Hapana mkuu huyo dada yupo sahihi kabisa,hili jambo haliwezekani kwa wanawake wengi.
Kwa wanaoweza acha wafanye,kwa ambao wanashindwa wasibezwe kwa sababu ni kweli na wao wanachoka.
Imagine mke mwalimu anarudi labda saa tisa kazini,akifika nyumbani kachoka hapo aanze kufua,kupika,kuosha vyombo huku wewe baba kama baba au mume umetulia kwenye sofa unachati jamii forum ukiwa na soksi miguuni zenye vitobo vimetafunwa na panya unasubiri kula.
Hii haikubaliki,nenda kamsaidie mkeo kazi kwa sababu wote mumetoka kazini.
Wanaume wengi wakitz bado tuna umwinyi sana na upuuzi flani ambao hauna maana yeyote,kwanza hizo kazi sio lazima kwa mwanamke kufanya kijamii tu ndio kwa kuwa wanawake wengi ni watu wa nyumbani ndio imeonekana ni kazi zao.