Wale tuliopoteza muda shule kusoma tukutane hapa

Kama ulichosomea unaona huna faida nacho, kwanini usisomee kitu kingine ambacho utakuwa na manufaa nacho?
Unamkuta mtu kakata tamaa kabisa na hajui kama yuko depressed
Kama una hela ya kozi nyingine bora kusomea hata bwana mifugo at least utajiajiri baadae
Kwa kweli maisha ni fumbo hujui ya kesho ila tupambane sana
Sasa boss ukienda kijijini na gari la kuazima na suti wakikuuliza million
 
Mkuu nimejiajiri since 2022 hadi saiv nipo nakula airtime kilaini kabisa ingawa bado sijafikiria kununua usafiri sababu jamaa zangu wa karibu wanaonizunguka kwa sasa wanao so sioni shida kuazima. Muda ukifika ntanunua
Kama umenielewa vizuri ni kwamba najutia kupoteza muda A-level na Chuo, hakukuwa na haja ya kupita kwenye izo level ukizingatia lengo langu la kusoma ilikua nije kuwa CJ katika siku za usoni. Hii kujiajiri ni Plan B ambayo imetokea tu pasipo kutegemea.
ivi vyeti sioni kazi yake kwa sasa kuna muda natamani kuvichoma
 
Sijafungua uzi kwa lengo la kujilinganisha kimaisha na mtu ila kwa wanaonijua humu wanajua nilipo kimaisha. Thanks anyway
Hauko sawa kiakili
Simu unayotumia imetokana na watu kuwekeza kwenye research na sio hiyo gari, nguo unazovaa, tv unayoangalia zote hizo ni matokeo ya elimu sasa unavyosema elimu haina faida ni kituko kwa kweli
 
Hatusomi ili tuajiriwe ni ili tuelimike Kwani ni wapi shuleni watu wamekatazwa wasijiajiri au ni wapi kwenye elimu kujiajiri ni plan b

Matajiri wote hatakama hajasoma ila antumia wasomi kutengeneza fedha
Kwa Tanzania form four hana tofauti kubwa sana na mtu aliyeoshia darasa la saba
 
Nimekuelewa vizuri sana kwa ufafanuzi huu, ila hakuna anaejua ya kesho
Bado uko vizuri mshukuru Mungu
Elimu ni nzuri ingawa unaona ulipoteza sana mda
Ila kama afya ipo unaweza kupasua kwa njia nyingine don't give up boss
Kumbuka uaminifu ni silaha na kinga nzuri katika maisha
 
Elimu haiozi kamanda..
Nchi bado inafunguka.
Keep hoping.
 
Hauko sawa kiakili
Simu unayotumia imetokana na watu kuwekeza kwenye research na sio hiyo gari, nguo unazovaa, tv unayoangalia zote hizo ni matokeo ya elimu sasa unavyosema elimu haina faida ni kituko kwa kweli
We ni kichwapanzi sio? Huezi ata kutofautisha kati ya elimu unayoiongelea na elimu ya Bongo?
 
Kwa masomo mengi kuanzia A level na kuendelea vitabu vinavyotumika vingi ni vya wazungu alafu wanakuja wahindi.

Tatizo sio elimu bali ilaumu nchi yako ya Tanzania kwa kutoweka mazingira wezeshi kwa wasomi kama wewe sababu haiwezekani elimu hio hio unaoiponda nchi nyingine imewasaidia sana yaani elimu hiii wengine wanaitumia kuvumbua vitu vipya alafu useme ni mbaya hapana ndo maaana una shida au stress za maisha

Wewe uliyesoma ndo unatakiwa uje na solution ya changamoto zilizopo nchini na sio kulalamika ndo uvumbuzi uliopo na ndo ulipo anzia na ukija na solution utatengeneza na ajira pia kwa wengine ooh elimu haina msaada msaada gani unataka

Edelea kuamini hivyo sababu una-uhuru huo ila sio kweli na haitakaa iwe kweli
 
Acha kisomesha kama kunapoteza muda ikiwa unasomesha
 
Hauko sawa kiakili
Simu unayotumia imetokana na watu kuwekeza kwenye research na sio hiyo gari, nguo unazovaa, tv unayoangalia zote hizo ni matokeo ya elimu sasa unavyosema elimu haina faida ni kituko kwa kweli
Mnatakiwa kuelewa maudhui ya mada
Hizo simu na tv zinatengenezwa na digirii ya kwetu ya madesa au kuhonga ngono upate cheti?
Elimu ina faida kwenye nchi za hao waliotuletea huu mfumo, hapa kwetu ni tia maji unatakiwa ujiongeze,
 
Au wangenywea pombe
Maisha hayana elimu hakupa sehemu utakwenda kwenye kusoma maisha maisha ni fumbo gumu sana maisha ni kumtanguliza mungu na kufanya kazi na kwa maarifa Cha muhimu kama ni mtoto Haina haja ya kumsomesha sijui awe na PhD au awe sijui dokta asome kawaida aanze kupambana na maisha na ukiangalia asilimia kubwa waliofanikiwa wengi hawana elimu
 
So Sorry, sijaelewa umeandika nini
Ukikutana na watu wamekaa ajirani yupo 2nd floor somewhere hapo town na mawani yake anachezea computer chini ame-park Subaru au Vanguard ya mkopo ukimwambia Tanzania hii elimu haimsaidii yeyote hata akisema atoke nje ya alichosomea atumie akili ya darasani kujaribu kwingine atashindwa hawezi akakuelewa.

Labda kuwa dalali ndiyo ataweza maana huko hakuhitaji mtaji ila vingine vyote vinahitaji mitaji na ndugu wa kuwapa mitaji ni kama wao wakiwafuata kuwaomba mitaji wanawanyima still wanawaona wazembe,hao ukiwatoa kwenye ajira zao ukawaambia wafanye maisha nje ya ajira miaka mitano mingi unazika wote wengine watakuwa vichaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…