Wale tuliopoteza muda shule kusoma tukutane hapa

Sijawahi kuipenda shule wala elimu, sijawahi kuwa serious na shule wala elimu na kwa bahati nzuri sijawahi kufeli chekechea mpaka chuo kikuu. Mimi nilisoma civil engineering kwa shinikizo tu la wazazi na kwakuwa nilikuwa very bright class nikafaulu na baada ya kumaliza chuo vyeti nimevifungia kabatini napiga mbanga nyingine nashukuru elimu imeniongezea ufahamu na maarifa.
 
Pesa ni namna utakavyotumia hayo maarifa kuzitafuta. Ila hoja ya msingi jua, lengo la shule sio kupata fedha, bali maarifa. Ukitaka kufanya jambo ambalo linakupa fedha ya moja kwa moja kachimbe madini.
My friend, kuna darasa la saba kibao wako more financially stable kuliko maprofesa wengi hapa nchini so sijui unaongelea maarifa yapi.

Binafsi nafanya mitikasi yangu kariakoo, %kubwa ya wapemba, wakinga na wachaga ambao wanamiliki biashara kubwa hapa Kariakoo walikimbia shule.

What's the point of regarding yourself as educated person with different honors while you got nothing in the Bank man?

Which knowledge are you talking about specifically?
 
Walimu ndio kundi la watu waliopoteza muda shuleni. Nasubir kupigwa mawe
 
Huu ufafanuzi ndio umenisaidia zaidi hoja yangu kuwa lengo la shule sio kupata fedha au ajira.
 
Kwa upande wangu elimu imenisaidia vitu vingi
1.wakati Niko Chuo niliweza kudate wasomi na wasio wasomi Nikaweza kupata hints kidogo (ya utofauti wao) so now ni choice yangu aidha nioe msomi au nioe msomiless
2.Nikajifunza namna ya kuishi na wapangaji wenzangu wa rika tofauti tofauti
3.Namna ya kujibu kwa hoja Bila kukurupuka
4.Exposure ya biashara na fursa japo mchawi mtaji(nimeweza kujifunza pia kuwa ni namna gani mtu anaweza toboa akiwa mbali na home)
5.Huwezi kusainishwa mikataba ya kiboya kirahisi rahisi na kutumika hovyo maana unakuwa na critical thinking

6.mwisho kupata kazi ni majaaliwa kufanya biashara pia yataka moyo
 
Muda unaotumia kusoma na kujifunza huwa haupotei bure kuna kitu bora umeweka kichwani na unatofauti kubwa sana na mtu alikoswa Elimu. Kinacholeta utofauti kwenye kufikiri elimu haina tija ni kusoma ajili ya ajira badala ya kusomea maarifa na pesa. Elimu ni nguzo kubwa kwenye utambuzi wa mwanadamu na egemeo la fikira, ujuzi na maarifa, Elimu ni siraha inayozuia ujinga ukutenga na kutokujua na kukujaza ufahamu na kuweka umbo zuri la akili.

Soma, somea maarifa ya kujitambua na kuwa mjuzi mwenye kufikiri ili kujijenga kutoa suluhu na sio lawama.
 
Kbongo bongo elimu yetu haifundishi namna ya kutafuta pesa!na hilo ndio muhimu kitaa!!
Una uhakika??,unataka kusema Vyuoni watu hawasomi Business au Economics au Finance???
Na sio kila moja katika hii dunia some course za ku generate pesa,kuna wengine kazi zao ni katika kusaidia Jamii kama Madaktari,Walimu,Askari n.k
 
Umuhimu wa ELIMU ni mkubwa mno mtu mwenye elimu na asiye na elimu ni mbingu na ardhi...

Elimu itakupa kila kitu hata Kama hauto ajiriwa popote

ELIMU itakuweka HURU na hauto kua na EXCUSES kujilaumu kua hukusomaa

NB.
Elimu ni kile kinacho BAKIA KICHWANI BAADA YA KUMALIZA KUJIFUNZA 🎓

ELIMU ni kujikomboa kifikra na kuya tawala Maisha yako na mazingira yako..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…