Walaa sina sifa zote hizo, Nina mapungufu yangu Ila nashukuru huyu Baba anajua kunichukulia, mfano huyo mdau aliyelalamika mke hawezi kusafisha kuku, Mimi nimezaliwa mazingira ya kimasikini, nimekua sijui kunyonyoa kuku wala kumkatakata, ukitaka kuku unaenda sokoni unatengenezewa...
Nimeolewa tumeenda kuishi mkoani hakuna huduma ya kutengenezewa kuku, Ila mume wangu alikuwa ananyonyoa, anamkata na atamchemsha...Mimi ataniachia kumuunga mchuzi....so unaona udhaifu wangu kaubeba, tumeepusha vinyongo.