Hujajua dhana ya kuishi wewe, unawaza kirahisi mno kuliko uhalisia wa mambo yenyewe.
Halafu sio kila mwanaume anayepiga kelele anaogopwa na kuheshimiwa. Kwa taarifa yako mke wangu hathubutu hata kufanya hivyo kwakuwa anajua kutouliza hovyo mambo ya kijinga kuna jibu lake.
Wewe unajua ni mke wa mtu unaweza vipi toka na kurudi asubuh bila taarifa? Unataka nikuulize nini hapo? Kuna suluhisho dogo tu hata mke wangu analijua vizur, ukifanya kosa la dhahiri usubiri nikuulize utaacha nifungwe kwa kuwa utanidanganya...Kwahiyo suluhu utaipata kwa waliokuzaa mimi siwezi kumhoji mwerevu aliyechagua ujinga.
Hata dini zimetupa suluhisho....rudisha mjinga kwao akafunzwe adabu huko, so hiyo siku mke wangu atafanya yale ambayo hayapo kwenye utaratibu basi anajua nini kitampata bila kumuuliza au kumfokea.
Chanzo cha mauaji ni kutaka kuhoji ujinga, tumeambiwa tuoane kwa wema na tuachane kwa wema.
Kuwa na msimamo kama kiongozi sio kupayuka hovyo na kupiga, ndio maana watu wanaojifanya kukaba kila kona ndio hao wanaishia kupigana na kuumizana. Na pia ukikurupuka kuokoteza madada ya mtaani ukayabadilishe yawe wake zenu jiandaeni kupigana tu. Mke mwema ni matunda ya familia bora, So tukaoea na kuolewa kutoka kwenye familia zenye adabu. Ukioa kwa baba na mama mkwe mlevi au mshirikina basi ujue umeoa wa mfano wao.