Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Hakuna mwanamke asiyependa kumdekeza mumewe apatapo nafasi, ila inategemea kwa mama mfanyakazi kama atapata muda jioni ni vizuri kupika na kumtengea mume ila ikitokea amechelewa kurudi labda , mume amuelewe na asicomplicate maisha kama dada yupo basi atasaidia kupika, ila mimi sitopenda dada amsevia mume wangu chakula ntajitahidi nimsevie mwenyewe ama ajisevie mwenyewe.

Ila on weekends kupika ni lazima mama mjengo nioneshe maujuzi jikoni harufu nzuri nyumba nzima hadi baba mjengo aseme leo kaingia mama mwenyewe jikoni rahaa.😀

Ila wanaume nyie mnadeka sana eti tuwatengee chakula, maji ya kuoga wakati mlivokua single mlikua mnasugua hadi sufuria na michanga na kubeba madumu ya maji, ila ghafla umeoa basi umegeuka mtotoo huwezi hata kusogeza maji ya kuoga bafuni🤪. Ila fresh tu tunawapenda hivo hivo watoto wetu.
Single vs kuoa ni vitu viwili tofauti na kufanya hayo sio hisani wala kudekezwa ni mandatory kwa mwanamke kufanya so long as umeolewa unless uniambie umeolewa Ili iwaje?
 
Yani upendo unapimwa kwa kubebesha mkeo ndoo bafuni, sijui kupika, sijui nini, kwangu Mimi naona huo sio upendo ni ujinga au naishi na partner asiye elewa nini maana ya mahusiano, love ya vi condition ka hivo sio true love hiyo, maana kupika mbona na ma chef wa kiume ni wapishi wazuri ina maana nao wapewe upendo.
Jibu swali ,upendo unapimwaje sasa? Unaolewa na huwezi fanya hayo Ili iwaje? Yaani nioe halafu mwanamke ashindwe kufanya majukumu ya ndani hapo naoa Ili iwaje?
 
Inaonekana huyo mkeo alikuzidi Elimu na kipato.! Ni hatari sana mwanamke akuzidi hivi vitu na akuheshimu kama mume.!

Ndio maisha move on.!
Anaweza akakuzidi elimu ila asikuzidi akili na maarifa
 
Na hivyo alikuwa anampiga! Mwanaume anepiga mwenza wake hajiamini, so anajaribu kumuonyesha kwamba Yuko juu. Sasa anaenda kukutana na mabazazi na anajua hajamuonyesha kumpenda na kumthamini. Lazma awe roho juu [emoji16][emoji16][emoji16]
Mjomba alikua akifikiria dinner meeting za kila siku anaona kabisa mama huko alikokua wakurugwa wameshamkula wife [emoji1787][emoji1787]

Sent from my MI 8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kuna jamaa yangu yeye mpaka alijihisi ni hanithi kumbe kamchoka mwanamke wake aliyekuwa na kiburi, hila, ujeuri na dharau, of recent kila akikutana naye kitandani baada ya kuwa pamoja kwa miaka kumi ngoma haidindi kabisa ila akienda nje anapiga mashine mchepuko wake hadi unakimbia unaacha chupi kwa msela.
Michepuko ishawaroga huko hata akili haifanyi kazi tena.
Hakuna mwanamke asomheshimu mwanaume wake, ukiona hauheshimiwi ujue wewe ni jipu haustahili heshima.
 
Nabii Isaya aliyaona haya......... ukisoma comments za humu hili andika linaenda kutimia.

Wakati huo wanawake saba watamvamia mwanamume mmoja na kumwambia, “Chakula na mavazi tutajitafutia wenyewe, lakini wewe utuondolee aibu yetu, uturuhusu tuitwe kwa jina lako.”
 
Mimi kupata unyumba hadi yeye atake , kuna kipindi alinipiga desh wiki 2 , bac siku aliyokuwa na hamu , alianza kujichekesha toka dinner, mapema akaenda kwa bed [emoji2922], nami nikasema ngoja nimuoneshe nami nikawahi kwa bed nikalala nikampa mgongo , akajiongelesha wee mi nikajifanya nakoroma , hadi asubuhi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], dah hizi ndoa hizi
Kwanza mimi biashara ya kujifunika shuka moja kukumbatiana na kugusanisha matako siwezagi ,ukiona nimefanya hivyo ujue ni siku ya mechi otherwise biashara za kutiana kila siku siwezi.

Nikisogelea mwanamke akizingua huwa silazimishi natafuta mchakato wa nje mpaka atakapokuwa tayari so naweza maliza hata mwezi na wiki kadhaa sijasex na wife na hakuna shida tulishazoea hivyo toka kitambo .
 
Sijaoa ila naishi na pepo juzi nmesafiri tu kauza Friji narudi nauliza naambiwa nmeongezea naagiza cm hiv ndugu zangu ni sawa ..nahitaji kuanzisha Uzi ili mnipe ushauri wakuu...sijui niendapo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Safi sana.
 

Siyo kweli kwamba huyo mwanamke ni multiple human being awe anaacha ya kazini a nafanya ya nyumbani!?

Yaani mnataka tushirikiane kwenye mambo ya kuingiza pesa and at the same time tuwafulie and every thing 100%?

Wewe mwanaume na nguvu zako unaweza kufanya kazi zako za ofisini na kisha kutimiza majukumu ya nyumbani?
 
Tujaribu kuvaa uhusika wa wanawake tutaona ugumu wanaopata.

Au wanaume tujifunze kuwasaidia kazi wake zetu tunaweza angalau kuona ugumu wa kazi hizo.

Mimi nakumbuka wakati wife analea mtoto wetu mchanga hatukuwa na binti wa kazi nilikuwa naamka saa kumi kasoro nakosha vyombo,nafua nguo,nadeki,nasafisha jiko,napika chai,natia maji chooni ya kutumia then saa mbili nakoga naenda kwenye ishu zangu,yeye wife anabaki anapambana na mtoto.

Tulikiiishi kipindi hiko bila binti wa kazi,lakini hizo kazi zote ningemuachia mzigo ungezidi kuwa mzito.
Ingekuwa kuna ugumu kuliko majukumu ya mwanaume basi makaburini kungejaa wanawake,sasa ni wengi lakini wanaume wachache wameyajaza makaburi.
 
Tatizo ni wewe mkuu sio mkeo.

Kwa karne hii ya 21 mkuu mkeo ishi nae kama demu wako,ishi naye kama rafiki yako na usiishi na mkeo kama mke wako.

Kuishi na mkeo kama demu wako maana yake mnaweza kupiga stori za nje ya mapenzi pamoja kwa muda mrefu mkiwa katika interest moja,sio muda wote mapenzi tu,hakuna maisha ya muda wote mapenzi tu,mapenzi yana muda wake na maisha mengine yana muda wake.

Dunia ya sasa sio lazima mkeo afanye kazi za ndani yeye,unaweza kumsaidia au mkafanya pamoja au ukatafuta mfanyakazi afanye.

Sio lazima yeye apike,tafuta mfanyakazi apike yeye.

KAMA MKE ANAENDA KAZINI KAMA WEWE NA ANARUDI BAADA YA MASAA KADHAA KAMA WEWE BASI ACHA HUYO MKE AWE KAMA WEWE tu yaani asifanye kazi za nyumbani kama ambavyo wewe hufanyi unaporudi kazini.

Kusolve jambo hili ungekuwa ukirudi kazini unaanza kummotivate wewe unamuambia wife mimi nafanya kazi hizi wewe fanya kazi hii,ili aone kwamba inawezekana kurudi kazini na kufanya kazi.

KWA MAANA NYINGINE TU NI KWAMBA SIO LAZIMA MKE KUFANYA KAZI ZA NYUMBANI,KUNA KAZI MOJA YA LAZIMA TU KWAKW KUIFANYWA KUIFANYWA KUIFANYWA.
sijui kama watakuelewa wanaume wenzio
 
Hafu hayo mambo I grow to see my parents hata watu wengine wanaume kujifanyia vitu vingi wenyewe tofauti na wanaume wa humu wanaopenda umwinyi, kwao upendo ni kumutumikisha mke ka punda wa dobi badala ya kumsaidia, ulezi wa watoto tu huwa ni kazi ngumu bado kuachiwa mambo mengine.
Dah wanaume kuweni na huruma na sisi huwa tunachoka tunahitaji kusaidiwa
Kati ya mwanaume na mwanamke anayetumikishwa ni nani hapa Duniani? Kutimiza wajibu wako ni kutumikishwa? Si Bora uishi mwenyewe sasa.
 
Wadau,

Nimekuja kugundua nilikosea kuoa baada ya kukaa kwenye ndoa miaka 15 na kupata watoto wanne. Dah nilijichanganya nikaoa a Corporate lady ambaye alikuwa mwanasheria kule Arusha, alikuwa ana vihela flani na connections za watu wazito ndani ya bongo....duh acha kabisa!!!

Nilikuja kujuta sana manake kazi zoote na mambo yooote ya nyumbani yalikuwa yanafanywa na mabeki tatu kuanzia Kufua nguo zangu, maji ya kuoga, kupika nk alikuwa hana time kabisa na nyumba yake. Hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake kila kitu anabishana na kushindana.

Mtu wa vikao vya dinner karibu kila siku. Miaka ya mwanzoni nilikuwa namdunda sana sana baadaye nikapataga kesi, wakati mwingine ilibidi niingie hasara ya kumpeleka hospitali na kumhudumia manake alikuwa na watoto wadogo.

Nikaamua kuingia kwenye pombe na michepuko ili nimpuuzie. Nikawa nampuuzia kama vile hayupo na yeye akanikazia, akazidisha kiburi na jeuri nikaanza tena kumdunda nikapata tena kesi kubwa manake ilikuwa nimuulie mbali.

Sasa baadaye nikafikiria sana watoto wangu tukafikia hatua ya kuachana na kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto. Sasa tumeweka nguvu zoote katika kuwalea watoto na hali imekuwa shwari kabisa kila mtu anaishi kivyake baada ya talaka.

Najua kuna wale watakaosema tuishi nao kwa akili. Nilijitahidi kufanya hivyo kwa miaka 15 lakini ikashindikana manake ningeishia jela baada ya kumtoa uhai na watoto wangeteseka.

Bora iwe hivi hivi wote tupo wazima wa afya.

ALAMSIKI, DUH USIOMBE KUKOSEA KUOA BORA UKOSEE KUZALIWA

KARIBU NI WADAU WENZANGU MLIOKOSEA KUOA.
huyu mkeo mvumilivu sana, huwezi pat mwingine kama yeye hicho kipigo kwa miaka 15 alikivumilia kwa sababu zipi yaaani.

can you please list them.

ni kitombo tu au nini mapaka akawa tayari kufia hapo kwako.
 
Kwamba wanaume wanaofanyiwa hayo yote ndiyo hawachepuki siyo? Wanaume mnajulikanaga hamna shukurani siku zote na ndiyo maana siku hizi hatutishiki na hizo kauli zenu za sijui kupandisha mke cheo, sijui kutembea na beki tatu kisa ndiyo anakufanyia kila kitu maana tumeshashuhudia ndoa za wake wanaofanya hayo yote kwa waume zao, na bado wakapandishwa vyeo au kusalitiwa na hao mabeki tatu kama kawaida sasa sijui mtatuambia nini asee!
Chochote unachofanya sio favour ni wajibu wako na mwanaume anatimiza wajibu wake.
 
Back
Top Bottom