.........


Kama ni coperate lady olewa na alpha males (in Karucee voice..... hawa wengine utaishia kuonekananuna kiburi jeuri na humuhudumii kwa kuwa tu ulibanwa na kazi yenye deadline binti wa kazi akapika chakula....(ika ndio hawa hawa wanaopangia hesabu mpaka mishahara ya wake zao)



Nataka kusema kitu kimoja


Kingine hakuna mwanaume anapenda mkewe amzidi kipato ikitokea ndo hvyo atakubali lakini wengi inakua shida plus mawivu na maugomvi.
So choose wisely mwenza wako,na Mungu awasimamie sana.
.
 
Utakavyoona wewe uko sahihi!lakini siko hukoo kumueka mwanaume mbele kuliko afya yangu!
Ila yapo na tunayaona na ndo yanayoendelea ktk maisha yetu ya kila siku...!!!
 
Mkuu oa mwanamke asiyeenda shule Ili awe ana kubeba mgongoni na wewe Binti zako usiwaendelekeze kielimu, wala kibiashara Ili waje kuwa wake wema
 
Labda ungewashauri tuu vijana wasioe kabla hawajipanga lkn sio kuwakebehi vijana walio na kipato cha chini katika nchi yenye asilimia zaidi ya sabini ya watu wasio na ajira rasmi tia maji tia maji.
Ameamua kukandia bana yeye mke wa balozi wa Ufaransa😅 nchini!

Vijana almost 70% hawana kazi rasmi wanaunga unga sasa hao wenzie anaosema wachague watu wenye hela matokeo yake wanakutana na hii hii 70% wanahairisha mpaka sasa wengi wameshafika 30 years old and still bila bila 😅😅😅
 
Haha.

Mkuu ni haki mke akirudi kazini aanze kazi za nyumba bila msaidizi yeyote wakati na yeye anachoka pia kutokana na kazi ?
Binti.....kuna vitu vingine mnazidisha....pamoja na kusaidiwa kazi na mabeki tatu bado mnashindwa hata kumalizia sehemu ndogo ya kazi
 
Ifike mahali mjue ndoa ni kuchukuliana.....

Mapungufu ya mwenza wako tafuta namna ya kuyabeba.

Mfano muajiri binti ambaye atakuwa vyema kwenye kupika. Na concentrate na stregth za mkeo.

Unapomjaza interest zako wakati si zake utaishia kuumia tu na kubeba mzigo moyoni.

Badala ya kutaka ajifunze ynavyopenda ajifunze chunguza yupo vizuri kwenye nini? Interest yake ni nini? Ndoto zake binafsi yeye kama binadamu ni nini? Umpush huko!!!
 
Binafsi sioni shida kusaidiana, endapo hatuna msaidizi, Ila kama yupo, ni jukumu la mke wangu kuhakikisha mambo yanaenda kupitia kwa msaidizi na yeye.

Sio sawa umemruhusu mke aamke saa 11 afajiri kwenda kazini, arudi saa mbili then aingie jikoni kupika just coz wewe ni kidume na yeye anatakiwa afanye kila kitu, sio sawa hata kidogo. Saidiane, tena mkiwa wenyewe saidianeni tu coz inaimarisha upendo.

Lakini pia sio sawa kumwachia dada kila kitu afanye yeye, yaani unamtuma dada kama gari bovu, njoo hapa, nenda pale, hata ukirudi hugusi watoto...NONSENSE!

Wote tubebe majukumu as familia sio ya mmoja, binafsi akiwepo dada sifanyi A wala B, natunza zangu bustani huko...
 
Mkuu oa mwanamke asiyeenda shule Ili awe ana kubeba mgongoni na wewe Binti zako usiwaendelekeze kielimu, wala kibiashara Ili waje kuwa wake wema
Si wanawake wote ambao wameenda shule ni feminists wala si wanawake wote ambao hawajaenda shule ni wives material.

Tutaoa walioelimika na wanaojitambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…